NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Tuesday, May 26, 2009

MASHINDANO YA UREMBO KILA KONA - UTANDAWAZI HUU UNATUPELEKA WAPI?

Wanablogu wenzangu, nilikuwa nimebanwa na pilikapilika za kubeba maboksi kwa wiki moja na ushee hivi. Sasa nimesharudi na kama kawaida tuendelezeni mapambano ya kuipigania jamii.
==================================================================
Inavyoonekana sasa kila kona ni mashindano ya urembo. Juzijuzi hapa nilisoma katika magazeti kwamba kulikuwa na mashindano ya kumtafuta Miss Maswa - wilaya moja katika Mkoa wangu wa Shinyanga. Halafu tena nikasoma kuhusu mashindano ya kumtafuta Miss. Malampaka - kakitongoji kamoja kule kule Shinyanga. Na karibu kila siku ukisoma gazeti ni lazima utakutana na aina fulani ya mashindano ya urembo mpaka haya mashindano Miss Landmine kutoka Angola.

Kwangu mimi naona kuna ruwaza (pattern) fulani hapa. Kwa kawaida sisi tunayo tabia ya kuiga vitu hata kuwazidi hao tunaojaribu kuwaiga, na hili si jambo la kufurahisha. Na katika haya mashindano ya urembo nadhani tunafanya vivyo hivyo - tena kwa kutumia vigezo vile vile vya hao mabwana wetu wenye utamaduni wenye hadhi. Tukiendelea hivi nadhani mwishowe tutakuwa na Miss Tarafa, Miss Kata, Miss Kijiji na hata Miss familia. Sijui tunaelekea wapi. Wakati mwingine hata nawasikitikia hawa dada zetu wanaojikondesha ili waweze kushiriki haya mashindano ya "urembo".

Mambo yamebadilika kwa kasi sana kwani juzijuzi tu hapa wembamba kwa Mwafrika ulikuwa ni dalili ya matatizo ya kiafya na watu walipendelea mwenzi aliyetakata. Na kutokana na mazingira ya kufanya kazi sana, wenzi hawa waliotakata hata hawakuwa na matatizo ya kiafya mengi kama saratani, kiharusi na shinikizo la damu - magonjwa ambayo sasa yanaenea kwa kasi bila kujali kama mtu amejikondesha ama la. Kwa ujumla utandawazi unavuruga kila nyanja ya maisha yetu. Sijui tunaelekea wapi.


4 comments:

 1. Mashindano ya umiss ni moja ya mia ya mambo tunayopaparuk
  ia,ni matokeo ya utandawazi na kwa vile ni dili acha waend
  elee lkn waelimike kwanza!

  ReplyDelete
 2. Ni kweli kabisa hata mimi hili jambo limekuwa likinipa kero. Kwani ni hatari kwa taifa la kesho. Yaani utakuta visichana vidogo sasa navyovimeanza kuacha kula kisa anataka kuwa mwembamba kama miss fulani.

  Hata sijaelewa kwa kwa nini kuwe na mashindano ya MREMBO kwani akili yangu ilikuwa inasema watu wote hapa duniani ni warembo. Sikujua kama Mungu aliumba kitu kibaya. Nami nasema kkwa kweli inasikitisha sana na kuogopesha.

  ReplyDelete
 3. Swali zuri, swali muafaka na swali lenye ukweli ndani yake.
  Umeshawahi kuona mtu analia msibani kuliko mfiwa? Lazima watamshangaa. Ndivyo tunavyoshangaliwa sisi tunaoonekana kuiga kuliko walioanzisha. Lakini hii haijaanza leo. Tazama Imani (hasa kwa wewe Kaka unayeishi Magharibi na ukishaishi nyumbani). Tumeiga kuliko ilivyo. Tumepindisha vitabu vitakatifu mpaka ni kero na nina imani kuwa waliosambaza dini hizi wakirejea Tanzania ya leo nao watashindwa. Maana tuna-modify mpaka tunapitiliza.
  Haya ya urembo ndio usiseme. Wanajichubua, wanajikondesha, wanavaa-uchi, wanatembea kwa kujiwekea kibiongo biongo, wanajilisha vyakula vya ajabu ili tu wawe kama wanavyoona kweney Tv bila kutambua kuwa si kila kionekanacho humo ni maisha halisi ya mtu.
  Utandawazi umefuta MSATRI MWEMBAMBA ULIOPO KATI YA MAIGIZO NA MAISHA HALISI na sasa wasiouona wanaishi kimaigizo katika maisha halisi.
  Bushman alisema "it's funny how people can be carried away"
  Blessings

  ReplyDelete
 4. Visit my site: http://www.concourseurovision.webs.com

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU