NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Wednesday, April 15, 2009

RAISI WA BOLIVIA AMALIZA MGOMO WA KULA

Evo Molares - Rais wa Bolivia amemaliza mgomo wake wa kula uliodumu kwa siku sita. Raisi huyu machachari na mpigania haki za wazawa wa taifa lake alikuwa amegoma kula akilishurutisha Baraza la Kongresi la Bolivia kupitisha mabadiliko ya katiba ambayo, pamoja na mambo mengine, yatamruhusu kugombea tena uraisi kwa kipindi kingine cha miaka mitano. Raisi huyo alikuwa anapitisha muda wake akiwa amelala kwenye godoro lililokuwa limewekwa sebuleni katika makazi yake rasmi kama raisi wa Bolivia.

Katika siku hizo sita alikuwa anakunywa maji na kutafuna majani ya mmea wa Koka - ambao ndio malighafi-mama katika utengenezaji wa Cocaine. Mmea huo hutumiwa na wenyeji wengi wa Bolivia na nchi nyingine za Latin Amerika kama kizuia njaa ingawa Marekani inapigana vita vya kufa na kupona kujaribu kuuangamiza kabisa mmea huo.

Baada ya majadiliano makali hatimaye Baraza la Kongresi limepitisha mabadiliko hayo na sasa yuko huru kugombea tena uraisi. .

Nilikuwa sijawahi kusikia mgomo wa chakula ukitumiwa na kiongozi wa nchi kama silaha ya kubadilisha katiba ili kujiongezea muda wa kutawala. Sitashangaa mbinu hii ikiigwa na viongozi wa Afrika ingawa sina uhakika kama kweli wanaweza kukaa siku sita nzima bila kula.

2 comments:

  1. Hii kali. Nami sijawahi kusikia hii. Nadhani ni mpya kwa wengi. Nadhani ni njia nzuri kwa raisi kushurutisha ila inategemea anashurutisha nini. Kugombea tenaaaa? Pleaseeeeee.

    ReplyDelete
  2. lakini alikuwa anakunywa maji hivyo kajitibia sio mgomo wakula kivile

    ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU