NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Friday, August 28, 2009

UTAFITI: KUTAHIRIWA HAKUWASAIDII MASHOGA KUTOAMBUKIZWA VIRUSI VYA UKIMWI

Ingawa tohara ya wanaume imethibitishwa kuwa njia mojawapo muhimu katika kupambana na maambukizi ya gonjwa la UKIMWI miongoni mwa wanaume wanaofanya mapenzi ya kawaida na wanawake, utafiti uliofanywa na Kituo cha Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa (Center for Disease Control and Prevention - CDC) cha Marekani umeonyesha kwamba tohara haisaidii cho chote katika kuzuia maambukizi ya UKIMWI kwa wanaume wanaofanya mapenzi na wanaume wenzao yaani mashoga. Mbali na mambo mengine, utafiti umeonyesha kwamba:
 • Maambukizi ya UKIMWI kwa wanaume wa Kimarekani wanaofanya mapenzi ya kawaida na wanawake yamebakia kuwa ya kiwango cha chini (pengine) kutokana na ukweli kwamba karibu asilimia 80 ya wanaume wote hapa Marekani tayari wameshatahiriwa. Pamoja na asilimia hii kubwa ya tohara CDC imesema kwamba itaendelea kuwahimiza wazazi kuwatahiri watoto wao wa kiume wanapozaliwa.
 • Zaidi ya nusu ya maambukizi mapya ya UKIMWI kila mwaka hapa Marekani yanatokea miongoni mwa mashoga ingawa mashoga ni asilimia 4 tu ya wanaume wote.
Utafiti huo ulihusisha wanaume 4,900 waliokuwa wakifanya mapenzi na wapenzi wao mashoga ambao tayari walikuwa wameshaambukizwa virusi vya UKIMWI. Matokeo yake yalionyesha kwamba hakukuwa na tofauti yo yote katika maambukizi. Mashoga waliotahiriwa na wale ambao hawakutahiriwa waliambukizwa virusi vya UKIMWI kwa kiwango kile kile kinachofanana.

Kutokana na utafiti huu serikali ya Marekani ikishirikiana na Shirika la Afya Duniani (WHO) imesema kwamba itaendelea kuhimiza tohara kwa wanaume wa marika yote katika nchi za Kiafrika kama njia muhimu ya kupambana na maambukizi ya gonjwa hatari la UKIMWI. Kwa habari zaidi kuhusu utafiti huu soma hapa.

5 comments:

 1. Mimi sipendi mashoga. Hata wote wafe na UKIMWI kwangu ni sawa tu.

  ReplyDelete
 2. Mama Kevin (Ubungo)August 28, 2009 at 6:23 PM

  Hii ni hatari. Kuna huu mtindo hapa Bongo unaoitwa TIGO. Vijana hawaridhiki siku hizi bila kupewa au kutoa tigo ambayo kifupi ni sodom. Kama unampenda sana boyfrendi even your husband eti ni lazima akuingilie kinyume yaani TIGO. Ndiyo maana UKIMWI unazidi kupamba moto. Thanks for this post. This is important information ingawa sijui kama inawafikia hasa walengwa who are busy reading udaku kwenye magazeti ya Global Publishers. Mungu atusaidie jamani.

  By the way mimi sichukii mashoga kama huyo anony. hapo juu. They are human beings like us who have chosen a different way of life. Na kwa nyinyi wanaume mnaotaka kupewa tigo, mna TOFAUTI GANI NA MASHOGA???

  ReplyDelete
 3. Yes, this is important. These girls must know that wanapokubali kufanywa kinyume cha maumbile eti tigo fashion wajue kwamba kama huyo jamaa ana UKIMWI basi wataupata. This generation real never ceases to amaze me!

  ReplyDelete
 4. Yeah ni hiyo njia ya kinyume na maumbile ndio inawaponza (If I can say that), na kuna njia nyingine pia wanafanya ila I can't say it maana mmh...mambo makubwa...anyway it seems like they should take more caution.

  Na kila mtu na opinion yake ikija kwenye issues kama hizi coz gays ni humans pia, just different when it comes to "pleasure" and whatever they think of...

  ReplyDelete
 5. Mama Kevin (Ubungo)August 29, 2009 at 2:36 AM

  Candy1, tuambie unaogopa nini? Binti mzima bado unaogopa kudiscuss mambo openly. Hukuchezwa nini? Mimi nitakung'ang'aniza mpaka useme!

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU