NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Friday, February 20, 2009

WATANZANIA: NI NINI KIMETUFIKISHA HAPA???

Hebu tazama hizi picha za kutisha kwa KUBONYEZA HAPA. Ni nini kimetufikisha hapa? Zile falsafa za upendo, undugu na umoja alizotuachia Mwalimu Nyerere ziko wapi? Kama taifa, tunaelekea wapi? Leo ni maalbino, kesho itakuwa zamu ya nani? Je, huu ni mwanzo wa mwisho wa Tanzania iliyokuwa inasifika kwa amani na upendo? Tukiweza kuzigundua sababu hasa ambazo zimetufikisha hapa, ndiyo tutaweza kupata suluhisho la kudumu la tatizo hili. Hili ni tatizo la kila Mtanzania na Watanzania wote tukiamua kulimaliza tunaweza tena mara moja (tusiitegemee serikali). Hebu na tupambane na kuhakikisha kwamba tunaitokomeza hii kansa kabla haijagoma kutibika!

4 comments:

 1. Yes, this is the beginning of the end for the peaceful and beautiful Tanzania. Very sad!

  ReplyDelete
 2. Unajua kuna maswali nimejiuliza tangu nisome maoni yako barazani kwangu. Ni kuwa haya ndio yameanza kutokea ama yamefichuliwa na hivi vyombo huria? Si unajua nyumbani habari zetu zilivyo? Unajua ripoti na taarifa "tunazolishwa" kutoka kwa vyombo vilivyoamua kujikita mijini? Kwani kama kusingekuwa na hizi newsroom huria tungeyaona haya kwa ukubwa tuyaonayo?
  Pengine hatukuwa mbali na tulipo, ila hatukujulikana kwa kuwa mwanga wa kutumulika kuuonesha uchafu wetu haukuwepo. Sasa tumemulikwa, sasa tumeonwa na sasa tunaonekana. Lakini bado hakuna anayeonekana kuwajibishwa. Hakuna anayewajibisha uhalisia na uasilia wa matatizo haya. Siasa si hasa kama alivyojisemea Dadangu Subi.
  Inauma saana na kusikitisha saaaana kuona ndugu zetu ambao ni kwa sababu ya kibaiolojia na ambayo hawana maamuzi ju ya sababu hizo, wanaanza kuishi maisha ya kujificha.
  Sijui, ila si nzuri

  ReplyDelete
 3. Mzee wa changamoto. Naona umegonga pointi (kama kinavyosema kizazi cha dot com). Kule nyumbani kwetu Shinyanga mauaji ya vikongwe kwa tuhuma za uchawi yalikuwepo tangu zamani, lakini kwa vile kulikuwa na redio Tanzania, Uhuru, Mzalendo na Daily News tu, mambo haya usingeyasikia yakitangazwa au kuandikwa sana. Leo hii mambo yamebadilika na mambo yako wazi zaidi. Ni wakati sasa wa kutafuta suluhisho - tena la kudumu!

  ReplyDelete
 4. Inasikitisha sana!:-( Mimi naamini ndio maana kuna maaeneo mengi watu walikuwa wanafikiri maalbino wanapotea tu !Naamini haya yalikuwepo muda mrefu.

  Nakubaliana na yote mlioyasema.
  Mungu ibariki Tanzania!

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU