NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Sunday, March 1, 2009

KUTOKA MAKABAILA MPAKA MAFISADI - TUMEPIGA HATUA?

Naona Profesa Ndumilakuwili yuko kwenye profesheni yake hapa. Anamnyemnelea jamaa ambaye amenona na moja kwa moja anachukulia kwamba pengine ni fisadi.

Enzi zile watu wenye "afya" (ambayo kwa sababu zisizoeleweka inaashiriwa na unene au kitambi) walikuwa wanaitwa makabaila, mabepari na makupe. Inaonekana sasa ukiwa na "afya" a.ka. mnene mwenye kitambi basi wewe ni fisadi. Je, wenye vitambi vya gongo na dengerua je?

Tumetoka makabaila, tukaingia wahujumu uchumi enzi za Moringe Sokoinne na sasa tumeingia mafisadi. Tumepiga hatua, tuko pale pale tumesimama tisti au tunarudi nyuma? Tutabadili majina mpaka lini?

3 comments:

 1. Afadhali tungesimama palepale. Tunapiga hatua. Ila ni mbili mbele tatu nyuma. Lakini si tunasonga? Ila kinyumenyume.
  Bahati ni bahati na kama hujasema ni mbaya au nzuri, basi kuna utakaowachota tuu. Kubadili majina kunawasaidia wenye kuyabadili. Lakini manufaa hakuna.
  Inasikitisha

  ReplyDelete
 2. kazi kweli kweli kwani sasa afya zote ni ufasadi tu na kwa kweli hatutafika mbal. Nakubaliana na mzee wa changamoto inasikitisha sana

  ReplyDelete
 3. Labda tunabadili majina kujaribu kuhadaa watu tatizo ni tofauti. Lakini angalau katika lugha tunapata kutumia misamiati mipya kwa tatizo la ugonjwa wa JULIANA kwenye UKIMWI.:-(

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU