NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Friday, June 19, 2009

DEGE (BOEING 777) LATUA SALAMA BAADA YA RUBANI KUFARIKI LIKIWA ANGANI

Dege la shirika la ndege la Continental aina ya Boeing 777 likiwa na abiria 247 likisafiri kutoka Brussels kwenda Newark, New Jersey Marekani limetua salama baada ya rubani wake mwenye umri wa miaka 60 kufariki ghafla dege likiwa angani tena juu ya bahari ya Atlantiki. Baada ya rubani huyo kufariki tangazo lilitolewa kama kulikuwa na daktari miongoni mwa abiria na abiria kadhaa walikwenda katika chumba cha marubani. Rubani wa ziada ambaye kwa kawaida huwa anaambatana na marubani wengine katika safari ndefu kama hii alikwenda na kuchukua nafasi ya rubani aliyefariki. Mpaka dege linatua Newark abiria wengi hawakujua kilichokuwa kinaendelea. Kwa habari zaidi bofya hapa.

Tarehe 29 Machi, 2009 rubani wa ndege ya shirika la ndege la Precision liyokuwa inaruka kutokea Mwanza kwenda Kilimanjaro (KIA) alipoteza fahamu baada ya ndege kuruka kutoka uwanja wa ndege wa Mwanza. Inavyoonekana kulikuwa na msukosuko mkubwa kwenye ndege baada ya tukio hili. Tembelea hapa kusoma maelezo ya abiria mmoja (anayejitambua) aliyekuwa katika ndege hiyo. Kwa watu kama mimi ambao hatujitambui sawasawa na ambao tunaogopa kusafiri kwa ndege sijui hii ingekuwa na athari gani kwetu kisaikolojia. Kamala, tunahitaji msaada wako hapa!

1 comment:

  1. Hiyo ishu ya Precision air kidogo inatisha dah. Ningekuwa abiria hata mimi ningekemea mapepo kama abiria wengine walokole walivyofanya.

    Hiyo ya Continental Airlines inaogopesha sana lakini unaweza kuona professionalism ya wenzetu. Safari za mbali wanasafiri na rubani wa ziada. Kwetu sisi who cares? Ndege zenyewe zimechokaaa kama mkweche wa basi unaosafirisha mkaa pale kijijini kwetu Maganzo.

    ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU