NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Wednesday, February 11, 2009

LOJIKI YA KIZAZI CHA DOT COM

Haya ni maongezi ya kweli ambayo niliyashuhudia hivi karibuni. Wazungumzaji walikuwa ni wapenzi matineja - wote Waafrika. Binti ni Mchaga kutoka Moshi na mvulana anatoka Cameroon ingawa wote sasa wanaishi Marekani. Kilichonishangaza ni kwamba vijana hawa hawajui kabisa na wala hawajawahi kuona mnyama aitwaye mbuzi. Pengine hili si jambo la kushangaza kwa vijana wetu wa dot com. Kilichonishangaza ni hii lojiki katika mazungumzo yao (tazama hapa chini):

Binti: A goat is a lamb. And a lamb is like a sheep
Mvulana: A sheep, therefore, is a female lamb.

Lojiki hii ilinichanganya kidogo. Lakini hawa ni vijana wa kisasa ambao pengine ukiwauliza kuhusu chakula alichokula Britney Spears mwezi uliopita watakueleza kila kitu tena kwa kina. Kazi ipo!

7 comments:

 1. Nimekufikia,nimekukaribia, na sasa nipo hapa naandika. Karibu sana tena sana ingawa nimechekewa kukukaribisha mwanazuoni mwenzetu.
  Karibu saaaaaanaaaa.
  nimekuja kukutembelea hapa leo na itakuwa hivi daima

  ReplyDelete
 2. Duh mshikaji hii ni babu kubwa sasa. Mbuzi ni kama or mfano wa Lamb na mumewake akasaidia upupu kwamba Sheep ni female Lamb duhhhh kaziiiiiii. Warudi shule mazeeeee. Or warudi Africa for sure.

  ReplyDelete
 3. hiyo ndiyo dotcom, unaowashangaa nao wanakushangaa wewe katika jambo moja au lingine, basi ishu nikushangaana. hakuna wakati hapa duniani ambao kizazi kilichotanguliwa kitaacha kushaangaana na kizazi kilichozidiana nacho.

  ndio maana mimi namshangaa baba na babu yangu kuwa mkristo kwani mimi naona ukristo kama vitu vya ajabu na yeye ananishangaa kwamba pamoja na kunibatiza bila ridhaa yangu, kunipa kipaimara nk, sipendi kusikia kitu kama eti mimi nimyahudi (mkristo)

  ReplyDelete
 4. We kamala wewe. Acha uhafidhina usio na maana. Babu yako alikuwa anakutafutia wokovu na halafu wewe unaishia kumshangaa? Huyo Mungu wako wa Kihaya atakufikisha wapi? Siku ya hukumu itakapofika utalia na kusaga meno na kujuta ni kwa nini hukumsikiliza babu yako. Okoka sasa wakati ungali bado una muda!

  ReplyDelete
 5. muhubir mmoja alikuwa akihubirikwa kuwatishia wahumini wasio mpatia sadaka kwamba ni watenda dhambi na siku ya mwisho watalia na kusaga meno! basi kumbe nyuma yangu vilikaa viajuza viwili ambavyo haviina meno, kili kiajuza kimoja kikainama na kukiammbia chenzake kwamba "thithi tuthio na meno tumethevu" nikagundua kummbe siku ya mwisho ikikaribia tu, wewe ng'oa meno yako, huwezi kuppata taabu wala nini si huna tena meno ya kusaga?????

  ReplyDelete
 6. Asante sana Mheshimiwa Mpangala kwa kunikaribisha kwa moyo mkunjufu namna hiyo, Tayari nimeshaanza kupazoea

  ReplyDelete
 7. Kamala, hii stori ya viajuza imenichekesha sana. Sikujua kama hata komedi unaweza. Safi sana!

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU