NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Tuesday, August 18, 2009

MNAIONA "PARADOKSI" KATIKA PICHA HII?

Nafikiri lengo la mtengenezaji wa picha hii inayokera (ambaye naamini ni mzungu au Mwafrika anayetafuta misaada kwa wazungu) ni kuonyesha, mbali na mambo mengine, kwamba wakati sehemu nyingine duniani wanapambana na unene, Afrika pamoja na utajiri wake wote, yenyewe bado watu wake wengi wana utapiamlo na wengine wanakufa kwa njaa.

Kama utafiti niliourejerea Ijumaa ya wiki jana ulivyoonyesha, sababu kubwa iliyotajwa kuwa chanzo cha unene ukiwemo ule wa futufutu (obesity) nchini Marekani ni umasikini. Swali la ki-paradoksi ni kwamba, inakuwaje sababu ile ile moja (umasikini) isababishe utapiamlo na kufa kwa njaa Afrika (ambayo ni tajiri sana) na unene (wa futufutu) Marekani na Ulaya?

4 comments:

 1. Inasikitisha kiasi kwamba la kusema linapotea.Ni hayo tu.

  ReplyDelete
 2. Kwakweli ni balaa. Umasikini tulionao Afrika si wa rasilimali isipokuwa ni umasikini wa jinsi ya kuzitumia rasilimali tulizonazo bilashaka na mabo mengine yanachangia kama wizi,ufisadi,ubinafsi n.k n.k.
  Katika nchi zetu tunao watu wenye uwezo wa kutanda lami nchi nzima, wapo pia wakujenga maghala ya kuhifadhia mazao lakini wapo pia wakujenga viwanda vya kusindika vyakula na mabombo mengi tu. Masuala ya utapiamlo na madhila mengine yanayotupata kamwe yasingetokea iwapo tungekuwa na uzalendona kujua vipaumbele. Tulio wengi tunatabia za KIHINDI, mhindi anakaa msajili wa majumba ana uwezo wa kujenga nyumba lakini hafanyi hivyo pesa anazopata anaweka benki za nje, pia wapo watanzania wengi tu wenye vijisenti vyao wanaweka benki za nje ambapo mke wake au hata ndugu yake yeyote hajui siku akiitwa mbele ya haki na pesa yote inapotea.
  Kwaweli kubadilisha hali inayotukabili Africa ni kazi sana. Tuanahitaji kupata elimu ya kutuwezesha kuzikataa vita na kuziogopa maana huyo muungwana aliyekondeana bila shaka anaweza kuwa ni wa Sudan, Ethiopia, Somalia lakini Tanzania si dhani kama tumefikia hali ya kutisha kama hiyo japo tunayo ya kwetu ya kutisha kwelikweli

  ReplyDelete
 3. ndio, wakati mwingine ni bora kutokula kuliko kula.

  wengi tunajaza matumbo na chakula hakina tija ndio maana tunanenepa.

  nafikiri hata nje ya afrika kuna njaa huku tukiwa tumejisalimisha mikononi mwa wazungu ili watugombanishe watakavyo wao. hapo ndipo tatizo

  ReplyDelete
 4. jamaa hajakosea ngoja atueleze ukweli shinyanga arusha kuna ukame wa kujitakia na hata sasa wanapelekewa chakula cha msaad kisa watu wanafuga ufugaji usiozingatia kanuni familia moja n"gömbe 4000 za nini zote hizo wakati hata nyumba hawana wanaharibu tu ardhi ya wajukuu zetu HABARI ndio hiyo hiyo katuni ukweli mtupu.

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU