NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Thursday, August 13, 2009

MASHINDANO YA UREMBO YAZIDI KUPAMBA MOTO TANZANIA - SASA KUNA MISS TOTOZ!

Haya unaambiwa ni mashindano ya Miss Totoz Temeke (2009). Ina maana kuna Miss Totoz Ilala, Kinondoni, na wilaya zingine Tanzania au yanafanyika kitaifa? Picha na post nzima nimevidokoa kutoka blogu ya Father Kidevu (samahani Father Kidevu). Ni kazi kwelikweli!

Miss Totoz 2009, Fatuma Issa

Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya, Dully Sykys, akiimba na watoto, wakati wa kutumbuiza onyesho la Miss Totoz Temeke 2009.

Miss Totoz Tmk 2009, Fatuma Issa(kati) akiwa na mshindi wa pili Jane Anthonyn na mshindi wa tatu Yunis Anthon wakati wa onyesho.

Mbunge wa Viti Maalum Al-Shymaa Kwegiar akiwa na washiriki wa Miss Totoz katika ukumbi wa Equator Grill Dar es Salam jana (10/8/2009)

Habari kamili kuhusu mashindano haya hatimaye nimezipata kutoka kwa Michuzi Jr

Fatuma Issa (7) ameibuka kidedea katika shindano la kumpata Malkia wa Watoto, Miss Totoz Temeke 2009 katika Ukumbi wa Equator Grill baada ya kuwashinda warembo wenzake 11 katika shindano lililokuwa gumu na la aina yake wakati majaji Mariam Chaheli, Jowalipokuwa wakichuja nafasi ili kumpata mrembo wa Ukweli kwa Watoto wa Wilaya ya Temeke.

Shindano hilo ambalo lengo lake ni kukuza na kuendeleza Sanaa kuanzia ngazi za chini lilikuwa na mvuto na msisimko mkubwa kutokana na watoto kuchuana vikali kila mmoja akiitaji kuibuka na ushindi na kuweka rekodi ya kwanza katika maisha yake katika shindano hilo, warembo waliobahatika kupanda jukwaani ni pamoja na Janey Anthony, Fatuma Issa, Zaituni Hassan, Neema Ally, Ester Frenk, Ashura Omary,Mariam Karama,Nasra Ally, Yunis Anthony, Angela Silayu,Happy Peter, na Eda Damian.

Aidha warembo waliobahatika kuingia katika hatua ya tano bora ni pamoja na Fatuma Issa, Jane Anthony, Yunis Anthony, Mariam Karim, na Ashura Omary,ambapo nafasi ya pili ilichukuliwa na Jane Anthony, na nafasi ya tatu ilichukuliwa na Yunis Anthony, Mgeni Rasmi katika Onyesho hilo la Miss Totoz alikuwa ni Mh. Mbunge wa kuteuliwa viti Maalum, Al-Shymaa Kwegiar, ambaye aliwapongeza waandaaji wa shindano hilo kampuni ya Jacqueline Intertaiment kuwa yana nia njema ya kuwapata washiriki wa masuala ya Urembo kwa miaka ijayo.

"shindano hili kusema kweli ni la kipekee, ukiwatazama watoto unagundua kuwa pia wanaitaji kupatiwa mafunzo haya ikiwa mapema ili ifikapo wakati wa mshiriki anakuwa apati tabu na pia anakuwa ana tena aibu kama tunavyowashuhudia baadhi ya washiriki wanashindwa hata kujielezea, kujibu swali hata kama siyo gumu, ukweli wengi wao wanakuwa na aibu, hivyo watoto wakianza kufunzwa angali wadogo bila shaka siku zijazo tutakuwa na washiriki wengi wa Urembo"alisema Al-Shymaa

Naye mratibu wa mashindano hayo kwa watoto Jacqueline Magayane alisema kuwa baada ya kupata watoto warembo wa Temeke sasa ni zamu ya ilala na kisha Kinondoni ambako warembo wa Miss Totoz watano kila Mkoa wa Kipolis watashindana kupata mshindi mmoja wa jiji la Dar es Salaam mapema mwaka huu, "kwa kweli ndiyo kwanza tunaanza kuweka changamoto kwa watoto wetu, kwani tunao warembo wengi sana watoto ambao wakipatiwa maelekezo wakiwa na umri mdogo watakuwa katika mazingira ya kutambua vipaji vyao na hivyo kuzidi kuviendeleza, kwa hiyo hadi sasa nimepata warembo wa Temeke watano na sasa watapatikana wengine wa wilaya zote na kisha watashindana ili kupata wa Jiji letu.

kikubwa ninawaomba watu mbalimbali kujitokeza kusaidia kufanikisha shindano hili ambalo ni changamoto kwa watoto wetu, ili pia waweze kujitambua umuhimu wao juu ya masuala ya Urembo wakiwa bado wadogo kama ilivyom katika masuala mengine kama mpira wa miguu, na kikapu watoto wanaanza kuelimishwa wakiwa wadogo na hivyo kukua wakijua namna ya kuvitumia Vipaji vyao"alisema Jack

Mshindi wa kwanza katika shindano hilo alizawadiwa TV na Cheni, wa pili na wa tatu Radio na Cheni wa nne na tano walipatiwa cheni kila mmoja, sambamba na washiriki wote kupatiwa vifaa vya shule ikiwamo vitabu, peni, na madaftari ambavyo vyote vilikabidhiwa na mgeni Rasmi Mh. Mbunge Viti Maalum, Al-Shymaa Kwegiar.

8 comments:

 1. Dah! Kazi ipo tena kubwa saaaaana!!!

  ReplyDelete
 2. Suala la mashindano ya urembo ni kama kasumba ambayo imetukaa vilivyo watanzania kwa sasa. Si viongozi wa ngazi za juu serikali wala si watoto wanaoanza kutembea nao huwa wapozi mbele ya wenzao na kutembea ki-miss. Kikubwa pia ni umasikini. Kama miss anashinda gari nyumba na zawadi nyingine kama UKIMWI MIMBA (ambazo huporomoshwa bila huruma)na magonjwa mengine ya zinaa. Lakini hii yote hutokana na uvivu wetu wa kufikiri na kuwa wa bunifu. Tunapenda vya mkato vingi.

  ReplyDelete
 3. watoto hawa wanaelewa nini kuhusu urembo naomba hao waandaaji washindwe na walegee,wawaache watoto wawe watoto!

  ReplyDelete
 4. Halafu zawadi zenyewe za kichovu kweli. Eti cheni. Umasikini kweli mbaya jamani. Mtu unapeleka kitoto chako kimalaika ambacho hakijui lolote eti upate cheni. Umasikini utatumaliza haki ya mama.

  ReplyDelete
 5. Hivi hawa wabunge wa viti maalum wana kazi gani hawa? Huyu naona hana kazi kabisa na nitashangaa kama ametumia shangingi la serikali kwenda kwenye shughuli ya KIPUMBAVU kama hii ya kudhalilisha watoto wasiojua cho chote. It is very sad! Yaani this country inakwenda kama mlevi tu, hakuna maelekezo, hakuna mwongozo hakuna cho chote. Kila mtu ni kuiba na kukimbia. Nchi inaangamia hii wallahi. Nyerere tunakuomba ufufuke, please please..

  ReplyDelete
 6. This comment has been removed by the author.

  ReplyDelete
 7. Mwalimu Leo vipi tena? Mbona umetoa maoni yako? Tuko pamoja.

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU