NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Thursday, August 27, 2009

HUYU MHUBIRI KANIFURAHISHA SANA

Hebu msikilize Mtume Onesmo N. Ndegi wa Living Water Center Makuti Kawe Dar es salaam (ni sekunde 42 tu). Mimi sina cha kuongeza.

7 comments:

 1. Mie bado natafakari swali hilo la PCCB/PCB!

  ReplyDelete
 2. inaitwa law of karma. action and re-action. lakini likipandwa moja, ytavunwa makumi na ndio maana tunzidi kuzaliwa tu

  ReplyDelete
 3. Kamala, kama kawaida yako - what are you saying here? What is law of karma? Ni kujitambua au? Mhubiri anawapa vidonge vyao mafisadi na wewe unakuja na law of Karma?

  ReplyDelete
 4. ndio. mhubiri anajaribu kuongelea asichokifahamu vizuri. nitaandika juu 'law of karma' baadaye bloguni

  ReplyDelete
 5. Kamala. Watu wote hawajui kitu cho chote except you - UNAYEJITAMBUA! Dah. Kazi ipo!

  ReplyDelete
 6. anony??????? nenda kwenye google na search karma au law of karma, utajua

  ReplyDelete
 7. Nionavyo mimi mawazo yaliyomo katika walaka wa watakatifu si mabaya, lakinu wakati (timing) na yanayojitokeza baada ya walaka yanatia shaka kama hamna ajenda ya siri.

  Kipindi chote cha utawala wa Nyerere haya hayakujutokeza. Alipokuja Mwinyi walaka zinazofanana na hizi zilijitokeza. Alianza mtakatifu Mtikila wakafuatia wengine. Alipokua Mkapa hali ilikuwa shwari. Ametokea Kikwete mambo yamebadilika baada ya kumaliza awamu yake ya mwanzo. Mengi yanasemwa juu yake na mikutano ya maaskofu juu ya utendaji wa Serikali imekuwa mingi. Vikao vya siri na vya wazi vimeongezeka zaidi hasa Bwana Silaha alipotangaza kugpmea uraisi. Hii inatutia shaka kubwa.

  Mimi kama mtanzania mpenda amani ningewaomba viongozi wetu wa dini msifanye hivyo kwa kutumia spika za dini. Acheni waumini wenu waadilfu waliyomo katika siasa watumie majukwaa ya siasa kufikisha huo ujumbe. Makanisa yana shule na vyuo vingi vya kisasa ambavyo vimetengeneza wasomi wengi wenye nafasi nyeti katika kila chama na ngazi mbali mbali za maisha. Tena wengine wamebobea katika uchumi, siasa, sayansi na kila fani. Wanajua siasa na uchumi kuliko ninyi. Waacheni waseme. Waaminini. Vinginevyo baadhi yenu mvue majoho ya dini kama bwana Slaa au Kalugendo muingie katika siasa mtumie spika za siasa.

  Nionavyo mimi kama madhehebu yote ya dini yatatumia majukwaa ya kisiasa kwa mwanvuli wa kuelimisha waumini na kuwaelekeza waumini namna ya kuchagua viongozi ni inaweza kuleta hatari. Ili limejitokeza baada ya baadhi ya wananchi kuonesha hisia kwamba Kanisa lina mpigia debe DR SLAA. Hisia kama hizo ndugu zangu japo zaweza kuwa hazina msingi hatutakiwi kuziachia ziwepo. Tuzipige vita kwa pamoja. Sisi sote ni ndugu waislamu, wakristo, wahindu, wapagani nk.

  Waumini pia tuwasikilize viongozi wetu na kuwaamini katika kazi na maelekezo yao ya kuabdu. Wanapotueleza mambo ya siasa tuwachukulie kama wanasiasa wenzetu au wapinzani wetu wa kisiasa. Tusiwaone wanajua siasa na uchumi kutuzidi. Wapo waliyosomea uchumi na siasa kama sisi lakini si wote wala hawatuzidi wote au viongozi wetu wa kisiasa wanaocheza nazo kila siku. Wala hawajui uchumi kuwazidi waliobobea kiuchumi. Tuwaheshimu na kuwafuata kwa mambo ya kiroho na tuwachukulie wa kawaida kama sisi na hata chini yetu kwa mambo ya kidini. Bwana anasema YA MUNGU MPENI MUNGU NA YA KAISARI (KIKWETE) MPENI KAISARI. Kuna biblia gani zaidi ya hii wanaisoma?

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU