NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Monday, April 6, 2009

MBUNGE WANGU NA MABILIONI YA WANANCHI

Lakini ukifika jimboni kwake hakuna lolote. Bilioni moja tu ingetosha kuchimba visima vya maji karibu katika vijiji vyote. Hii ingemfanya aingie katika Historia kwa kuwa mbunge wa kwanza kutumia pesa "zake" kuhakikisha kwamba jimbo lake lote lina maji safi. Kuna raha gani kukaa na mabilioni yote haya huku watu wako wakiwa hawana cho chote? Sitashangaa akishinda tena ubunge mwaka kesho na hata kuukwaa uwaziri tena! Katika uchaguzi uliopita alifanya kufuru kwa kugawa baisikeli, mabati, vitenge, sukari, chumvi, pesa, kanga na hata pikipiki. Bado changamoto tuliyonayo ni kubwa!

3 comments:

  1. Achimbe visima jimboni kwake achekwe?labda kama malaria imempanda kichwani,utashangaa akigombea tena ubunge jimboni kwake atashinda tena kwa kishindo hana tofauti na Mugabe,watu wanalalamika ikifika wakati wa uchaguzi wanawachagua tena.

    ReplyDelete
  2. PASSION4FASHION.TZ... Si angepatengeneza pale Dutwa alipozaliwa basi angalau paonekane kwamba hapa ndipo kweli anatoka Bilionea wa Rada? Angechimba visima vya maji pale, jenga zile shule vizuri na kutengeneza angala ofisi za walimu wa Dutwa Secondary School. Yaani we acha tu. Umasikini ndiyo unaponza watu na sitashangaa akishinda tena mwaka kesho. Kitururu - ndiyo kazi bado ipo, tena kazi kwelikweli si mchezo!

    ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU