NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Wednesday, April 1, 2009

CHANGAMOTO YETU...

Baba kakaa na kupiga akili akaona hakuna "option" na akaamua kumtia mtoto wake kwenye tenga ambalo kwa kawaida hutumika kusafirishia wanyama kama mbuzi na kondoo tena ambao mara nyingi wanakwenda kuchinjwa. Sikuweza kuipata habari hii kamili lakini natumaini huyu mtoto alipona na siku moja atakuja kusimulia kisa hiki. Hii ni changamoto yetu sote kwani sidhani kama ni sahihi katika karne hii ya 21 tuendelee kusafirisha wagonjwa wetu katika matenga!

5 comments:

 1. Ni masikitiko na huzuni isiyo kifani.
  Linganisha picha hii na picha chache tulizoziona zenye kutaja mamilioni ya mishahara ya wabunge kwa ajili ya wananchi wa jimbo lake, yaani kwa miaka 48 bado wabunge hawajaweza ku-formulate njia nzuri ya kusaidia umma wanaouwakilisha?
  Kushindwa kwa jamii ni kielelezo tosha cha kushindwa viongozi wao.
  Nakubali kuwa haiwezekani mbunge akasuluhisha ama kurekebisha kila tatizo la jami iyake, lakini hili? hapana. Hili linaashiria hali ni mbaya kwa kila kona utakayolitizamia. Vipaumbele vyao ni vipi hawa watu lakini?

  ReplyDelete
 2. Kwa kweli ni masikitiko makubwa sana. Na hapa umenikumbusha nilipokuwa mdogo nilikuwa naishi kijiji kimoja kiitwacho KINGOLI. Kijiji hiki kipo "Porini kabisa" ambako gari linafika mara moja kwa moja. Sasa siku moja mama mmja alikuwa mjamzito na uchungu ulikuwa umemwanza palepale dispensari haiwezekani. Watu (wanaume) wakapiga bongo na wakatengeneza miti na kamba kikawa kama kitanda wakamlaza na kuanza Safari ya kumpeleka PERAMIHO. Kwa bahati mbaya, Asubuhi tulipoamka tulisikia yule mama kafa na mtoto pia. Nami natumai mtoto alipona na namsifu baba kwa kupata akili kama hiyo.

  ReplyDelete
 3. Kwa kweli, habari ya usafiri ni tatizo kubwa sana hapo nchini. mtu anaweza kufa hasa sehemu za vijijini kwa sababu tu ya kukosekana kwa usafiri wa haraka. Yasinta you made me remember mdogo wake mama aliyeugua ghafla, sasa kumbeba mwanamke mkubwa ni kazi kwa kuzitumia hizo miti, baada ya kutembea kwa muda, dada yule alifariki njiani bila hata kufika hospitalini. Well, sijui nini kifanyike, maybe wenye magari ni namna mojawapo ya kufanya biashara yako, nunua gari lako, liweze sehemu hizo. Utaokoa watu, pia utapata mtaji, kuliko kuitegemea serikali inayojifikiria kuliko watu walioiweka serikali hiyo. Mbarikiwe.

  ReplyDelete
 4. Subi, ni kweli. Wakati wa Mwalimu wananchi walijitengenezea barabara. Sijui zilikuwa za nini. Hata kwenye hiyo picha ya huyo baba na mtoto naona kuna barabara nzuri tu. Yasinta na Laiser, habari za wagonjwa huko vijijivi kwa sababu ya kutowahishwa katika vituo vya afya ni kusikitisha. Cha ajabu ni kwamba habari kama hizo ni za kawaida sana huko vijijini. Wazo la kupeleka mikweche ya magari huko ni zuri. Shida ni kwamba watu ni masikini mno na zingatia kwamba Tanzania bado ni vigumu sana kupata mikopo. Hao wenye pesa wanataka magari yao yafanye shughuli mjini ambako kuna pesa zaidi. Nani atapeleka gari lake kijijini?

  ReplyDelete
 5. Morgan Heritage waliimba kuwa "what they spend for a day, can feed a working family for a year." Na Da Subi amesema na pia Da Yasinta na Laizer wamenena hapo. Sina hakika na vigezo vitumikavyo kubainisha ni wapi panahitaji kukarabatiwa kama si kujengwa upya Tanzania. Yaani kuna wakati najiuliza kama hawa waheshimiwa huwa wanalala usingizi mnono ilhali wanajua kinachoendelea kuwasibu wananchi. Nimeshaona wagonjwa wakipelekwa kwenye zahanati wakiwa kwenye machela ambazo unajiuliza kwa umbali na ubovu wa barabara toka watokako mpaka waendako hakutasababisha magonjwa mwngine kama mgongo1!! Lakini ndio kwetu. Nilipoandika kuhusu wimbo wa Tell Me How Come ndilo nililokuwa nikiongelea. Kuona watu wakijimwayamwaya na marupurupu kibao huku wananchi wakiangalia kwa macho ya ziada kuona kama wataiona kesho.
  Mungu Bariki

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU