NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Wednesday, June 3, 2009

UJIRANI GANI HUU??? - WAZUNGU KWELI KIBOKO

Naona huyu mzee haamini kama kweli jirani yake anaweza kumfanyia hivi. Lakini kwa wazungu hili si jambo la ajabu. Sisi Waafrika tunayo namna yetu ya kutatua ugomvi na misukosuko - ikiwemo kupigana vijembe kwa kutumia lugha ya mafumbo kupitia kwenye kanga, nyimbo, umbea na kwingineko. Yote kwa yote mnaweza kupigana vijembe na mwishowe mkaanza tena kuombana chumvi na unga pamoja na kuazimana kanga na vipodozi. Ubinafsi wa hawa wenzetu umepindukia kimo - kila mtu na lwake na mkikosana kidogo tu usije ukashangaa akakufanyia kama huyu babu alivyofanyiwa. Na hapo huwezi kumfanya lolote kwani hiyo "decoration" ipo katika yadi yake na ukivuka hilo geti la mbao tayari unakuwa umeingilia himaya yake. Kazi kwelikweli. Halafu eti ndiyo tumekazana kuwaiga hawa jamaa pamoja na tabia zao.

9 comments:

 1. Hahahahaa!! hii kiboko,sasa hapo tuseme ndio anamwambia aongee na........kaaaaazi kweli kweli,ah sisi ni mwendo wa khanga tu,ujumbe unafika.

  ReplyDelete
 2. Ha ha ha haaaa kweli kazi kwelikweli. Ila wazungu wana mambo yaani hata ukitaka kukatisha njia ya mkato kwenye uwanja wako kasheshe mno.

  ReplyDelete
 3. hapo nadhani anamwambia kiss my fuckin ass!ashakum!hivi wakubwa tufanye nn kujikwamua ktk halii ......utumwa wa kifikra...kila cha hao weupe ni kizuri na chafaa kuigwa

  ReplyDelete
 4. akikuuzi pitia mumyhery umalize udhia

  ReplyDelete
 5. Ningekuwa mimi ningepandikiza wadudu wanaokula huoa mmea ili waule wote

  ReplyDelete
 6. This comment has been removed by the author.

  ReplyDelete
 7. Bennet, siyo wote wana utalaamu wa mimea na wadudu. Hapa mimi ningemzukia usiku na kuumwagia sumu ya kukausha majani within 1 hour. Hii inauzwa madukani na haihitaji utaalamu wo wote.

  ReplyDelete
 8. NI HAKIKA KUWA HAYA YAKIFANYIKA NA KUZINGATIWA TUTAPUNGUZA KUONGEZEKA KWA HILI GONJWA.

  www.harusiyetu.blogspot.com
  www.ajirazetu.blogspot.com

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU