NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Monday, April 13, 2009

ELIMU YA JADI INAYOFIFIA

Kwa vile tumefundishwa kwamba ili kupata moto ni lazima uwe na kiberiti, wengi wetu tunaweza kufa na njaa kiberiti kikikosekana. Kwa vile tumefundishwa kwamba ili uweze kukoga ni lazima uende mtoni, kisimani au bafuni, wengi wetu tunaweza kufukuta kwa vile eti hakuna maji, lakini si kwa hawa Wasan wenyeji wa Jangwa la Kalahari. Elimu yao imewapa mbinu mbadala za kuweza kupambana na kuyamudu mazingira yao vizuri. Na hawa hawahitaji kukaa madarasani na kupata maPhD. Elimu yao ni hai na imefumana mumo kwa mumo na maisha na mazingira yao. Halafu mtu kutoka nje anakuja na kuiita elimu hii kuwa ya kishenzi! Ni aibu kubwa kwamba elimu hii ya jadi inazidi kuangamia na kufifia kwa kasi ya kutisha.

Wanaume hawahitaji kiberiti kukoka moto (Picha zote na Petri Kosina)


Mizizi hii ina maji ya kutosha kunywa na hata kuoshea watoto!

5 comments:

 1. Kweli akiba haiozi na akili ni nywele, kila mtu ana zake hata wenye upara.
  nhe he he, huyo mama ameficha kipisi cha sigara kwenye sikio? kanikumbusha mafundi mbao na randa - mainjinia!

  ReplyDelete
 2. Kazi kwelikweli, Ni kweliaiba haiozi. Subi ameweka hiyo sigara akishanyonyesha mtoto anataka avute hukugundua:-)

  ReplyDelete
 3. Dah!!! Hapa nimekumbuka mbaali sana japo sikuishi maisha haya yote. Nakumbuka wakati ambao kwa kuwa hakuna kibiriti na wazee hawataki sigara "iliwe na upepo" walikuwa wanaigeuzia ndani na kuifanya isiteketee.
  Lakini kuna mengi ambayo hata kwetu hayaonekani kuwekwa japo kwenye kumbukumbu. Mfano ni namna wanavyoweza kutunza mwili wa mtu mpaka nduguze waje bila kuugandisha wala kuudunga sindano ama "kulifunga tumbo" lisioneshe mimba kwa wakati fulani. (Sijui hii inatendekaje na ina athari gani kitabibu. Labda Da Subi atanisaidia). Nakumbuka wanavyofunga msosi nyumbani kwenye jani la mgomba na unakuwa wa moto kwa muda wote utakaokuwa unachunga ng'ombe wako ama unasafiri (Hotpot). Nikiwa Lindi ambako kulikuwa na maji ya chumvi walikuwa na namna ya kutumia majivu (na wengine wakitumia vitu vingine) kuchanganya kwenye maji kisha kukata chumvi na kuweza kuyatumia kama "maji baridi".
  Kuna meengi ya kujivunia ambayo sasa yanaonekana kama ya kipumbavu kwa kuwa tu asili yake ni wketu na si kwao. Niliwahi kuandika makala moja yake Kaka Ndesanjo Macha na unaweza kuipata http://changamotoyetu.blogspot.com/2008/08/jungu-kuu.html
  Asante Kaka Matondo kwa Changamoto hii

  ReplyDelete
 4. Naona dada Subi na Yasinta wamevutiwa na hiyo sigara masikioni. Safi.

  Mzee wa Changamoto, nitaiangalia hiyo makala uliyoirejelea hapa. Kuna kitabu ambacho kimeshaandikwa kuhusu mambo haya au ndiyo yanakufa kifo cha kibudu? Mengi ya mambo haya yanayo mizizi sahihi kitabibu na mengi yanaendelea kuthibitishwa. Niliangalia programu ndefu juu ya Hoodia ambayo Barbara Walters/Diana Sawyer? mwenyewe alikwenda kule jangwa la Kalahari na kuona jinsi hawa Wasan wanavyoweza kula majani yake na kukaa muda mrefu bila kusikia njaa. Leo hii Hoodia inalimwa kule Jangwani Arizona na imeshakuwa patented na wajanja kutengeneza vidonge vya kusaidia kupunguza uzito...Ningekuwa mtu wa sayansi ningeomba grant kwenda kuya-document haya mambo kabla hayajatoweka kabisa!

  ReplyDelete
 5. hi,
  how nice is your blog,i like it..
  keep it up,
  dont forget to come and meet me @
  http://samvande.blogspot.com,
  regards

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU