NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Sunday, June 19, 2011

LEO NI SIKU YETU AKINA BABA....

 • Kwa akina baba wote - waanzilishi na walinzi makini wa mfumo dume. Leo ni siku yenu ya kukumbukwa kwa mchango wenu katika uzazi na malezi ya watoto. Nami nachukua nafasi hii kuwatakia akina baba wote maisha marefu na umakinifu zaidi katika malezi ya watoto.
 • Mimi kwa bahati mbaya (au bahati nzuri sijui!) sikuwahi kumwona baba mzazi kwani aliitwa na Mungu wakati nikiwa na miezi mitatu tu. Jamaa enzi zile wakachoma na picha zake kabisa kwani hawakuona haja ya kutunza picha za mtu aliyetangulia mbele ya hukumu. Leo nami nina watoto na ninajaribu kuwapa upendo wa kweli na kuwafundisha yale niliyojifunza kule Unyantuzu. Akina baba popote mlipo - Happy Father's day!
 • Kwa vile mimi ni mpenzi mkubwa wa "Country music", huyu hapa Keith Urban na Song for dad.

2 comments:

 1. Hizi kalenda wee acha tu !Mie sitashanga tukuambiwa tarehe fulani ni siku ya kinyeo!:-(

  ReplyDelete
 2. @Mku Masangu: Unajua sikujua Country Music kwako inapanda aisee!


  Kuna siku moja Papaa Mubelwa BANDIO aka Mzee wa CHANGAMOTO ambaye karibu kila posti ya kwenye blogu yake huwa anaishibisha kwa reggae alinishangaza pia kwa kunukuu miziki fulani ya COUNTRY mpaka naye ingawa sijamuuliza ila nahisi Country music inapanda ingawa pale kijiweni kwake kitisha toto unawaweza kufikiria anasikiliza Roots Reggae pekee na hata ndombolo haipandi aisee!:-(

  Samahani nimepitiliza!:-(

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU