NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Tuesday, May 5, 2009

TUZO ZA HESHIMA KWA WANAFUNZI BORA

Habari hii nimeipata kwa Michuzi Mdogo na iliwahi kuongelewa katika blogu mbalimbali. Ni wazo zuri sana hili kwani litasaidia katika kuhamasisha vijana wetu wasome kwa bidii. Ni wazo ambalo wizara ya elimu inapaswa kuliunga mkono.


Wanafunzi Bora Tz nao Kuneemeka na Tuzo za Heshima

Tuesday, April 28, 2009
Profesa,Wakali Kwanza,Tundaman kusindikiza tuzo za Wanafunzi bora TZ.

Hii ni kwa mara ya kwanza kabisa nchini kushuhudia tuzo za elimu zikitolewa kwa wanafunzi waliofanya vizuri kwenye ngazi za shule za msingi pamoja na sekondari na katika utoaji huo wa tuzo wanamuziki mbalimbali ambao ni Profesa Jay,QJ na Makamua,Tundaman,Spark pamoja na kundi zima la Bongo Dar-Es-Salaam wakiwemo kusindikiza utoaji wa tuzo hizo mwezi ujao ndani ya viwanja vya Leaders.

Tumezoea kusikia tuzo zinatolewa kwa wanamuziki bora,waigizaji bora wachezaji bora na tuzo nyingine mbalimbali lakini kwa hapa nchini hatujawahi kusikia tuzo zinatolewa kwa wanafunzi bora nchini lakini kwa mara ya kwanza PTECHS inakuletea tuzo kwa wanafunzi bora nchini ambazo zitakuwa na lengo moja kuu na la muhimu la kutaka kuwapa moyo wanafunzi ili waweze kufanya vizuri na kuinua elimu nchini.

Mmoja wa waandaaji wa tuzo hizo za elimu,Godfrey Maginga alisema kwamba yeye pamoja na wenzake waliweza kukaa chini na kujiuliza maswali kwanini kila siku zinaibuka tuzo mbalimbali na elimu inakuwa inapewa kisogo na ndiyo maana wameamua kuchukua uamuzi wa kuandaa tuzo hizo maalumu kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari Tanzania.

"Kila siku tunasikia tuzo kwa wasanii mbalimbali lakini hata siku moja hatujawahi kusikia tuzo kwa wanafunzi ambao ni kizazi chetu cha kesho hivyo ndiyo maana tuliamua kuandaa tuzo hizi za wanafunzi wanaofanya vizuri nchini"Alisema Godwin Maganga.

Akielezea kuhusu mchakato mzima wa tuzo hizo,msemaji huyo alisema tuzo haziwezi kutolewa bila ya burudani yeyote ile hivyo kusindikiza utoaji wa tuzo hizo wameamua kuwaalika wanamuziki mbalimbali ambao nao watahamasisha wanafunzi kushiriki mashindano ambayo yanawapelekea kupata tuzo hizo pamoja na burudani.

Bongo 5 iliweza kuongea na baadhi ya wanamuziki hao ambao watatoa burudani siku hiyo na walisema kwamba ni moja ya changamoto ambayo itaweza kuamsha juhudi za wanafunzi nchini kufanya vizuri mashuleni.

"Kwakweli ni moja kati ya tuzo ambazo zitawapa mwamko wanafunzi wa kusoma kwa bidii ili waweze kupata tuzo hizo"Makamua.

Naye Profesa Jay,mzee wa mitulinga alisema kwamba tuzo hizo ni moja kati ya tuzo zinazotakiwa kupewa heshima zake nchini kwa kuwa ni moja kati ya tuzo ambazo zinaweza kuibua viongozi wa kesho.

Tuzo hizi zinatarajiwa kutolewa may 23 ndani ya viwanja vya Leaders.

No comments:

Post a Comment

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU