NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Wednesday, May 6, 2009

KANISANI WAMENIUDHI

Wiki jana nilipeleka mtoto kanisani kwa ajili ya darasa lake la katikati ya wiki. Tulipoingia kanisani darasa lilikuwa bado halijaanza ingawa kulikuwa na watoto wengi pamoja na wazazi wao. Pengine kwa ajili ya kusubiri mwalimu afike, kulikuwa na slide show ya picha kutoka sehemu mbalimbali duniani - bustani nzuri na kangaroo kutoka Australia, mito na majumba marefu kutoka Japan, barafu na milima ya theluji kutoka Uswisi n.k. Ilipofika "zamu" ya Afrika zikaja picha za wagonjwa wa UKIMWI tena ambao wako nyang'anyang'a kabisa kiasi kwamba watoto walishtuka na wengine kufunika nyuso zao na kuanza kulia. Mhudumu mmoja wa kanisa aliyekuweko karibu na mitambo alizima ile slide show mara moja. Nimeandika barua ya kulalamika kuhusu jambo hili kwa uongozi wa kanisa. Kama mada ilikuwa ni uzuri wa mazingira kama walivyofanya katika mabara mengine - mbona wasionyeshe Mlima Kilimanjaro, Serengeti n.k. ilipofika zamu ya Afrika? Mbona wasionyeshe wagonjwa kutoka Australia, Japan na Ulaya? Au huko hawaugui na kufa? Inasikitisha sana kuona kwamba maoni ya kipumbavu na kibaguzi kama haya yamo mpaka makanisani - sehemu ambayo mtu ungetegemea kwamba kutakuwa na upendo, usawa na heshima kwa wote!

15 comments:

 1. Ni dharau ya hali ya juu ambayo WaAfrika bado tunahitajika kuipinga na kuipiga vita kwa kila hali. Nahisi hasira na uchungu wako, pole sana. Ina athari kubwa sana kisaikolojia hasa kwa mtoto anayekua.
  Pole sana!

  ReplyDelete
 2. Haya mambo yapo sana!

  Lakini tupo Waafrika ambao ndio tunayapeleka katika kuombea misaada. Nishawahi kuhudhuria kwenye kisemina cha mazingira na inta kalcha komunikesheni ambako kila mtu akiluwa anaonyesha mazingira ya kwao halafu mshikaji mmoja MBONGO tuliokwenda naye nafikiri alionyesha mpaka picha za janga la njaa Ethiopia. Nilipomuuliza akaniambia wewe tulia kabla semina haijaisha hii ni gia yakuombea misaada.  Na kama unakumbuka enzi za APATHAIDI Afrika kusini, walikuwa wana halalisha kabisa kuwa siye Waafrika sio watu kamili makanisani.

  Na karibu wote hao wako hai!:-(

  Inasikitisha!

  ReplyDelete
 3. matondo na uprof waka MNANIAIBISHA!

  hujasoma historia? hujui kuwa dini na hasa ukristo ni kitovu cha ubaguzi mpaka leo hii? hujui kuwa Yesu kristo na wafuasi wake ni wazungu, wazee wote muwasomao ni wa zungu isipo kuwa shetani ndiomwafrika?

  hujui kuwa toto la Nuhu jinga ndilo lililozaa waafrika? soma mwanzo 24.

  unampelekamwanao kanisani kwa lengo lipi? ili asome na kujua sehemu ya imani za dunia hii au ili ajikane na kujikataa na kujiona mzungu?

  unanihaibisha kutokujua kuwa dini ni kitovu cha ubaguzi

  ReplyDelete
 4. Da Subi, huyu mtoto ana miaka minane na bado hajafika Afrika (Tanzania). Sasa analia kila mara na kunionea huruma kwamba ninatoka huko kwa wagonjwa wa ajabu. Bila shaka zile picha zilimtisha sana. Nina mpango wa kumpeleka Usukumani akapaone na pengine hii itabadili msimamo wake. Mwanafalsafa Kitururu, nakubaliana nawe: sisi hasa ndiyo wa kulaumiwa kwa kukubali kubaguliwa na kujidharau sisi wenyewe. Kama alivyosema Eleanor Roosevelt - mke wa F.D.R aliyekuwa rais wa Marekani - Nobody can make you feel inferior without your consent. Kazi tunayo!

  ReplyDelete
 5. Kamala, naona shoka lako la UTAMBUZI limenishukia tena bila huruma. Ningekuwa sikufahamu wewe ni mtu (mwenye msimamo) wa aina gani ningejitetea, ningeutetea Uprof. wangu na hata pengine ningeanza kuchukua madarasa ya yoga na utambuzi. Sitafanya hivyo. Naomba niseme jambo moja tu kwamba, nadhani watu wengi tunafahamu matatizo na matumizi mabaya ya dini za Kimagharibi (mfano mateso yaliyoletwa na kanisa la Roma, dini kutumiwa kama chombo cha ugandamizaji n.k). Kinachoifanya dini iendelee kuvutia watu - mbali na ahadi zake za kuishi raha mustarehe paradiso milele na milele - ni ile moral code yake. Mbali na mambo mengine wazazi wengi tunapeleka watoto makanisani ili tukasaidiwe malezi, tukiomba na kuamini kwamba watoto wetu hawa tuwapendao wataweza kuziheshimu Amri za Mungu - wakijiheshimu wao wenyewe pamoja na binadamu wenzao wanaowazunguka. Kwamba wakiweza kuwatendea wengine kama wanavyotaka wao watendewe basi tutakuwa tumepata watoto ambao watafanikiwa - wao pamoja na jamii yao. Hali huku ughaibuni tuliko ni mbaya zaidi na malezi ya watoto ni mojawapo ya mitihani migumu kabisa ambayo wazazi tunapambana nayo. Ndiyo maana ninampeleka binti yangu kanisani. Pengine badala ya kwenda kanisani itabidi sasa nimtafutie madarasa ya UTAMBUZI na yoga!

  NB: Nimeshaona mabadiliko makubwa katika mtazamo wako kuhusu kuheshimu maoni ya watu wengine wanaotofautiana nawe kimtazamo pamoja na lugha unayotumia katika comments zako mbalimbali tangu uweke ile post yenye kichwa cha habari "Prof. Mbele: Bingwa wa Mijadala". Kama ulivyosema, naamini kwamba ulijifunza kitu cha muhimu katika mjadala huo. Endelea kufanya hivyo!

  ReplyDelete
 6. ndio prof. kuwa makini, namaanisha umeshafaanya utafiti wa kutosha kuwa amri za dini ni ngumu kufuata au hazifuatiki. huyu mwanao kama ni wakike inabidi uwe makini kwani wahubiri wanatabia ya kuwabaka na kuwalawiti watoto wadogo hata hapa bongo lakini marekani ndo wanaongoza hasa wakatoliki (kama wewe ni mkatoliki= wagwerwa!)

  sasa unadhani kuna nini hapo?

  ndio, madarasa ya utambuzi ni muhimu kwani mwalimu wa utambuzi sio kama mhubiri, mwalimu huyu atakwambia utende jambo analolitenda yeye. wanafundisha kupitia uzoefu na sio zile za 'unisikilize ninayosema na sio ninayotenda'

  kujitambua ndio elimu muhimu ya kuokoa kizazi cha sasa. mfano halisi ni mimi imeniokoa kutoka mbali sana.

  hata hivyo nakubaliana nawe, ukrito una vitu falani vinavyovutia sana kwa kweli kimwili japo sio kiroho

  ReplyDelete
 7. Natamani kama ningekuwa nawe kwa kweli nadhani kwa hasira zangu ningewauliza pale pale. Kwani hii inatokea kila mara utasikia Afrika kuna njaa Afrika hwana nguo nk. Halafu wao wanakwenda kutembelea MBUGA ZETU NZURI NA MLIMA WETU MRURI. Lakini badala ya kuonyesha hizo wanaacha na kuonyesha mabaya tu kuhusu AFRIKA. Mungu roho inaniuma sana tena sana. Ni kweli ni dharau kubwa sana.

  ReplyDelete
 8. Dada Yasinta, sijui kwenu huko Sweden lakini hapa Marekani ukisikia Afrika inatajwa ni lazima kuwe na janga fulani - njaa, vita, magonjwa na hivi karibuni hawa "majambazi" wa baharini wa Somalia. Utafikiri kwamba sisi tunachofanya ni kupigana, kufa kwa njaa na magonjwa tu. Ni kweli hakuna kitu kizuri ambacho watu hawa wanaweza kuwafundisha watoto wao? Hawajanijibu barua yangu na sijui watasema nini.

  Kamala umenichekesha kuhusu suala la watoto kubakwa na kulawitiwa. Hata huko kwa Wakatoliki ni mapadri wachache waliofanya hivyo vitendo. Pengine unatumia ile methali yetu kwamba samaki mmoja basi wameoza. Suala hili la kubaka na kulawiti watoto ni suala la mtu mmoja mmoja na mimi naamini kwamba watu hawa wana matatizo ya kiakili au pengine wanahitaji elimu ya UTAMBUZI. Je, una uhakika kwamba watu wa UTAMBUZI kamwe hawawezi kutenda jambo kama hili? Siku moja ikitokea mtu wa UTAMBUZI (siyo wewe) akabaka au kulawiti katoto itakuwaje?

  ReplyDelete
 9. kaka Matondo Ulaya ni Ulaya kwote ni hivyohivyo hawaongei mambo mazuri kuhusu Afrika yetu ni mambo kama hayo hayo magonjwa, njaa na pia kuwa tu wachafu, na kuchafu kusema kweli inasikitisha sana. Cha ajabu wanapenda kwenda Afrika

  ReplyDelete
 10. Profesa Matondo, inabidi nikupongeze kwa msimamo wako thabiti kwa kuweza kuwaandikia uongozi wa kanisa. Hakika kitendo walichofanya ni cha udhalilishaji, japo Afrika kulingana na mataifa ya magharibi ni kitovu cha umasikini na maradhi.

  Lakini ukweli unabakia pale pale daima, Afrika itabakia kuwa lulu ya furaha pamoja na umasikini wetu kulinganisha na maisha ya ubinafsi na uchoyo waliyonayo wenzetu wa magharibi.

  Ni mara chache sana kusikia eti mwafrika anajiua kwa kujisikia mpweke, kama ilivyo kwa wenzetu weupe. Ni maisha ya namna gani mtu anafia ndani ya nyumba yake hata jirani hana habari,mpaka harufu ianze kunuka ndiyo wanapata kuja mtu kafa hapa, yote haya sababu ya ubinafsi na uchoyo.

  Binafsi sijisikii raha yeyote kuishi hapa Ulaya zaidi ya kuchuma vihela vyao.

  ReplyDelete
 11. Daudi Kaghembe.May 7, 2009 at 8:29 PM

  Daktari Matondo umenishtua kidogo kusikia mwanao ana miaka nane na hajawahi kufika nyumbani Tanzania. Je, anazungumza kiswahili? Jitahidi mkuu uwe unawapeleka nyumbani angalau kila baada ya miaka miwili.Hii itawasaidia kujifunza mambo mengi kivitendo badala ya nadharia tu. Mimi mwanangu alikuja huku (UK) akiwa na miaka mitatu (sasa ana miaka nane) lakini anaongea kiswahili kizuri tu (japo lafudhi ina utata) na ana ufahamu na mambo mengi ya nyumbani.

  ReplyDelete
 12. Malkiory - "Binafsi sijisikii raha yeyote kuishi hapa Ulaya zaidi ya kuchuma vihela vyao" Nakubaliana nawe. Wengi wetu tupo hapa kwa sababu mbalimbali - kubeba maboksi, elimu ya watoto, huduma za afya n.k. Kuhusu maisha ya kijamii ni ZIRO. Jirani yangu hapa ni polisi na siku moja moja huwa tunapungiana mikono, na siku zingine tunapishana kila mtu kivyakevyake. Inaudhi kama nini mtu unapogundua kwamba huna chumvi na inabidi uendeshe maili tatu nne kwenda kuitafuta madukani wakati ungeweza tu kwenda kwa jirani akakusaidia. Ajabu ni kwamba mambo haya yanakuja kwa kasi hata huko nyumbani - ubinafsi, uchoyo vinatawala sasa na maisha yetu ya kusaidiana, kujaliana na kushirikiana yanakufa (hasa sehemu za mijini). Ni huzuni kwa kweli.

  Bwana Kaghembe -usishtuke. Huku ni mbali sana na mtu kwenda nyumbani inabidi ujipange sawasawa ukizingatia kwamba ukifika kijijini watu watataka kuona "matunda" ya Marekani. Pengine wewe unaweza kwenda nyumbani mara kwa mara kwa sababu ni karibu kidogo na muhimu zaidi si mbeba maboksi na kwa hivyo una uwezo wa kufanya hivyo. Mbeba maboksi kama mimi nitaweza wapi kwenda Usukumani mara kwa mara? Tuwasiliane ili nami unipe mikakati mipya ya kupambana na maisha haya ya ughaibuni bwana.

  NB: Binti Kiswahili anacho cha kuombea maji. Yeye alizaliwa hapa na kumswahilisha ni kazi kwelikweli. Kama mwanao alikuja UK akiwa na miaka mitatu tayari alikuwa ameshapata misingi imara ya Kiswahili na ningeshangaa kama angekisahau mara moja. Suala la lafudhi hilo linaeleweka kwani pengine mkazo (stress) wa Kiingereza na Kiswahili vinaingiliana. Hilo ni jambo la kawaida kwa watu wanaomudu lugha zaidi ya moja.

  ReplyDelete
 13. wewe ni mwalimu wa kiswahili na bila shaka unfundisha kiswahili japo mwanao hajui kiswahili = muujiza wa nguuuvu

  mimi sijasema wanautambuzi hawawezi kubaka bwana mzee. nao ni binadamu kama binadamu wengine. au kwa uhakika zaidi ni kuwa, hata mimi nafanya ngono! ila wanautambuzi wanajitahidi kutokuongozwa na hisia na wakiona hisia zinawazidi, basi wanaweka mambo hadharani. kwa mfano, hawaoi ili waweze kufanya ngono na wanawake/waume wengi wawapendao, nk

  nalinganisha mapadre na ngono kwa sababu hawaoi kwa utaukufu wao. ni muujiza kwa mtatkatifu aliyeshinda tamaa za mwili kubaka na kulawiti huku watakatifu wenzie wakishindwa kumtambua mpaka afumaniwe na kushitakiwa harafu waumini waombwe sadaka ili waje kumkomboa kwa kutumia matoleo ya waumini. ni vizuri tukiwa wakweli bwana kuliko kujifanya kuwa vile tusivyo au kujitia kuchukia tunayoyapenda na kuwazuia wengine kufanya yale tuyafanyayo kwa sana

  ReplyDelete
 14. Daktari Matondo nani kakwambia mimi si mbeba boksi? Mimi pia nabeba boksi mkuu, hivyo kwenda nyumbani mara kwa mara ni dhamira tu. Kwa upande mwingine nakubaliana nawe kuhusu ughali wa nauli kwa kutokea huko Marekani kwani kabla ya kuja huku (UK) niliwahi kuishi Lansing City, Michigan state kwa takriban miaka mitatu hivyo naelewa unachokisema. By the way, kuna bwana mmoja niliishi naye vizuri sana nikiwa huko, anaitwa Deo Ngonyani, yeye ni profesa wa lugha za kiafrika (kama sijakosea) yuko Michigan state university, je mnafahamiana? Kama hamfahamiani basi nitafurahi kusikia mnatafutana. Naye nitamuuliza kuhusu wewe nadhani bado nina namba zake za simu.

  ReplyDelete
 15. Kamala, unanifurahisha sana kwa comments zako. Mwalimu wa Kiswahili + Mtoto asiyezungumza Kiswahili = Muujiza wa nguvu. Ni lazima tuingize mazingira katika hiyo fomyula yako Mulangira na pengine tutaweza kupata jibu tofauti kidogo. Nilipokuwa mtoto nilikuwa nikiwaona mapadri/maaskofu na majoho yao na kuwaona kuwa ni watakatifu kweli kumbe nao ni binadamu tu kama sisi.

  Bwana Kaghembe (ingekuwa Kagembe lingekuwa jina la Kisukuma). Ndiyo, kwenda nyumbani kutokea huku ukiwa na familia inabidi mtu ujipange sawasawa. Huwa nachepuka mwenyewe tu kila ninapoweza, japo dhamira ninayo ya kuwapeleka watoto kwenda kunywa maziwa ya Usukumani.Profesa Ngonyani namfahamu sana na huwa tunawasiliana mara kwa mara. Alifiwa na mke wake mwaka jana (kama hufahamu)

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU