NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Tuesday, August 11, 2009

KWA NINI TUSIWE NA REGINALD MENGI HALL PALE MLIMANI?

Hivi karibuni idara ya Lugha za Kiafrika na Kiasia hapa chuoni ilihamia katika jengo jipya linaloitwa Pugh Hall. Pugh mwenyewe ni milionea ambaye alisoma hapa miaka ya 60. Alisoma darasa moja na Bill Graham ambaye alikuwa gavana wa jimbo la Florida, seneta na baadaye mgombea wa uraisi kupitia chama cha Democrat.

Miaka mitatu hivi iliyopita Pugh alitoa pesa (zaidi ya dola milioni 15 ) na akaamua kujenga hilo jengo hapo chini. Ndanimwe kuna Bill Graham Center ambayo inajikita hasa katika kuwaanda vijana wanaotaka kufanya kazi za umma (public service), Idara ya Lugha za Kiafrika na Kiasia (kuwafunza Wamarekani lugha, fasihi na tamaduni zingine) pamoja na Programu ya Historia Simulizi ya Samuel Proctor (ndiyo, wenzetu wana programu za kutunza historia yao!). Ni jengo la kisasa kabisa lenye kila kifaa cha kisasa cha kiteknolojia.

Kwa vile tunaiga, mbona na sisi tusiige tabia ya hawa mamilionea? Ati, mbona tusiwe na Reginald Mengi Hall pale Mlimani? Kuna ubaya gani tukiwa na Rostam Aziz Hall? Edward Lowassa Hall? Andrew Chenge Hall? ...Hii itapunguza shida ya malazi kwa wasomi katika vyuo vyetu. Natumaini serikali haitashindwa kuunga mkono juhudi kama hizi kwa kuchangia pesa zaidi kukamilisha majengo haya yatakayojengwa na mamilionea wetu watakaoamua kuliachia urithi wa kudumu taifa lao lililowatajirisha!

3 comments:

 1. Mmh, that should be interesting kwa hao "millionaires" wa kwetu kufanya hivyo, I wonder if it may work...

  ReplyDelete
 2. Well!! Nakubaliana nawe kuwa tunaiga, na nakubali kuwa tunaiga ili kuwekeza lakini swali ni kama tunaiga ili kuwekeza kwa wenzetu ama kwetu. Kama ingekuwa ukijenga jengo hilo hulipi kodi kwa miaka 5 haijalishi unaingiza nini, ungeona wangapi wangejitolea. Sisi tunaiga "maendeleo" yanayoigizwa na kutufanya kuwa mbali na uhalisia wa maisha. Kuna visingizio viiingi kuhusu hili wakisema UTANDAWAZI na mengine. Na ndio maana tunaiga hata na haya hapa (http://mrokim.blogspot.com/2009/08/miss-totoz-2009.html#comments) ambayo tunaweza kusingizia kuwa tunavumbua vipaji.
  Lakini yaliyo ya maana kuiga tunaweka kando. Hatumuigi Rais (wa Botswana kama sikosei) aliyeamua kukata gharama kwa kusimamisha safari kwa ndege ya Rais na kupanda first class na wajumbe MUHIMU. Hatuigi nchi zinazohimiza CarPool ili kukata gharama hasa kwa waheshimiwa, tunazidi kuagiza MI-GAS GUZZLER. Hauiigi Marekani ilipo-freeze mishahara ya watumishi wa ikulu na serikali kuu, tunawaongezea marupurupu kwa kusinzia Bungeni.
  Aliyewaloga viongozi wetu alishakufa na waliohudhuria mazishi wote wamepoteza kumbukumbu lilipo kaburi. Hatuwezi hata kutambika sasa kuondoa MIKOSI tunayoiita viongozi.

  ReplyDelete
 3. Candy1 - kwa nini isi-work? Mimi sioni sababu ya kuto-work. Mzee wa Changamoto - kama kawaida yako - ni maneno ya kufikirisha na yenye kugusa hisia. Uchungu wako nausikia katika sentensi hii:

  "Aliyewaloga viongozi wetu alishakufa na waliohudhuria mazishi wote wamepoteza kumbukumbu lilipo kaburi" Mwenye masikio na asikie!

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU