NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Wednesday, April 22, 2009

BONDIA MSHINDI NA MUNGU WAKE

Huyu bondia aliyeshinda naona anaomba na kumshukuru Mungu wake kwa kumwezesha kumfletisha bondia mwenzake. Huyo aliyefletishwa naye akipata fahamu sijui atamlaumu Mungu kwa kuruhusu afletishwe na mpinzani wake au pengine atachukua mtazamo chanya na kumshukuru Mungu kwa kufletishwa kwake akijipa matumaini kwamba kufletishwa huko kutakuwa funzo kubwa katika mapigano yake yajayo. Imenifurahisha kuona jinsi Mungu anavyogawa "mibaraka" yake kama bondia huyu anavyotudhihirishia; na sisi binadamu tunavyoipokea mibaraka hiyo!

3 comments:

 1. simon aliwahi kuuliza kuwa 'labda shetani asifiwe' badala ya yesu pekee

  ReplyDelete
 2. Kamala, kwa nini unasema hivyo?

  ReplyDelete
 3. Unajua kuna utata saana linapokuja suala la imani katika nguvu ya Mungu kwenye kutuongoza sisi. Angalia wenzetu wanaojilipa katika kutimiza nia yao ya kuitetea dini na kupinga dhuluma dhidi ya dini yao na ukiangalia video zao kabla ya kuondoka kwenda kujilipua huwa wanamuomba Mungu. Sasa ndugu zangu nao wanamuomba Mungu kuwa wakishapelekwa huko wao warejee salama. Lakini wanajua kuwa kule wanakwenda kupigana na kuuana, ina maana wanamuomba Mungu awawezeshe kuua na wasiuawe.
  Inachanganya kwa kweli.

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU