NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Monday, April 20, 2009

VIJANA WETU "WATUNDU" TUNAWASAIDIAJE?

Ni kweli kwamba elimu yetu haitupi utundu na maarifa ya kuweza kujiajili. Tunategemea kuajiriwa baada ya kuhitimu. Ni kweli pia kwamba elimu yetu ni butu na haizichokonoi akili zetu na kuchochea udadisi wetu mpaka tukafikia kilele cha umakinifu na welewa wetu . Tunakariri tu, tunashinda mitihani, tunahitimu na kwenda kuukabili ulimwengu hivyo hivyo...Mbali na matatizo yote haya, bado tuna vijana wenye vipaji ambao, hata bila elimu hii tuijuayo, wameweza kufanya ugunduzi na kujitengenezea vifaa ambavyo vimethibitishwa kisayansi kuwa vinafanya kazi. Mfano ni huyu kijana hapo kwenye picha. Je, wagunduzi wetu hawa wanapata msaada wo wote wa kitalaamu (au kifedha) kuweza kuwaendeleza? Au ni yale yale ya kuoneana wivu, kupigana vita na kutokomezana? Kijana huyu anaingiza karibu sh. 45,000 kwa siku kwa kuuza hizi antena ambazo mwenyewe anazitengeneza. Vipi kama angepewa kibanda, akasaidiwa kifedha na utaalamu zaidi? Sera yetu inasemaje kuhusu Watanzania wagunduzi kama huyu kijana? (Picha kutoka gazeti la This Day tarehe 18/4/2009 - ukurasa wa mbele - kupitia blogu nzuri ya Kennedy)

No comments:

Post a Comment

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU