NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Friday, June 19, 2009

HIKI CHOO NIMEKIPENDA

Hebu tazama ubunifu huu wa Mwafrika - choo safi kabisa (tena inavyoonekana ni cha "kisasa") ndani ya mbuyu. Hapa hakuna haja ya kiyoyozi wala kipasha joto bali necha ndiyo inatawala.

Mbuyu umekuwa ukitumiwa kama makazi na makabila mengi yanayoishi sehemu kame ambako ndiko hasa mmea huu unastawi vizuri mf. Watindiga na Wafulani. Kuweka choo cha kisasa ndaniye ni kupanua tu matumizi yake ya tangu zamani ingawa si ajabu watu wanaotetea mazingira wakadai kwamba kitendo kama hiki cha kuugeuza mbuyu kuwa choo si kitendo cha kujivunia kwani kinahatarisha maisha yake.

6 comments:

 1. Mheshimiwa, hapa nimekupigia saluti, hii tutainukuu

  ReplyDelete
 2. Kweli watu wanajua kubuni. Hii safi sana

  ReplyDelete
 3. Yaani jamaa kajitahidi sana anastahili sifa, inamaana mbuyu hauendelei kukua tena? lasivyo sijui baadae itakuwaje

  ReplyDelete
 4. mh> nakumbuka kula mapera na kujisaidia sehemu, uliota mpera kule kwetu! nikiwa kwetu huwa nawaangalia wala mapera na kusema kimoyo moyo; mngejua chanzo chake?? labda haina maana japo yawezekana alijisaidia ndege na kutesha mbuyu kwa hiyo labda choo ni historia ya ulikotoka

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU