NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Saturday, January 24, 2009

MANABII WETU NA SAFARI ILIYOSHINDIKANA YA KUELEKEA NCHI YA AHADI

Baadhi ya sura hapa ni za manabii wetu wa kweli waliotukomboa (au wanaopigania kutukomboa) kutoka "Misri" yetu ya umasikini, magonjwa, dhuluma na kutuahidi kutupeleka katika nchi ya ahadi. Mbona safari yetu inaonekana kama vile imekwama? Bado tunazunguka jangwani au ndiyo tumeshafika walikoahidi kutupeleka? Wanakotupeleka ndiko? Je, nchi ya ahadi ipo? Kuna anayejua iliko?

3 comments:

 1. Blogu nzuri profesa. Ninafurahi kuona wanazuoni wanaongezeka katika ku-blogu. naomba niulize jambo katika post hii. Hivi Mugabe anastahili kuwamo katika watu 100 mashuhuri katika afrika?

  mwaipopo.blogspot.com

  ReplyDelete
 2. Amani, Hshima na Upendo kwako Profesa.
  Mara zote tafsiri za hawa MASHUJAA zinatokana na upande tuliopo ama tunaoamua kufungamana nao. Ni kutoka huko unakokuta hata shujaa anakuwa gaidi kama hatimizi matakwa ya "wakubwa". Kwani si twaona status ya Mandela ilivyobadilika bila yeye kubadili matendo? Aliyekuwa akiaminika kuwa GAIDI na MKOROFI akawa shujaa na Baba wa Taifa kwa kuwa tu "ulimwengu" umehalalisha juhudi zake. Mtu kama Gaddafi ambaye alisemekana kuwatesa wananchi wake na kuwaunga mkono magaidi na kuonekana kama gaidi fulani kwa kuwa tu amekataa kukaguliwa silaha za maangamini akaja kuonekana MWANADEMOKRASIA kwa kuwa tu ameiruhusu Marekani kuikagua nchi yake kuangalia silaha. Lakini anakuwa mwema hata kama hajabadili lolote kwa wananchi. Kwa bahati mbaya hata viongozi wetu wanachaguliwa nani awe rafiki na nani awe adui wetu na wanaendeleza propaganda hizo kwa wananchi wao. Naamini wako wengi zaidi ya 100 japo sina hakika kama hao wote waliokuwa wamewekwa hapo bado wanachukuliwa kama mashujaa. Nahisi kuna ambao wameshabadilishiwa status.
  Naomba kuwakilisha

  ReplyDelete
 3. Bwana Mwaipopo, Mugabe alianza vizuri sana. Ni lazima tukumbuke kwamba ndiye aliyeongoza mapigano ya kupatika kwa uhuru wa nchi yake na alikuwa kiongozi mzuri. Mambo yamekuja kuharibika wakati safari inakaribia mwisho ingawa pia watetezi wake wanasema kwamba ni kutopendwa kwake na "wakubwa" ndiyo hasa kumeharibu mambo - wakubwa ambao wanafanya kila wawezalo kuhakikisha kwamba anatoweka. Mzee wa changamoto umenena vyema - status mojawapo inayoleta utata ni huyu Mugabe. Bado ni shujaa au ameshageuka na kuwa msaliti. Kwa Marekani na Uingereza ni dikteta tena katili ajabu. Je, wananchi wa Zimbabwe wanamwonaje?

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU