NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Friday, June 12, 2009

MAGAZETI YA UDAKU - OBAMA NI SHOGA!!!

 • Magazeti ya udaku likiwemo hili la Globe yamekuwa yakiandika, tena kama habari kuu katika ukurasa wa mbele kabisa, kwamba Obama ni/alikuwa shoga. Mwanaume mmoja aitwaye Larry Sinclair amekuwa akidai kwamba alikuwa mpenzi wa Obama kwa miaka mingi wakati ule akiwa bado seneta kule jimbo la Illinois; na kwamba walikuwa wanatumia madawa ya kulevya pamoja. Kashfa hizi zilianza zamani wakati Obama bado akiwa mgombea wa uraisi na bado zinaendelea. Larry Sinclair amekuwa akidai kwamba yeye pamoja na mwanaume mwingine shoga aliyekuwa mwimbishaji wa kwaya katika kanisa la zamani la Obama kule Chicago (huyu aliuawa mwaka 2007) waliwahi kuwa na uhusiano wa kishoga na Obama. Hata hivyo alipopewa "polygraph test" ili kuweza kujua kama alikuwa anasema ukweli ama la kuhusu kashfa hizi, alishindwa na matokeo yalionyesha kwamba alikuwa anadanganya.
 • Nyumbani sisi bado tunafikiri kwamba kila kitu kinachoandikwa katika gazeti au kuwekwa mtandaoni ni cha kweli lakini hawa wenzetu wanajua kwamba huu ni udaku na hakuna mtu ambaye anajali. Ndiyo maana Obama aliweza kushinda uraisi pamoja na magazeti haya kuandika udaku wote huu. Siku tutakapoweza kung'amua kwamba mambo mengi yanayosemwa katika magazeti (hasa haya ya udaku yaliyofumuka kila kona ili kuishibisha kiu ya utandawazi) ama si ya kweli au hayajathibitishwa basi tutakuwa tumepiga hatua kubwa. Nimeandika makala ndefu yenye kichwa "Ze Utamu Imetufundisha Nini?" kuhusu jambo hili na makala hiyo itatoka katika gazeti la Kwanza Jamii la Jumanne tarehe 16/6/2009. Nitaiweka hapa baadaye kidogo.
 • Ishu hii bado inaendelea. Bofya hapa kuona jinsi hawa jamaa wa Globe walivyoishikia bango.

13 comments:

 1. Dah!!! Hapa nimejifunza kitu!

  ReplyDelete
 2. ndio maana wanatulazimisha sisi wa afrika kwa kuwa wao ni machoko

  ReplyDelete
 3. inawezekana ikawa kweli haiwezekani ashabikie vitendo vya kishoga aliyakuwa yeye rijali

  ReplyDelete
 4. LIES LIES LIES

  ReplyDelete
 5. lisemwalo lipo ngawa si asilimia zote.

  ReplyDelete
 6. uongooooooo na ifutwe hyo habari tuuuu?

  ReplyDelete
 7. Soma habari za udaku na skendo kwenye mtandao huu mpya kabisa na wa kisasa udaku leo

  ReplyDelete
 8. Non sense story,no prove

  ReplyDelete
  Replies
  1. Do you know Swahili sir? That's the whole point of the author - to show that not everything that is put in the internet is true. And fellow Tanzanians should ignore most of the crap they find on the net!

   Delete
  2. i think so he doesn't know swahili

   Delete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU