NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Monday, March 30, 2009

MAZINGIRA YASIYO SALAMA KIAFYA YAKO WAPI?

Nimetatanishwa na dai kuu katika picha hii. Mazingira yasiyo salama kiafya yako wapi katika picha hii? Hivi si ndivyo chakula kinavyoandaliwa huko vijijini ambako zaidi ya robo tatu ya Watanzania wanaishi? Hebu tufanye lojiki ya kitoto kidogo hapa chini.

(1) Chakula hiki kinapikwa katika mazingira yasiyo salama kiafya
(2) Zaidi ya robo tatu ya Watanzania hupika chakula katika mazingira kama haya
(3) Kwa hivyo zaidi ya robo tatu ya Watanzania hupika chakula katika mazingira yasiyo salama kiafya.

Na hili ni jambo la KUTISHA!!!

Nyongeza: Shuleni enzi zile wapishi walikuwa wakipika ugali na ndizi (za kutosha zaidi ya wanafunzi 600) kwa kutumia kuni huku majasho pamoja na KAMASI vikidondokea humo humo kwenye ugali na ndizi zetu. Ukiongeza na maharage yaliyooza basi we acha tu. Wengine walinenepeana, wengine walikondeana lakini hakuna aliyeugua.

1 comment:

  1. "Shuleni enzi zile wapishi walikuwa wakipika ugali na ndizi (za kutosha zaidi ya wanafunzi 600) kwa kutumia kuni huku majasho pamoja na KAMASI vikidondokea humo humo kwenye ugali na ndizi zetu..."

    Usinikumbushe bwana. Kweli tumetoka mbali na inasikitisha kuona kuwa hali bado haijabadilika. Hata mimi sioni mazingira yasiyo salama kwa afya katika hiyo picha ni yapi? Kijijini kwetu Songea bado wanapika hivi hivi. Ina maana ni mazingira yasiyo salama kwa afya pia. Mazingira salama ni yepi????

    ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU