NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Monday, August 17, 2009

HATA ADOLF HITLER ALIJUA

Adolf Hitler (1889-1945), yule dikteta hatari aliyetaka kuitawala dunia nzima, alijua kwamba nguvu na mamlaka yake yalitegemea "ujinga" na kutofikiri kwa umma. Alisema hivi:

"What luck for rulers that men do not think"

Rais George W. Bush (II) yeye alisema hivi:

“You can fool some of the people all the time, and those are the ones you want to concentrate on.”

Ni mambo mangapi ambayo wanasiasa, viongozi na "watawala" wasingeweza kuyafanya kama wangekuwa wanatawala umma unaofikiri? Nchi kama yetu na Afrika kwa ujumla ingekuwa wapi kama umma wake ungekuwa umeamka?

Mwanamapinduzi Che Guevara alisema "I am not a liberator. Liberators do not exist. The people liberate themselves." Dawa ya ufisadi, uonevu, rushwa na matatizo mengine mengi yanayotukabili ni umma ulioamka. Na watawala wetu wanajua hivyo.

5 comments:

 1. Nakunukuu...."Dawa ya ufisadi, uonevu, rushwa na matatizo mengine mengi yanayotukabili ni umma ulioamka. Na watawala wetu wanajua hivyo."
  Umemaliza Kaka.
  ASANTE

  ReplyDelete
 2. mambo yanapendeza pale yule anayepaswa kuwa liberate wengine anapokuwa ndiye mdanganyaji au kulazimika kukwaa visiki vya wadanganyaji wale!

  we unaona dalili ya kuamka bongo?

  suruhu ni kujitambua tu, ndipo mambo yatakapoeleweka mzee

  ReplyDelete
 3. Wakati mwingine mimi huwa nafikiri kwamba tunahitaji elimu kama mkombozi ili tuweze kufunguka macho na kuona madhila tunayotendewa na watu tuliowapa dhamana ya maisha yetu.

  Haiingii akilini watu tuiowapa dhamana ya maisha yetu wanajinufaisha wao tu. Kikikaribia kipindi cha uchaguzi basi wataongea mpaka mishipa kuwasisimama lakini moyoni wanasema WAJINGA NDO WALIWAO Jamani tunahitaji elimu ya urai

  ReplyDelete
 4. Asanteni. Kamala, dalili za watu kuamka Bongo zipo sana. Ugumu wa maisha unawalazimisha watu kuamka na kuanza kuhoji mambo yanavyokwenda. Siku wakiweza kutambua kwamba kilo za sukari na chumvi pamoja na pea za kanga na vitenge wanazopewa wakati wa uchaguzi haziwasaidii sana, wakataka viongozi watakaowaletea maendeleo, wakahoji na kufuatilia maendeleo yao, mkondo mpya wa demokrasia utakuwa umechomoza. Naamini tumepiga hatua kubwa sana kutoka enzi zile za "zidumu fikra sahihi za mwenyekiti" mpaka wakati huu. Mambo yanabadilika.

  Anony. - mambo yanaumiza eeh. Lakini hata hiyo elimu ya uraia nani ataandaa mitaala. Unataka tuanze tena kukaririshana ahadi za MwanaTANU, miiko ya viongozi, misingi ya ujamaa n.k. bila kujali utekelezaji wake? Wakati ukifika watu wataamka tu, subiri utaona.

  ReplyDelete
 5. ndio. kumbuka hata blogu zetu hizi zaweza kufanya kazi nzuri sana zikitumiwa vizuri kama chanzo cha elimu kwa ziwafikiao

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU