NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Wednesday, March 25, 2009

JE, WATADUMU KATIKA NURU?

Nimevutiwa na ari na shauku ya kujisomea inayoonyeshwa na watoto hawa pichani. Wanaonekana kuwa na kiu ya elimu na wako tayari kujifunza. Huu ndio wakati ambao akili zao changa dadisi ziko tayari kufinyangwa, kuelekezwa, kulishwa na kuongezewa kile walichonacho tayari ili hatimaye waweze kufikia upeo wao na kuwa vile wanavyotakiwa kuwa. Mfumo wetu wa elimu unahakikishaje kwamba udadisi, ari na shauku ya watoto hawa kujifunza haukinzwi na wala kukunguwazwa? Je, watoto hawa watadumu katika nuru ya kupenda kujisomea? Inajulikana kwamba Watanzania ni watu ambao hatuna utamaduni wa kupenda kujisomea na waandishi wengi wameshalalamika sana kuhusu vitabu vyao kukosa wasomaji. Ni wakati gani ambapo tabia ya kupenda kusoma vitabu hudorora na hatimaye kufa kabisa? Na kama hatujisomei, sisi ni taifa ambalo tumo nuruni au gizani?

Samahani kwa maswali mengi lakini haya ni maswala ambayo huwa yananikera na kunikereketa sana.

1 comment:

  1. Maswali ni mazuri, na ni kweli watanzania ambao hatupendi kusoma vitabu. na pia kusoma vitabu kama hujaanzia tangu msingi, yaani mwanza au mtoto anapoanza au hata kabla hajaanza shule. Na pia ni kazi ya wazazi kuwahimiza watoto wao kusoma vitabu. Lakini sasa kama mzazi naye hajui hata kitabu ni nini basi hapo inakuwa kasheshe. Nakumbuka wakati mimi nasoma katika darasa langu nusu ya darasa walikuwa hawajui kusoma wala kuandika majina yao. Lakini kwa sasa nina imani watoto wengi wamepata moyo wa kusoma vitabu. Kwa hiyo tukazani kuwahimiza ila kizazi kijacho kiwa safi zaidi.

    ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU