NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Tuesday, March 3, 2009

MATUNDA YA KIASILI NA MAISHA YA KUMBUKONI

Picha hii kutoka kwa Mjengwa imenikumbusha mbali sana. Enzi zile tukichunga ng'ombe Unyantuzu Bariadi tulizoea kula hayo matunda meusi madogomadogo ambayo kwa Kisukuma (Kinyantuzu) yanaitwa Nhobo. Yakiiva yanapasuka na inabidi uwe na meno imara kuyatafuna hasa pale mwanzoni. Ukishavuka hii hatua ya mwanzo basi yanakulainikia mdomoni na kutoa utomvu mweupe mzito mtamu unaonatanata. Unatafuna mpaka unahakikisha kwamba utomvu huo umeisha. Unatema makapi yanayobakia, unachukua tunda jingine na kuanza upya. Asante sana Bwana Mjengwa kwa picha hii ambayo imenipa taswira nzuri sana ya maisha yale 'simple', matulivu na yenye ridhiko tuliyoishi enzi zile tukiwa watoto.

1 comment:

  1. Ntobo inaonekana ni tunda tamu kweli maana naona ni kweli amekukumbusha mbali sana. Nakubaliana nawe vyakula vya asili ni vitamu sana nami sasa umenikumbusha nilipokuwa mdogo kuna matunda fulani yanaitwa"MADONGA" haya ni makubwa mviringo kama chungwa na ndani yana mbegu ndogondogo na nyamanyama ni matamu sana. Napanda vyakula vya asili. Asante

    ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU