NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Saturday, January 31, 2009

NIMEULIZWA SWALI

Prof. Nimefurahishwa sana na hiyo post ya wanafalsafa waliojitahidi sana kutuondolea hofu ya kifo. Swali langu kubwa ni hili: BILA KIFO KUNGEKUWA NA DINI?
Asante.
Edwin.
===========
Swali zuri na gumu ndilo hilo lishaulizwa. Eti jamani, kama tungekuwa tunaishi milele bado tu tungehitaji dini? Au dini zipo kama njia ya kutufanya tukishinde kifo - zikituahidi maisha baada ya kifo ama peponi au Jehanamu?

6 comments:

 1. Sina hakika kama comment yangu ya kwanza imefika maana imeonesha error. Lakini mtazamo wangu ni kwamba dini hasa za asili hazikuwekeza juhudi kwenye maisha baada ya kifo. Dini za asili zilikuwa zikijishughulisha na maisha ya sasa. Kuanzia maombi na matambiko kwa ajili ya watoto, mvua, mafanikio na mengine mengi kwa maisha tuliyonayo sasa. Huku kuwekeza zaidi katika maisha baada ya kifo kumekuja katika hizi dini za mapokeo ambapo sasa hivi tunajitahidi kuwekeza maisha ya sasa na hayo yajayo ambayo tunaamini yapo kwa IMANI (ambayo ni hakika ya mambo yatarajiwayo na bayana ya yasiyoonekana). Kwa hiyo kulingana na mtazamo wangu, bila kifo kungekuwa na dini za asili maana bado zinazungumzia namna ya kuishi na kufanikiwa sasa kuliko baada ya kifo.
  Ni mtazamo wangu na naalika changamoto

  ReplyDelete
 2. Kabla ya kufa ni vigumu kweli kuhitimisha maongezi ya KUFA:-(

  ReplyDelete
 3. mimi siamini kabisa kwamba kuna kifo au kufa kwa hiyo siwezi kujua kama dini zipo na sioni ni wapi dini zitanipeleka wakati hakuna kifo wala kufa bali kuna kuivua hii miili na kwendelea na mambo mengine nje ya mwili.kwa hiyo kama unaamini kuna kufa basi bado uko mbali sana kiroho!!!

  ndio maana Kristo alikufa, na mwenda mbinguni mwili wake ukazikwa harafu siku ya tatu akarudi kwenye mwili na kuondoka nao kwenda mbinguni na sas ni zaidi ya miaka 2000, usiniulize huo mwili huko unaishije wakati mwili ni mali ya dunia na mwili unategemea vyakula vya ardhini tu ili uishi yaani nafaka, matunda majani na maji, sasa wa Kristo sijui unakula nini kwa miaka 2000 sasa.

  hakuna kufa ila kuna kuuvua mwili wala hakuna mjinga, gaidi au katili atakayekuhukumu baada ya kufa. hukumu ni ujinga wa binadamu tu wa mahakama jela nk na sio kimaumbile.

  ReplyDelete
 4. Mzee wa Changamoto - ni kweli dini zetu za asili hazikumakinikia zaidi kifo bali maisha ya hapa hapa duniani. Katika matambiko ya kimila niliyohudhuria nilipokuwa mtoto kifo hakikutajwa kabisa ingawa tulijua kwamba waliokufa walikuwa hai na ndiyo maana tulikuwa tunatambikia kuwaomba watusaidie. Matambiko hasa yalilengwa katika kuondoa utasa wa mwanajamii, kuleta mvua, kuzuia majanga n.k. Na hii inaingia akilini kwa sababu kusema kweli maisha ya baada ya kifo ni IMANI ya mtu. Mchango mzuri sana Mulangira. Bwana Kitururu wewe ni mwanafalsafa uliyekomaa na katika blogu yako ni kawaida yako kuuliza maswali magumu-chokonozi. Pengine itabidi ukusanye post zako zote na kutoa kijitabu. Nitakuwa tayari kutoa msaada wa uhariri na mawazo. Tatizo hata hivyo Watanzania wengi hawapendi kujisomea na "kufikiri". Na Bwana Kamala nimeisikia pia falsafa yako kuhusu kifo - hakuna kifo bali kuna kuvua miili. Ngoja tumsubiri aliyeuliza swali tumsikie ana maoni gani. Tuendeleeni kubadilishana mawazo na kuimarishana kifikra, huku tukiipigania na kuionyesha jamii njia.

  ReplyDelete
 5. Naam. Tumsubiri aliyeuliza tuone kama ana majibu ama mtazamo tofauti wjuu ya hili. Maana kuuliza swali kunakuwa na utata kiasi na watu wakichangia wanaweza kusaidia kukupa jibu ama kuboresha mtazamo wako

  ReplyDelete
 6. Nitafanyiakazi ulichoshauri Profesa!

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU