NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Sunday, March 8, 2009

SIKU YA WANAWAKE DUNIANI - NAMUENZI MAMA

Ndio wanaojidamka saa 10 alfajiri kwenda kutafuta maji ya kunywa. Ndio wanaotembea maili nyingi kwenda kutafuta kuni. Ndio wanaofanya kazi mashambani kutwa ingawa mara nyingi hawafaidi wakizalishacho. Ndio mhimili na nguzo kuu ya familia na malezi. Ndio.....NI AKINA MAMA....

Katika kusherehekea sikukuu ya wanawake duniani leo napenda kuchukua nafasi hii kumshukuru na kumpongeza mama yangu mzazi Eunice Longh'we Mgema Dindai pamoja na akina mama wote duniani. Mama - wewe ni shujaa wangu nambari wani. Baada ya kuondokewa na mumeo mpendwa tukiwa bado wachanga hukukata tamaa bali ulitulea vyema na kuhakikisha kwamba tunasoma - ukilima pamba kila mwaka ili tupate karo ya shule. Hatuna cha kukulipa mama mbali na kusema tu asante kwa kujitoa muhanga kwako - leo hii sisi na wajukuu zako tunayo maisha yenye ridhiko na matumaini. Mungu akubariki sana na daima utabakia kuwa shujaa wetu!!!

Tunaungana na Boyz II Men katika wimbo wao wa A Song to Mama katika kukushukuru na kukutakia maisha marefu na yenye afya - wewe pamoja na wanawake wote duniani. Bila nyinyi pamoja na umakinifu wenu katika malezi ya watoto sidhani kama tungekuwa na jamii. ASANTENI SANA!!!

11 comments:

 1. Kwa kweli asiyemuhushima mama yake na kumwambia sasa mama asante kwa kunileta duniani hapa basi afadhali achukue nafasi hii na kumwambia. Kwani hakuna kitu kinaweza kufananishwa na mama. HONGERA wanawake wote duniani. Msalimie mamako kaka Masangu

  ReplyDelete
 2. Kaka asante sana kwa ujumbe wako,kwakweli umeonyesha kuwa unamthamini kila mwanamke, au kila mama sio mama yako tu pekee bali nikila mwanamke, ni kweli mwanamke ni nguzo ya familia,binafsi nimeshuhudia familia nyingi sana hapa duniani watoto wengi wanalelewa na mama wengine baba zao bahati mbaya wamefariki na kuwaacha watoto wadogo,lakini kina mama hujinyima kwa kila kitu na kuhakikisha watoto wanapata mahitaji yao muhimu,chakula, mavazi na elimu kweli hakuna kama mama,na mimi natumia nafasi hii kwa kumpongeza mama yangu na kusema mama nakupenda sana, bila wewe mimi leo hii nisingefika hapa nilipo leo asante sana mama.

  ReplyDelete
 3. Nice to meet U, I am from Dumai Indonesia. Visit me on www.hendri-rena.net. Succesfull 4 U. See U again

  ReplyDelete
 4. tehe tehe. matondo najiuliza kama ujumbe huu amefika kwa mama yako au ni kwa ajili ya sisi tunatembelea blog hii peke yetu. yasinta ujumbe wako juu ya mama ni mtamu na labda ole wangu nisiyejua upendo wa mama wala kupendwa na mama toka udogoni lakini napendwa na mke wangu kwani na yeye atanizaa. ni kwa kupitia yeye ni tapanda mbegu itakayoujaza ulimwengu.

  NB: hakuna aliyeomba kuzaliwa na kuzaliwa kwetu ni matokeo ya michezo fulani tu ya mama na 'labda' baba

  ReplyDelete
 5. Asanteni nyote. Yasinta - salamu zako zilifika. Asante sana. Kamala, ndiyo mama anafahamu. Nilimpigia siku hiyo nikaongea naye na kumshukuru tena. Alishangaa sana kusikia kwamba eti kuna siku ya wanawake duniani. Japokuwa yeye ni mzee sana lakini bado akili yake ni sharp na bado anafanya kazi alizozizoea mf. kuokoteza kuni, kulima kila anapoweza n.k. Kamala - kwa wanaoamini katika "Higher Power" wanaamini kwamba kuzaliwa kwao siyo ajali ya kimaumbile wala matokeo ya "michezo fulani tu ya mama na 'labda' baba" bali kuzaliwa kwao kulipangwa na kwamba maisha yao yana thamani na tena wanalo jukumu la kutenda hapa duniani. Hawa wanaishi (au tuseme wanatakiwa kuishi) "purpose-driven life" wakiheshimu na kufuata matakwa ya hiyo "Higher Power" wanayoiamini. Kwa hivyo kuna watu watakaotofautiana na hiyo falsafa yako ya ki-ombwe (nothingness) na "michezo" kama chanzo na lengo hasa la maisha yao. Mimi ni mmoja wao!

  ReplyDelete
 6. matondo yafaa kabisa uone naandika kwa mkabala upi. ni kweli sisi sio ajali wala bahati mbaya. ila kwa wazazi wetu wanafikiri wanatumiliki, wajiojua kuwa tulikuja kwa malengo tofauti na ya wao kutaka tukamilishe failures zao, basi sisi ajali za ngono zao na si vinginevyo. otherwise ilibidi tuwepo na hivyo tumekuwepoo na tutaendelea kuwepo mpaka pale tutakapotimiza malengo ya kuwepo kwetu au tukidhiirikaa kushindwa kuyatimilisha malengo yetu na hivyo kuondoka na hapa naongelea kuwepo nikimaanisha kuwa ndani ya miili yetu

  ReplyDelete
 7. Kamala,nimekupata. Kutofautiana na wazazi ni jambo la kawaida na karibu kila mmoja wetu kwa namna moja au nyingine ameshapambana nalo. Wakati mwingine wanakuwa na pointi na wakati mwingineni ni tofauti za kimitazamo tu. Kwa vile ni wazazi wetu, tunapaswa KUWAHESHIMU na kuwaelimisha pole pole tena kwa upendo. Baada ya muda watatambua kwamba ulimwengu wa sasa umeshabadilika na watoto wa sasa siyo wale wa enzi zao. KAMWE hakuna faida yo yote tutakayoipata kwa kukosana na wazazi wetu. Tena tukumbuke kwamba nasi ni/tutakuwa wazazi na tutapambana na michakato ile ile ambayo wazazi wetu wamepitia. Upendo na heshima ndiyo silaha ninayoiamini katika kusuluhisha tofauti zetu na wazazi. Tukubali kutokubaliana nao kwa upendo na heshima!

  ReplyDelete
 8. haya matondo na nilisahau kukupongeza juu ya kuwa na mama anayeokoteza kuni nk. ukipotoka utampeleka mjini japo ukweli ni kwamba inabidi aishi kwenye utamaduni wake aliouzoea hata kama mwanae ni tajiri vp.

  ReplyDelete
 9. Kamala. Hapo umesema kweli. Nilishajaribu mambo ya mjini haikuwezekana kabisa. Nilichojaribu ni kumpelekea baadhi ya mambo ya mjini (ambayo sisi tunadhani ni ya msingi) huko huko kijijini. Tena ukimkataza kwenda kuokoteza kuni au kwenda kulima kijishamba chake basi mtagombana sana! Atakuuliza - "unataka nifanye nini? Nikae tu kama mtu aliyekwishakufa? Hoja nzito hizi mtu unakosa la kujibu. By the way, Kamala mimi si tajiri bwana, labda wewe. Na hapa nadhani sijakuchokoza usije ukaanza kunisomesha mambo ya kujitambua kuhusu suala la utajiri, umasikini n.k. Mimi naamini kwamba sihitaji kuwa "tajiri" ili kuwa na furaha na kuishi maisha yenye ridhiko na matumaini. Ndiyo maana kidogo huwa nashangaa kwa mfano mtu kama Mzee wa vijisenti (ni mbunge wangu) anajisikiaje anapochota mabilioni na kuyaficha na watu jimboni mwake hawana hata maji ya kunywa wakati kisima kimoja cha maji safi na salama hakizidi hata dola 2,000 (akiwaambia wanakijji wachimbe wenyewe na yeye alete mitambo)? Kwa dola chini ya laki 1.5 tu angeweza kuwa mfano wa kuwa mbunge wa kwanza ambaye jimbo lake lote lina maji safi na salama...Pengine ridhiko na furaha ni kuyaona tu haya mabilioni yamekaa benki na kuzaliana. Halafu siku moja mtu unakufa na kuyaacha yanagombaniwa! Wewe utajiri unauonaje?

  ReplyDelete
 10. hili la utajiri na utajiri kama wa mbunge wako naona siko kwenye nafasi nzuri ya kuliongnelea sasa hivi na llabda huko mbeleni naweza kulipatia nafasi nzuri, muhimu na imara zaidi.

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU