NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Wednesday, April 1, 2009

ELIMU YA JADI, FALSAFA YA ASILI NA "USASA"

Wazungu walifanikiwa kutuaminisha kwamba kabla ya kufika kwao hatukuwa na elimu. Wakatuchezea fikra zetu na kutufanya tuamini kabisa kwamba walikuwa wametuletea "mwanga" Baada ya kuisoma hadithi hii ya Marafiki Watatu na Simba ambayo inapatikana katika kitabu hiki, mara moja utagundua kwamba hata kabla ya mawasiliano yetu na 'wagawa ustaarabu" kutoka Ulaya tulikuwa na elimu iliyokomaa, ya kweli na iliyoshabihiana na mazingira yetu. Nimeikumbuka hadithi hii baada ya kuona mijadala ambayo imekuwa ikirindima katika blogu mbalimbali katika kujaribu kuelezea "msomi ni nani?" na athari za wasomi katika jamii. Na kwa mara ya kwanza inabidi nikubaliane na Kamala ambaye haamini "kabisa kwamba ili uwe msomi unahitaji vyeti na kuvuka madaraja..." Isome hadithi hii fupi hapa chini
======================================

Marafiki Watatu na Simba

Hapo kale palikuwa na watu marafiki watatu. Marafiki hawa walisoma sana na wali­kuwa na maarifa sana ya namna mbalimbali, lakini hawakuwa na hekima. Watu hawa watatu walikuwa na rafiki yao mmoja. Rafiki huyu hakusoma sana lakini alikuwa na hekima nyingi.


Wakati mmoja, mmoja wao aliwaambia wenzake wasafiri ili waonyeshe uhodari wao. Wote wakakubali lakini wawili walikataa kumchukua rafiki yao wa nne kwa sababu hakuwa na maarifa. Rafiki wa tatu akasema afadhali wamchukue. Basi wale wawili wakakubali.


Wakaenda mpaka porini. Hapo wakaona ngozi na mifupa ya simba mfu. Mmoja mio­ngoni mwa wale marafiki wenye maarifa akasema sasa wataonyesha uhodari wao kwa kumtia uhai yule simba. Akasema yeye ataweka mifupa yake pamoja. Wa pili akasema atamtia nyama, damu na ngozi nzuri, na wa tatu atamrudishia uzima wake. Mtu wa nne mwenye hekima na bila maarifa akasema kwamba simba atakuja kuwaua. Lakini hawa­kumsikiliza. Basi yeye akapanda juu ya mti.


Wale watatu wakamtia simba uhai. Yule simba akawa hai na tena mkali sana. Aka­warukia na kuwaua wale watatu mara moja. Ukawa ndio mwisho wa maarifa yao. Yule mwenzao alikaa kimya mpaka simba akaenda zake. Akashuka mtini na kurudi kwao.

No comments:

Post a Comment

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU