NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Thursday, August 27, 2009

ATI, TANZANIA IMEANZA KUTUMBUKIA KATIKA UDINI?

Nimeiona hii katuni ya Musa Ngarango kutoka katika blogu ya Mjengwa na ikanikumbusha mambo kadhaa. Mwalimu Nyerere alijitahidi sana kupambana na udini pamoja na ukabila kwani aliamini kwamba kama vitu hivi viwili vingeachiwa vingeweza kuhatarisha mustakabali na umoja wa taifa. Na kwa kiasi kikubwa alifanikiwa (Msikilize hapa kuanzia dakika ya 9:06).

Kutokana na ule waraka wa maaskofu wa kanisa katoliki, waislamu nao inasemekana wametoa waraka wao (soma hapa). Hali hii inawafanya watu wengi waanze kujiuliza kama Tanzania imeanza kutumbukia katika tatizo la udini - jambo ambalo linaweza kuwa la hatari kama tulivyoshuhudia katika sehemu mbalimbali duniani. Ni lazima tuwe waangalifu sana na jambo hili ili tusije tukajuta baadaye. Cha kushangaza ni kwamba serikali imekaa kimya na inavyoonekana ni kama vile imemwachia Komredi Kingunge Ngombare Mwiru ashughulike na suala hili. Ngoja tuone atasema nini kuhusu huu waraka wa Waislamu!

2 comments:

  1. Siujui hiyo imekaaje, kwasababu likitokea tatizo wanaombwa watu wa dini wasaidie, wakisaidia itaitwaje? hawajachanganya dini na siasa?
    Katika maisha yetu dini ipo na inatuongoza, kwahiyo pale matatizo yanapokuwepo,dini zinaingia kutoa maoni, ili kupambana na matatizo hayo, labda kwa vile wametoahoja kabla hawajaambiwa wasaidie, na labda kwavile wengine watatoa na wao nyaraka zao,kitu ambacho hakitakiwi. Kwa vyovyote iwavyo, dini hazitakaa kimya matatizo yakikithiri, ila hapo najiuliza ni jinsi gani dini zifanye ili zisichanganye dini na siasa

    ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU