NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Saturday, January 10, 2009

MAISHA NI KULA NA KULIWA - LITERALLY

Picha hii imenivutia kwani inaonyesha jinsi msimbo tata wa maumbile unavyofanya kazi. Huu ni ulimwengu wa kula na kuliwa - literally. Siku ukienda Serengeti katazame vizuri - kila mnyama yuko kwenye harakati ama ya kumla mnyama mwingine au kuzuia asiliwe. Ni ulimwengu wa kula-kuliwa. Halafu kuna binadamu ambaye akilinganishwa na wanyama wengine kimaumbile ni kiumbe dhaifu sana - hana makucha wala meno makali, hana umbo la kutisha, hana ngozi ngumu kujikinga na hali mbaya ya hewa wala mashambulizi ya adui, hana harufu mbaya kuwakinaisha maadui zake wa kimaumbile wasimle, hana... Isitoshe binadamu ni mmoja kati ya wanyama ambao watoto wao huchukua muda mrefu zaidi kuweza kujikimu na kujilinda wenyewe. Hebu mlinganishe mtoto wa binadamu na mtoto wa swala ambaye humchukua si zaidi ya nusu saa kuanza kukimbia. Mbali na mapungufu yote haya binadamu ameweza kukwea mpaka kileleni kabisa mwa msimbo wa Ikolojia na maumbile kutokana na uwezo wake wa kufikiri. Uwezo huu umemwezesha kuwafanya wanyama wengine wamtumikie. Kinachoshangaza hata hivyo ni kuona jinsi binadamu anavyovuka mipaka ma kuutumia vibaya uwezo huu. Binadamu leo ni mnyama pekee ambaye anaweza kuua wanyama wenzake kwa sababu zinginezo mbali na chakula au kujilinda. Na wajanja wachache huweza "kuwala" binadamu wenzao kwa kuwanyonya na kuwakandamiza. Wewe uko katika kundi gani - linalokula au linaloliwa? Kama uko katika kundi linalokula wenzie basi kaa chonjo kwani mambo yamebadilika...Na wewe unayeliwa, utaliwa mpaka lini na hawa wajanja wachache?

1 comment:

  1. Mimi sijui kama ni mlaji au mliwa. Aisee prof, umeniamsha kweli. I have to find out....

    ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU