NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Friday, August 7, 2009

UTAFITI: WANAUME HUTUMIA MWAKA MZIMA WA MAISHA YAO WAKIKODOLEA MACHO WANAWAKE

Nimesoma juu ya utafiti huu ukanichekesha. Watafiti sasa wanasema kwamba kwa wastani mwanamme hutumia dakika 43 kila siku akibung'alia wanawake tofauti tofauti wanaokaribia 10. Hii ni sawa na kutumia mwaka mzima wa maisha yake (tukihesabu kuanzia miaka 18 mpaka miaka 50) akitazama wanawake. Sehemu kubwa ambazo watu hupenda kufanyia shughuli hii ni katika maduka makubwa, katika baa, nightclubs na pengine tunaweza kuongeza barabarani (inasemekana baadhi ya ajali hutokea kwa sababu madereva wa kiume hawaangalii wanakokwenda bali wamekaza macho kwingineko kuangalia wanawake wanaotembea barabarani).

Wanawake nao pia wamo. Kwa wastani wao hutumia dakika 20 kuwacheki wanaume tofauti wanaofikia 6 kila siku. Hii ni sawa na miezi sita ya maisha yao ya kati ya miaka 18 na 50.

Umbo la mwanamke ndiyo sababu kubwa inayowafanya wanaume kumkodolea macho mwanamke wakati macho ya mwanamme ndiyo huwavutia zaidi wanawake. Tukumbuke hata hivyo kwamba utafiti huu ulifanywa kwa wazungu na ukifanywa kwetu pengine utaibua sababu na takwimu tofauti. Kwa habari zaidi soma hapa.

Kuna anayebisha kuhusu jambo hili la kutazamana?

4 comments:

 1. Kweli Mkuu hapa umeleta mawazo yakinifu kabisa. Mie nafikiri ni kweli kabisa.Sasa kuna linalotakiwa kufanyika hapa maana kama vile ni muda mwingi unapotea na tunakumbushwa "Time is money", ndio kusema basi tunapoteza hela vilevile.

  ReplyDelete
 2. Sidhani kama kuwaangalia kwa mwaka kunaweza kuathiri maisha ya mtu. Ila fikra zinazokaa akilini ndio shida. Yaani kama unatumia mwaka kumuangalia na "taswira" inaji-loop akilini kwa miaka 10. basi ukizidisha mara wale unaokutana nao.....
  Hapa kuna haja ya ku-invest kwenye dawa ya matamanio kwa kinababa. Lol
  Asante kwa somo zuri Kaka

  ReplyDelete
 3. Nicky - mimi huwa sikubaliani na hii ishu ya eti time is money kwani ni dhana ambayo huwa siielewi vizuri. Unapougawa muda na kuuthamanisha na pesa, suala zima la kuishi linapoteza maana na kama kweli utataka kuitekeleza dhana hii basi utaishia kukimbiakimbia tu na pengine hutalala kwani utapoteza pesa. Napenda dhana ya muda ya Kiafrika.

  Mzee wa Changamoto - umenikumbusha jibu la mhubiri mmoja alipoulizwa katika kipindi cha vijana jambo la kufanya vijana wakiona mwanamke mzuri na "automatically" wakamtamani katika fikra zao. Mchungaji aliwahakikishia vijana kwamba kumwangalia mwanamke "mzuri" na hata kuvutiwa naye si dhambi, dhambi inaanza pale unapoanza kupanga mikakati akilini mwako jambo la kufanya. Alisema "huwezi kumzuia ndege kuruka juu ya kichwa chako lakini unaweza kumzuia asitue kichwani" Sijui kama mchungaji huyu alikuwa sahihi ama la!

  ReplyDelete
 4. Masangu, aksante kwa mada. Wataalamu wanasema kuwa mutu moja napata mawazo 50,000 kwa siku (masaa 24). Hayo ni pamoja na mabaya na mazuri. Nakubaliana na Rev wako kwani kati ya mawazo hayo 50,000 unaweza tu ukachagua unayoweza kuyaweka akilini kwani uamuzi ni wako. Ukiamua kuweka mawazo mabaya a.k.a. machafu ama matakavitu yatakuchafua siku nzima. Na madhara yake yanaeleweka kama msongo, magonjwa yasoelewekaeleweka, shinikizo la damu nk.

  Ukiweka mazuri a.k.a matakatifu siku yako itakuwa swaafi.

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU