NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Tuesday, March 31, 2009

MFALME MSWATI III

Hii nimeiiba kutoka kwa FATHER KIDEVU. Hawa ni wakuu wa nchi wanachama wa SADC walipokuwa katika mkutano nchini Swaziland hivi karibuni. Mstari wa mbele toka kushoto ni Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania, Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe, Mfalme Mswati III wa Swaziland, Rais wa Afrika Kusini na Mwenyekiti wa SADC, Khaglema Montlante, Rais Joseph Kabila wa Congo DRC na Rais Armando Guebuza wa Msumbiji. Mstari wa nyuma toka kushoto, Waziri Mkuu wa Lesotho Phakalitha Mosisili , Rais wa Malawi, Bingu wa Mutharika na Rais wa Zambia Rupia Banda.

Kilichonivutia ni huyu Mfalme Mswati III. Mbali na kulaumiwa sana kwa utamaduni wake wa kuoa vibikra vipya kila mwaka, na kuishi maisha ya kifahari kupindukia huku wananchi wa nchi yake ndogo wakihangaika katika umasikini, huwa ninavutiwa naye kwa jinsi anavyoonekana kusimama kidete kupigania utamaduni wake (ambao bila shaka ndiyo unamwezesha kuweza kuendelea kutawala na kunyakua hivyo vibikra vipya kila mwaka). Inapendeza kama nini kwa mfano katika picha hii kuona wenzake wameulamba kwa suti kali za bei mbaya lakini yeye amevaa mavazi yake ya jadi. Ingependeza zaidi kama mavazi haya "simple" yangeendana na maisha yake halisi anayoishi. Yote kwa yote - hata kwa hili dogo - anastahili "sifa" Na huwa ninakerwa na makelele ya watu kutoka nje hasa Ulaya wanaodai kwamba wakati wa kuwa na wafalme umeshapita wakati wenyewe bado wana malkia...

4 comments:

 1. I wish ningekuwa mimi ndiyo naoa hivyo vikra vipya kila mwaka. Raaaahaaaaaa!!!!!!!!

  ReplyDelete
 2. Aisee umenikumbusha. Sijawahi kubikiri mtu aisee. Kuanzia leo naanzisha kampeni ya kutafuta bikra wa kubikiri - tena yule ambaye age yake iko legal. Kwa wakati huu hata hivyo sidhani kama nitampata...

  ReplyDelete
 3. Eh! Comments zenu siku hizi....!

  ReplyDelete
 4. Nyie mnaotafuta mabikra, nyie wenyewe ni "mabikra wakiume....????"

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU