NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Thursday, May 14, 2009

HAPA KIPANYA ANATUAMBIA NINI???

Ni uthibitisho wa ile dhana kwamba Watanzania hatupendi kusoma vitabu? Au ni ile imani iliyoenea kwamba eti wazungu ni wadadisi na wasiochoka kusaka maarifa mapya - katika mazingira yo yote yale na kwa gharama yo yote ile? Kama ni kweli kwamba Watanzania hatupendi kujisomea, tumeshawahi kujiuliza ni kwa nini? Inawezekana kwamba pengine kusoma vitabu si njia pekee ya kujipatia maarifa. Au pengine vitabu vingi vina "maarifa" ambayo hayaendani na mazingira yetu na watu hawaoni sababu ya kupoteza pesa zao na muda wao kununua na kusoma vitu ambavyo havitawasaidia?

Vitabu tuliletewa na wakoloni na ni wazi kwamba tulikuwa na njia zetu za kurithishana na kupeana maarifa hata bila uwepo wa vitabu. Tunajua pia kwamba elimu yetu ya wakati ule kabla hatujaingiliwa na wakoloni ilikuwa ni elimu ya moja moja ambayo ilitufunza kutenda na kupambana na mazingira yetu ana kwa ana - siyo hii ya sasa ya kukariri vitabu wakati mwingine hata bila kujua unachokisoma na kukikariri kina maana au faida gani katika mazingira yako halisi. Nimechoka kusikia kila mara kwamba eti Watanzania hawapendi kujisomea. Wakati umefika sasa wa kujiuliza ni kwa nini hawataki kusoma vitabu na kama kweli ni lazima wasome vitabu ndiyo wapate maarifa, nini kifanyike!

13 comments:

 1. yaani vitu vingine bwana. nimeandika vitabu vitatu na kuvipeleka kwa wachapishaji wakavikataa eti havitalipa na hivyo navitafutia pesa kwani nina uhakika vitalipa tu na vitauzwa kwa sana. waadishi wengi wanaadika mambo yao ya shuleni kwa watu ambao hawajasoma wakidhani vtasomwa. watz wanahitaji vitu vya tofaut vinavyoendana na mazingira yao. naamini vya kwangu vitauza tu na kusomwa. kusoma kitu kizuri ni lazima na hivyo utalazimika kununua tu sio idea zilizooza za jamaa wanaojiona wanaweza kuandika kama nini.

  matondo una vitabu weye?

  ReplyDelete
 2. Kamala, unaweza kutupa title za vitabu vyako? Kwa vile una uhakika kwamba vitanunuliwa na kusomwa basi jitahidi uvichapishe - hata kama ni kwa pesa zako mwenyewe. Pia kama kuna kimoja unachopenda nikisome na kutoa maoni yangu, nitakuwa tayari kufanya hivyo. Mimi ninayo miswada hapa mingi tu ambayo nimeiweka kando kutokana na shughuli za kikazi. Baada ya mwaka mmoja hivi nitakuwa nimefikia lengo langu la kikazi nililokuwa nimejiwekea na nitakuwa na uhuru zaidi wa kumalizia na kupiga msasa miswada yangu. Vitabu vyangu viwili vya kitaaluma (isimu) viko kwa wachapishaji.

  ReplyDelete
 3. Wacha nianze kwa kutaka kutabiri sababu ya vitabu vya Kamala "kukataliwa". Ni kwa kuwa havina udaku, havina habari za kuchokonoa maisha binafsi ya watu, ama vinafikirisha, ama vinaelimisha zaidi ya upeo wa wavivu wa fikra. Jamii yetu (kwa bahati mbaya) inalazimishwa kuona kuwa UDAKU ndio jambo la kusoma, jambo linalolipa na linalohitajika kwa watanzania. Mauzo ya magazeti ya udaku yako juu sana ukilinganisha na magazeti ya kawaida. Watembeleaji wa habari za udaku na zenye kuhusu maisha binafsi ya watu, zenye kuchafua majina ya watu na kuumbuana ndio wengi kuliko watembeleaji wa habari za kufikirisha, kutambulisha na kukomboa. Yaani hata haya majamvi utaona kuwa kwenye habari za kiutambuzi, kiuchambuzi ama zenye mistari kadhaa ya kusoma, watu hawapiti na hata wakipita hawatoi maoni. Wanataka taswira tuu na zisiwe za maana ndio watajazana. Habari ndefu yenye kupata maoni lazima iwe yenye kumpa mtoaji maoni namna ya kukosoa. Wanataka picha zisizofikirisha.
  Tunarithisha kizazi upuuzi ambao utatugharimu saana kuusafisha. Kibaya zaidi ni kuwa wenye dhamana na uwezo wa kurekebisha ndio wenye kuendeleza haya.
  Kamala, andaa na chapisha kwa gharama zako kwani kitauza tuu. Wapo wenye uhitaji wa hayo usemayo kila siku kwenye blog na hata wasiotambua kupotea kwao, watatambua hilo muda si mrefu na kuvirejea.
  Blessings

  ReplyDelete
 4. MATONDO,

  moja wwapo ni 'kijana wa kizazi cha dotcom' kingine ni mauaji ya albino; ujinga na upotevu wa kiroho,

  kingine ni juu ya kutafuta wachumba kwa wakristo.

  kuna kingine juu ya malumbano ya mahakama ya kadhi na OIC niliogopa kukiendeleza nisijetangaziwa fatwa.

  ni vidogo tu vitakavyouzwa kwa bei rahisi na vina maudhui muhimu. nitaaangalia uwezekano wa kukutumia kimoja ili upitie na kuona kama sio vyote

  ReplyDelete
 5. Matondo,

  Nadhani kusoma vitabu kunaweza kuwa njia mojawapo ya kuongeza maarifa endapo tu msomaji atakuwa na nia ya kuelewa kwa kina kilichomo au kilichoandikwa kwenye kitabu. Napenda kumnukuu Dr Benjamin Carson, aliposema kuna wale ambao wanasoma vitabu kwa nia ya kufaulu mtihani na kuna wale ambao husoma vitabu kwa ajili ya kuongeza maarifa. Kwa ujumla tabia ya kupenda kusoma humfanya mtu kuwa na wigo wakuelewa mambo kwa upana.

  Mwisho, napenda kusema kusoma si njia pekee ya kuongeza maarifa.

  ReplyDelete
 6. Mzee wa Changamoto,

  Kimsingi, nakubaliana hoja yako kwa asilimia mia. Baada ya kupitia magazeti na blogs mbalimbali nimekuja kugundua wadau wengi hupendelea kutembelea tovuti zilozojaa udaku lakini kwa bahati mbaya zile ambazo zinaandika kuhusu masuala chanya haziangaliwi kabisa.

  ReplyDelete
 7. labda tujiulize ni kwanini udaku unapendwa mno kwani hii ni kwa dunia nzima na sio bongo pekee? kwa nini?

  ReplyDelete
 8. Chakusikitisha ni kwamba Afrika tunapoteza njia za kiasili za kufundishana na njia tulizoletewa kama za vitabu nazo hatuzitumii!:-(

  ReplyDelete
 9. Ndugu Kitururu, kuongezea hoja yako, ni kuwa kwa miaka mingi waAfrika tumelalamika kuwa hatutendewi haki na vyombo vya habari vya nje, kwamba vinatudhalilisha na kupotosha ukweli juu yetu.

  Sasa, wakati tunayo fursa ya kutumia tekinolojia za mawasiliano zilizopo leo, kama vile hizi blogu, tukaelezea habari za kweli na muhimu juu yetu na kuwaelimisha walimwengu na sisi wenyewe, sisi tunazitumia kupashana udaku :-)

  ReplyDelete
 10. @Prof. Mbele: Yaniinasikitisha kweli!:-(

  ReplyDelete
 11. tunahitaji kujenga msingi tanu awali wa kujisomea na kuwasaidia watoto wapende kujisomea.

  leo hii si ajabu mimi au wewe mara nyingi zangu tunazowanunulia watoto wetu au wa ndugu zetu mwaserere au magari ya 'midoli' ya chini na badala ya zawadi kama vitabu.

  wazazi,walezi watu wazima tunabidi tuwe cheche na chachu ya kusoma.

  kasafari bado karefu ila naamini tutafika tu

  ReplyDelete
 12. Kwa kweli watz hawapendi kusoma, vitabu kwa nini?
  hawataki kujifikirisha.mbona udaku unapendwa kote?
  mahala pengine watu wanasoma vyote udaku-kujiburudisha
  na vitabu-kupata maarifa

  ReplyDelete
 13. Tuongelee kuhusu vazi la Taifa

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU