NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Thursday, February 26, 2009

TUSIJE TUKAJISAHAU TUKASAHAU KUSAHAU

Umeshawahi kusahau mahali ulipoweka funguo zako? Pesa je? Au kama ulifanikiwa kumkwepa konda wa daladala na hivyo ukasafiri bure jana? Bado unalikumbuka jina la mpenzi wako wa kwanza?

Wataalamu wanasema kwamba kusahau ni jambo la kawaida na si mara zote ni dalili za moja kwa moja za magonjwa kama Dementia au Azheimer. Kutokana na habari nyingi ambazo ubongo inabidi uzitunze, wataalamu wamegundua kwamba, mbali na kujipumzisha wakati ukiwa umelala (ingawa bado ubongo wako huendelea kufanya kazi kuhakikisha kwamba moyo unapiga, unapumua n.k.) ubongo inabidi ujisafishe kwa kuziondoa na wakati mwingine kuzifuta kabisa habari ambazo wenyewe unadhani kwamba si za muhimu.

Hata hivyo inakubidi uanze kuwa na wasiwasi kama ukianza kusahau jina la mkeo/mmeo, mahali ulikoficha mabilioni ya fedha zako za ufisadi na kama jana ulipata kinywaji ama la!. Hizi zaweza kuwa dalili za magonjwa kama Dementia au Azheimer. Na kama umesahau kama unapumua ama la (japo umo katika shangingi lako tena lenye viyoyozi), basi yawezekana kabisa ikawa tayari umeshakoma kuishi ingawa bado UPO. Na siku nyingine ukimsahau mtu hebu jaribu kujiuliza, YEYE ANAKUKUMBUKA?

Kwa mazoezi mbalimbali ya ubongo bofya hapa. Lakini kabla ya yote, tusije tukajisahau tukasau kusahau!

7 comments:

 1. Madelo ga wiza!!!nilikuwa sijawahi kutembelea blog yako,kaka una blog nzuri nimeipenda hongera sana.

  ReplyDelete
 2. Mrs. Masanja. Wabeja sana. Nayega gete. Nimeziona pia fasheni katika blogu yako. Inavutia kama nini kuona watu wabunifu kama ninyi. Muendelee kufanikiwa na Mungu awabariki daima!

  ReplyDelete
 3. asante kwa kuwa mfuatiliaji wa blog yangu nilikuwa safarini sasa nimerudi tena kijiweni. nami leo nimekuja tu kukutembelea kwanza.

  ReplyDelete
 4. Karibu tena Yasinta. Nilikaribishwa vizuri sana na wanablogu na tayari nimeshapazoea. Asante

  ReplyDelete
 5. Nimependa zoezi la ubongo.

  Kwa leo nimepita kuweka sahihi kwenye kitabu cha wageni.

  Kazi nzuri sana kaka yangu.

  ReplyDelete
 6. Haya ni mawazoni kwelikweli. Kuanzia tittle mpaka yaliyomo. Pretty nice.
  Thanks

  ReplyDelete
 7. Mheshimiwa Bwaya, asante kwa kupitia mitaa hii. Mimi pia huwa sipitishi siku bila kupitia mitaa yako ya utambuzi na ninapokuwa na sekunde nachangia mawazo yangu huko. Mzee wa Changamoto - wewe ni mwenyeji wa mitaa hii na daima huwa nafurahia komenti zako wenye upeo wa juu. Mimi pia ni mwenye sana wa mitaa ya changamoto. Tuendelezeni libeneke - polepole tu tutafika!

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU