NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Monday, February 16, 2009

HATIMAYE SERIKALI YAUKOROMEA "UANDISHI UCHWARA" WA HABARI

Kutokana na kufumuka kwa magazeti ya udaku (ambayo yanaweza kuandika udaku wa aina yo yote kumhusu ye yote, po pote na bila kujali cho chote), serikali hatimaye imeonyesha kukerwa na hali hiyo duni ya kiwango cha uandishi wa habari nchini (aka uandishi uchwara). Sijui itachukua hatua gani. Je, utitiri huu wa magazeti ya udaku, ni uhuru wa habari uliopindukia kimo? Hata hivyo ni lazima tukiri kwamba magazeti haya ya udaku yanapendwa sana po pote duniani na ndiyo yanauzika zaidi kuliko magazeti makini ya uchambuzi (Uingereza na Marekani ni mifano mizuri). Kwa vile tumeukubali (au tuseme imetulazimu tuukubali) utandawazi, mimi nadhani magazeti haya yanayoandika habari hizi za uzushi zisizo na kichwa wala miguu hayaepukiki. Utandawazi ni zimwi tena lisilotujua. Swali ambalo tunatakiwa kujiuliza ni hili: Ati, zimwi lisilotujua laweza kutula lisitumalize?

Kwa maoni mengine kuhusu suala hili, mtembelee mzee wa changamoto kwa kubofya hapa

"Uandishi uchwara" kutoka gazeti la Tanzania Daima la Februari 13, 2009 (hisani ya kennedy blogu)

Kutoka gazeti la udaku la Kiu la Februari 13-15, 2009 (hisani ya kennedy blogu)

2 comments:

 1. Uzuri wa sehemu kadhaa za dunia nilizopitia ,watu wengi wakisoma habari kwenye magazeti ya udaku wanajua kuwa ni habari za udaku. Wakitaka habari za uhakika bado huenda kwenye magazeti au source za uhakika za habari.

  Chakujiuliza ni kwamba Tanzania tunatofautisha habari za udaku na habari za kweli na maana.

  Hivi hata upigaji wetu wa kura kwa wapigiwa kura KWA WENGI WETU tunajua au tunauwezo wakutambua waahidiyo na wasemayo yanawezekana au hata ubwabwa unaweza kutufanya tufikiri aliyeleta ubwabwa atajenga barabara?

  ReplyDelete
 2. Hata magazeti kama Rai, Tazama, Mtanzania na mengine yamegeuka ya udaku ili kuwapakazia wapinzani. Nadhani tatizo la wabongo ni kupenda mambo ya hovyo kama udaku na kuchukia mambo ya maana kama kujielimisha. Nimeishi Kenya. Hawana magazeti ya uchafu yaitwayo ya udaku zaidi ya kijarida kimoja kikali cha kuichachafya serikali.

  Kuna matepeli na wapumbavu wachache wametajirika na kupata umaarufu wa kirahisi- cheap populism tokana na kuichafua jamii yetu kwa kuanzisha na kuendesha magazeti ya uchafu.
  Dawa ya kuondokana na magazeti ya uchafu ni kuyafungia tu. Maana licha ya kuandikwa na vihiyo na wasaka ngawira, hayana tija yoyote. Hata hivyo serikali inayashabikia kwa kuyasajiri kwa wingi ili watu wengi wapotelee huko badala ya kuangalia na kuhoji madudu inayofanya chini ya chama cha majambazi na mafisadi.

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU