NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Tuesday, April 7, 2009

HII NDIYO NJIA BORA KABISA YA KUFUNDISHIA HESABU

Kujumlisha, kutoa, kugawanya na hata kuzidisha vinaweza kufundishika kwa urahisi sana kwa njia hii - vyote katika mazingira yetu wenyewe. Kuna vingapi ambavyo tunaweza kuvifanya vikawa vyetu na tukafundishana kulingana na mazingira yetu, tukaepuka kukaririshana na kuumizana vichwa bure? Kuna ulazima kweli wa kukariri Hydrological Cycle? Mbona mtoto asiambiwe kuweka bakuli la maji katika jua halafu aone baada ya masaa manne kutatokea nini na aunde nadharia zake mweyewe kuelezea nini anafikiri kimetokea? Au akifumwa anadokoa mguu wa kuku jikoni, mbona asiulizwe kuelezea mvuke huo wa joto katika sufuria ulikotoka na unakoenda? Tuache kukaririshana bila sababu. Tukiweza kuwafanya watoto wetu wakaiona elimu kupitia jicho la mazingira yao wenyewe, utakuwa mwanzo wa mapinduzi makubwa sana katika elimu yetu. Hebu fikiria kama ungefundishwa Newton's Laws of Motion kwa njia hii!

5 comments:

 1. Kaka matondo nimefurahi sana kuiona picha hii kwani imenikumbusha mbali sana. Kuwa mtoto safi sana unajua watoto wanajifunza mambo mengi hata bila wenyewe kujua wanajifunza kitu. Na ni wepesi sana kujifunza. Nimekumbuka nilipokuwa mdogo nilikuwa nachaza mchezo fulani mnakuwa wawili na kunakuwa na mawe kumi na mbili madogo na moja kunbwa la mviringo na unarusha lile kubwa juu na kujaribu kuokota yale kumi lakini moja moja na kuyaweka ktk mkono wa mwingine. Ni kweli michezo mingi inayocheza na watoto , hawachezi tu wanajifunza kitu. kazi kwelikweli

  ReplyDelete
 2. Ombi naweza kuitumia hii picha nimeiopenda na inanikumbusha mbali sana wakati wa ujana wangu

  ReplyDelete
 3. Pasaka njema kaka pamoja na familia yako.

  ReplyDelete
 4. Yasinta, hakuna haja ya kuomba. Lengo letu ni moja na itumie vyo vyote unavyoona.

  Dada PASSION4FASHION.TZ asante kwa kunitakia pasaka njema. Niko safarini. Hata wewe nakutakia pasaka njema pamoja na familia yako. Mungu azidi kukubariki daima...

  ReplyDelete
 5. Ahsante kaka Matondo. Nami nachukua nafasi hii na kusema Heri sana kwa Pasaka. Na usafari salama Mungu yu pamoja nawe.

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU