NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Saturday, March 28, 2009

MKIONA NIKO KIMYA MJUE KWAMBA NIMEKWENDA KUPAMBANA NA "MZEE WA VIJISENTI" KUWANIA UBUNGE WA BARIADI MAGHARIBI

Hebu tazama huu ulaji. Yaani hata nimekosa la kusema. Mzee wa Vijisenti kaa chonjo naja! Natania tu kwani sina mabilioni ya kwenda kuwahonga wapiga kura (picha kwa hisani ya Kennedy)

4 comments:

 1. Masangu, hii nchi ya Tanzania imedhulumiwa vya kutosha. Inahitajika elimu kwa wananchi kuwafahamisha nini cha kufanya maana tayari kuna watu wameshaanza kuwaonesha ni nini wanachodhulumiwa. Ikishafahamika lugha ya kuwaelewesha wananchi, itakuwa rahisi sana kufanya mabadiliko ya kuiondoa ile nchi katika dhuluma kubwa iliyoko kwa sasa. Wale walioidhulumu walijua lugha ya wananchi ni fedha ndiyo maana wakawapatia kofia na khanga na tisheti na sherehe za takrima. Sasa inahitajika mtu wa kuwauliza kama hivyo walivyopewa vinawatosha kuondoa machungu ya kukosa maji, kukatikiwa umeme, kutokuwa na huduma bora mahospitalini, kuishi bila ya barabara za nzuri, kukosa ruhusa ya soko la bidhaa zao, udanganyifu katika malipo na mafao yao ya uzeeni, afya, ajali nk nk nk. Wachoke na siasa za uchaguzi zinazoahidi mambo yale yale kila baada ya miaka mitano. Watu wanaahidi mambo lukuki, wakipata uongozi wanaonesha kama wanaanza kazi mwaka ukikatika wanazugazuka, ukikaribia mwaka wa tano, wanaanza tena kurepea viraka kujidai wanafanya kazi. Hii danganya toto haifai. Nimechoka kweli na huu uongo! Haifai. Haifai!

  ReplyDelete
 2. Duh hizo posho ndio maana hawaachi kulala kwa babu wa mlingotini.

  ReplyDelete
 3. Dada Subi. Kampeni za uchaguzi uliopita zilinishangaza. Mzee wa vijisenti alikuwa anagawa baisikeli, sukari, kanga, vitenge, chumvi na wale wajanja walikuwa wanapata mpaka pikipiki. Zilikuwa ni kampeni za gharama kubwa mno ambazo kwa mtu wa kawaida kamwe haiwezekani. Na watu kwa sababu ya umasikini walikuwa wanafikia hata kupigania hizi zawadi. Tatizo ni umasikini wa watu na mwamko mdogo walionao. Nawafahamu vijana wajanja ambao walipata mitaji ya kuanzishia biashara kutokana na mapesa yaliyokuwa yanamwagwa na wengine wameweza kutajirika. Kama kweli hakuna mlo wa bure (there is no free lunch) mabilioni haya yanayomwagwa katika kampeni ni lazima yarudi kwa njia moja au nyingine. Na hapo ndiyo "vijisenti" vinakuja. Nionavyo mimi hali imeanza kubadilika na baada ya muda si mrefu wananchi pamoja na umasikini wao watatambua kwamba kilo tano za sukari au pea mbili za kanga kila baada ya miaka mitano (tena kwa peza zao wenyewe zilizoibwa) pengine siyo "bei" halisi wanayostahili kwani demokrasia na haki kamwe haviwezi kununuliwa. Pamoja na kudaiwa kuwa na mamilioni ya dola Mzee wa vijisenti hajafanya cho chote jimboni mwake mbali na kuwa na wahamasishaji walio mbele kuongoza migao ya pesa kwa wafuasi watiifu waendao kama kondoo. Hawa ndio walishughulika na kuandaa mapokezi yale ya "kishujaa" baada ya ile skendo ya vijisenti iliyompotezea uwaziri. Safari bado ni ndefu lakini wananchi wameanza kuamka na hali inabadilika. Lakini kwa sasa hali ilivyo inatisha, inasikitisha, inakera na kama ulivyosema Haifai. Haifai kabisa!

  Egidio - kwa posho kama hizi wataachaje kushinda kwa babu wa mlingotini?

  ReplyDelete
 4. Ndo maana tuna bunge bubu,hawawezi kupingana na serikali kwa lolote kwani serikali imeisha wanunua.Kinachotakiwa ni kuhakikisha kwamba baadhi ya sheria za namna hii zinaondolewa.Baado tunatwikwa mzigo wa kumtunza waziri mkuu na rais wastahafu kwa mamilioni kama hayo je kunasiku nchi hii itakwamka kiuchumi wakati pato la taifa linaishia mikononi mwa wajanja wachache?

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU