NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Friday, March 13, 2009

PICHA HIZI ZINAKUKUMBUSHA NINI?

Hasa kwa vijana mliokulia vijijini au mnaoyafahamu vizuri mazingira ya vijijini, picha hizi zinaleta kumbukumbu gani? Mimi zimenikumbusha mbali sana kwani huu ndio ulikuwa wakati wetu enzi zile tukiwa vijana (kama asemavyo mwanafalsafa Simon Kitururu) wa kuwa kwenye fani. Sasa ninapoziangalia picha hizi kidogo nashangaa. Kwa nini wavulana (ambao pengine ndio wenye nguvu zaidi) hatukujitolea/hawajitolei hata siku moja kumsaidia binti kubeba hiyo ndoo ya maji ili aweze kusikiliza hoja kwa makini na raha?

6 comments:

 1. Swali nzuri sana na nasubiri jibu toka kwa vijana wote.Asante sana kwa swali hili

  ReplyDelete
 2. ehehehehehehheheh

  wewewe umenikubusha mbali. nikiandika hapa nitajaza blog hii lakini we acha tu kila lika na utamu wake. sasa akimsaidia ndoo unafikiiri atapataje mwanya wa kushusha vina? si watawahi na kufika home mapema?

  akimuona mtu mzima anajificha kwanza. ila yawezekana wakaingia kichakani na labda kulazimika kurudi mtoni. usiombe wakutane na nyoka wakati nguo zimeshuka hadi magotini au atokee mtu mzima, wewe?

  gafura haoooo hawaagani mpaka siku nyingine!

  mapenzi ya hivi ni matamu kuliko ya kisasas.

  ReplyDelete
 3. Mmmh mimi sisemi mengi ila zimenikumbusha mbali sana,

  Kaka Simon siuseme tuu, wengine tutaziba masikio au mnong'oneze basi kaka Masangu.lol.

  ReplyDelete
 4. Mfumo dume una historia ndefu. Na unapokuta mwanaume anajiona mfalme asiyehojika, usimlaumu.

  Hivi vijana tulikulia katika mazingira hayo unategemea nini? Kubadilika baada ya semina ya juma moja?

  ReplyDelete
 5. Kawaida hawa mabwana wanajifyagilia upande wao, wanatafuta kujiridhisha na sio kuridhishana. Wala usitegemee kama mawazo ya kumsaidia yatakuja labda kwanza litoke jibu la kukubaliwa ombi lake ndipo ataanza kujishebedua et mh aa hebu lete nikusaidi mpenzi,,,, kwakuwa kaanza kuona nyota njema inaanza kung'aa vyenginevyo..

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU