NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Friday, August 14, 2009

UTAFITI: WATU WEUSI NDIYO WANAONGOZA KWA UNENE

Utafiti uliofanywa na Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (Centers for Disease Control and Prevention) vya Marekani unaonyesha kwamba watu weusi ndiyo wanaongoza kwa unene wa futufutu (obesity) hapa Marekani. Utafiti huo umeonyesha kwamba karibia asilimia 36 ya watu weusi ni wanene futufutu ikilinganishwa na asilimia 24 tu kwa wazungu. Hii ni hatari kwa sababu unene huu wa futufutu ndiyo kisababishi kikubwa cha magonjwa kama kisukari (diabetes), magonjwa ya moyo, kiharusi, shinikizo la damu na baadhi ya saratani. Hii pengine inaweza kueleza ni kwa nini watu weusi ndiyo wanaongoza kwa kufa mapema hapa Marekani.

Sababu kubwa iliyotajwa katika utafiti huu ni umasikini. Watu weusi ndiyo masikini zaidi na kwa hivyo hawana pesa za kujinunulia vyakula vizuri visivyonenepesha (kama mbogamboga), bima za afya na pesa za kujiunga na vilabu vya kufanyia mazoezi (gyms).

Sababu zingine ni za kitamaduni. Imetajwa kwa mfano kwamba katika utamaduni wa watu weusi unene (ukiwemo huu wa futufutu) hauonwi kama ni tatizo na kwa hivyo watu hawaoni sababu za kujibidisha kupunguza uzito wao. Mambo ya kuitana Big Dady (jibaba), Big Mama (jimama) na hata tabia ya watu weusi kupenda wanawake wanene ni sababu za kitamaduni zinazochangia ufutufutu kwa watu weusi.

Wanawake weusi ndiyo wanaongoza zaidi katika unene huu wa futufutu wakifuatiwa na wanaume na halafu watoto. Jimbo la Maine ndilo linaongoza kwa kuwa na watu weusi futufutu wengi zaidi (asilimia 45). Kwa habari zaidi soma hapa.

Niliposoma utafiti huu nilifikiri mambo mawili. Kwanza, kwa nini unene huku ni dalili ya umasikini wakati sisi kule nyumbani ni (ilikuwa) dalili ya utajiri? Pili, kwa nini watu weusi ndiyo wanaongoza kwa umasikini hapa Marekani? Nani alaumiwe kwa tatizo hili?

40 comments:

 1. mh, aisee mbona huwa nawaona hata wazungu wanene? hata vitiambi hapa bongo vinatisha. huwa napenda kusimama na kuwaangalia watu wanene na kucheka, inafurahisha japo haiamini ni kwa vipi mtu ananenepa vile.

  ReplyDelete
 2. Sikubalini hata kidogo kwani nimeona wazungu ambao wamenenepa mpaka huruma. Ila basi tu!!

  ReplyDelete
 3. Watu weusi wamelaaniwa. Popote pale utakakowapeleka iwe ni Afrika, Ulaya, US, Jamaika, Haiti all ni the same. Incompetence, laziness, dirty and poverty. Halafu tukiambiwa kwamba we are a cursed race tunalalamika. I wish I were not black becauese it is a shame. Nikipata mzungu wa kunioa au siku nikienda nje, I will never come back to Africa again.

  ReplyDelete
 4. NAOMBA NITOE MAONI KUHUSU MAONI BADALA YA UTAFITI.
  Ndg yangu Aika umeandika (na hapa nanukuu) "I wish I were not black becauese it is a shame." Labda si wewe pekee unayetamani kuwa ungezaliwa na rangi nyingine, lakini kama hao uwatamanio wangekimbia matatizo ya rangi zao badala ya kuyapenda, basi leo usingetamani kuwa kama wao. Labda unge-wish kuzaliwa colorless. Lakini yaonekana unajua kinachokufanya usitamani weusi na umetaja hapo juu (nami nanukuu) "Incompetence, laziness, dirty and poverty." ambavyo kwa bahati nzuri si ulemavu na vyote vyaweza kubadilishwa na watu wanaotambua na kuanza kuvishughulikia. Hakuna haja ya kuukimbia uafrika kwa kuwa wazungu "wana maendeleo". Haya na matatizo ya UTUMWA WA KIAKILI ambao tumeshuhudia ukiwaumiza wengi na hata viongozi. Inasikitisha kuona mtu kama Kikwete anakubali kuwa Tanzania ni maskini wakati tuna rasilimali nyingi kuliko nchi zilizoendelea. Bila aibu wanasema SISI NI MASKINI. HUO NI UMASKINI WA FIKRA kukubali mtu asiyekutakia mema aku-define wewe ni nani. Yaani tunaaminishwa kuwa upungufu wa pesa ni umaskini hata kama tuna madini, amani, upendo, utulivu, ushirikiano ama chochote wasichonacho. Ni akili za namna hii nilizoziandika hapa (http://changamotoyetu.blogspot.com/2009/04/labda-sisi-si-maskini.html) na naamini kwa kusoma hapo itasaidia.
  Lakini pia, kwa kusoma sentensi ya mwisho (nainukuu) "Nikipata mzungu wa kunioa au siku nikienda nje, I will never come back to Africa again" naweza kutoa sehemu ya lawama kwako kwani najua KAMA HUJATOKA NJE YA NCHI AMA HUJAWEZA KUJITAMBUA NA KUITAMBUA BARAKA ILIYO NDANI MWAKO, utaendelea kuwatukuza wanaokutawala na kuendelea kuwafanya wakutafsiri wewe katika namna utakayoendelea kujidharau na kujiona hufai na kuikimbia asili yako.
  Waliokwenda nje na wanaoitafuta kweli ya maisha ya nje wanajua tofauti ya IMANI ya "nchi za nje" ilivyo na uhalisia wa maisha. Nami sina la zaidi juu ya hili. Ntasema kama alivyosema Lucky Dube kuwa "i lived his world and i've seen the other world, i've got nothing to say. I put my coat on my shoulder as i walk away i heard myself sing, the grass is greener on the other side, till you get there, you see for yourself". Labda nikukumbushe kuwa Hata Bob Marley alisema "YOU CAN'T RUN AWAY FROM YOURSELF". Kuukimbia Uafrika wako ni sawa na kukikimbia kivuli chako. Hutakiona kama kutakuwa na giza, lakini mwanga ukichomoza utakiona tuu. Just RISE UP, WISE UP, WAKE UP and SHAKE UP. Kumbuka usia kwetu kuwa "Emancipate yourselves from mental slavery, none but ourselves can free our minds"
  Unaweza kusoma zaidi kuhusu hili la kupenda kuwa usivyojua utakuwa kwa kuangalia mandiko yangu ya wimbo wa THE OTHER SIDE hapa (http://changamotoyetu.blogspot.com/2009/01/them-i-them-lucky-dubethe-other-side.html)

  Blessings

  ReplyDelete
 5. We unayejiita mzee wa Changamoto. Quotations za wavuta bangi wa reggae hazitasaidia kitu lakini ukweli unabakia palepale. Inakuwaje kila mahali ukiweka tu mweusi mambo yanaharibika. Hebu tazama EVERYWHERE. What is wrong with us? Hata kule Marekani - mbali na haya mambo ya unene, nimeambiwa pia kwamba watu weusi kule ni wavivu, wanapenda kulalamika sana wakitaka serikali iwasupport kwa kila kitu, wachafu, hawapendi kujiendeleza n.k, n.k, n.k. Si unaona kile kimbunga kilichopita kule New Orleans. Yaani jama walikuwa exposed kabisa.

  Sihitaji kujitambua kwani ninajitambua sana. Naamini kwamba hata wewe deep in your heart unajua kwamba something is terribly wrong with black people whether in Africa, Guyana, America, Carribean au popote pale. Tena usiwategemee sana hawa watu wa reggae. Most of them were losers, hippies, weed smokers who were far detached from reality. Ukivuta bangi hata hujui unachoimba and I think this is what was going on with them. Unamquote Bob Marley - mtu ambaye alikuwa anavuta I kilogram of weed per day. Are you kidding me? Please brother RISE UP, WISE UP, WAKE UP and SHAKE UP!

  ReplyDelete
 6. Yawezekana kuna ukweli katika usemayo ANON lakini haimaanishi kuwa hakuna ukweli usiousikia. Sidhani kama nitabishana na ambaye amekiri kuwa HAJATOKA NJE YA AFRIKA na AKIOLEWA NA MZUNGU NA KUTOKA NJE YA AFRIKA HATAREJEA. Kwa hiyo ntafanya iliyo njema kwa KUKUACHA UWE MSHINDI FOR THE SAKE OF PEACE.
  Nakuombea umpate wa kukuoa ambaye atakutoa huko uliko na akupeleke huko utakako. Na tuombe kuwa ufanikishe nia yako lakini najua utaona mtazamo wako utakavyokuwa ukishaijua kweli yao.
  Weed??? Sitaki kuongelea hilo kwani ni wachache wameweza kutetea haya usemayo kuihusu.
  Sooooo!!!! Umeshinda na "nimeshindwa"
  Blessings

  ReplyDelete
 7. very interesting na labda weusi tuna kasoro!!!! siamini hivyo. binadamu amekukwa akitafuta furaha kupitia maendeleo na sasa kila kinachofanyika kuleta maendeleo kinageuka kuwa laana. si wazungu wameendelea? sasa angalia matokeo ya maendeleo hayo! upuuzi mtupu! angalia mabadiriko ya hali ya hewa, Vita, ubinafsi uchoyo nk.\

  wakati mwingine ni bora tukabakia kuwa kama waafrika tu. kwani maendeleo nini ni na tunahitaji nini sisi kama binadamu? kumiliki mali nyingi? au?

  the main qustion should be why, what and who. not races.. common, nimeandika sana juu ya umoja wetu kama bindamu bila kujali rangi. Aika, unaamini umejitambua japo huuishi huo utambuzi wako. nenda kwanza ulaya ukaolewe na muzngu ili uwe naakili""""

  kutajirika kama wazungu sijui kwani hatuji na kitu wala hatuondoki na kitu. maisha yetu ni marefu kabla na baada ya kuiacha miili yenye rangi kuliko kuitukuza.

  sijui niseme nini ila kama unadhani weusi wako ni ishu, basi tumia mkorogo ubadili ngozi, tia dawa kichwani zitabadilika, nk, nk

  ReplyDelete
 8. Aika, Aika ,Aika wanishangaza kweli. Mimi ni mwanamke na nimebahatika kuolewa na E VERY HANDSOME BLACK MAN-VERY TANZANIAN na kamwe sikuwahi kutamani kuolewa na mzungu awe fukara au tajiri ili muradi tu mzungu? Unatia aibu lakini sishangai sana kwakuwa unatoka mkoa wa Kilimanjaro hiyo ndo kasumba yenu. Wewe kama mwanamke kabla ya kusubiri mwanaume kwa vyovyote atakavyokuwa hata kama ni wa kutoka ahera ama toharani achilia mbali ni mzungu una mpango gani na maisha yako? Unasubiri ukombozi toka kwa mwanaume wa kizungu? Usitutie aibu wanawake wenzako. Wazazi wako wamekupeleka shule ili uelimike. Kumbuka mwanamume si ajira. Ndo nyie mnaokesha kwa masongo na kuua maalbino ile mpate bahati ya kuolewa na wazungu. Angalia kipindi cha THE BIGGEST LOOSER (channel E) na ujichagulie kutoka pale mchumba kwani wengi kutokana na maunene yao wamekosa hata wazungu wenzao wa kuwaoa kwakuwa unajinadi JUST SERVE YOURSELF

  ReplyDelete
 9. Aika hata kama ningekuwa mwanamume wa kizungu nisingeoa mwanamke mpumbavu kama wewe. Una kasoro kubwa sana katika ufahamu wako. Mzungu akiamua kuoa wamamke mwafrika ni kwamba kampenda kama alivyo siyo eti kwakuwa ameukana uafrika wake. Jiatambue kwamza kama mwanamke kisha kama mwafrika. Duania ya leo si ya kusubiri mwanaume. Ndo nyie mgeuzao waume zenu waliowaoa kwa mapenzi kuwa ATM. Mpaka leo unasubiri mzungu uli utoke nje ya Tanzania (Africa?)Wewe si mvivu kama waafrika wengine siyo wasuibiri nini wenzako ulaya kama kariakoo.
  Kila la heri kwa kusubiria ndoto yako itimilike (Kuolewa na mzungu)unatutia aibu wanawake wenzako.

  ReplyDelete
 10. Hi Mzee wa Changamoto. Asante kwa kuRISE UP, WISE UP, WAKE UP and SHAKE UP na kunielewa. Achana kabisa na hao wavuta bangi wa raggae. Hopeless! Nitakuwa naangalia blogu yako often.

  Kwa anony uliyeolewa na E VERY HANDSOME BLACK MAN-VERY TANZANIAN hujui kwamba ana nyumba ndogo huyo? Ni lini ulipima UKIMWI wewe? Pengine tayari keshakuambukiza huyo halafu bila aibu unatupayukia hapa eti E VERY HANDSOME BLACK MAN-VERY TANZANIAN. E VERY HANDSOME BLACK MAN-VERY TANZANIAN my foot! Mianaume myeusi hii kama kawaida ndiyo inaongoza kwa kutongoza nje, magonjwa, uzembe na mengineyo. MBONA LAKINI HAMTAKI KUAMBIWA UKWELI NYIE??? As for me using mkorogo kuwa mweupe sina haja. Hayo nawaachia akina Maimartha Jess wasiojiamini. Kujitambua na msimamo ni bora zaidi kuliko kujikwangua nje.

  Mi sisubiri ukombozi wa mwanaume wa kizungu. For your info, nina kazi nzuri na pesa zangu mwenyewe and I am beautiful lakini kamwe nshaapa mwanaume mweusi haniguzi KAMWE. For what? Lazy womanizing HIV+ bastards!!!

  We anony wa August 17, 2009 1:23 PM. Kwako wewe sina hata haja ya kukujibu. Ni wanawake kama wewe ambao bado mnakubali kuonewa na kufanywa vikaragosi na hao VERY HANDSOME BLACK MAN-VERY TANZANIAN. Hopeless and pathetic! Na nyote mnaopiga makelele hapa please tell me precisely, ni KWA NINI KILA MAHALI UKIWEKA MTU MWEUSI MAMBO YANAHARIBIKA??? WHAT IS WRONG WITH YOU PEOPLE? I am sure hata mbinguni mambo yatakuwa ni yale yale for blacks...

  ReplyDelete
 11. Hey baby sikujua kama na wewe ni "mweusi" kumbe mwenzetu wewe ni mzungu wa kweli yaani ubongo wako ni mweupe. Kwani unafikiri wazungu hawana nyumba ndogo? Kwani wao pia hawaugui UKIMWI? Kwakuwa u mweusi pia hata wewe mambo yako yameharika? Uzuri ulionao ni wa nje ama wa ndani? Sidhani kama kuna mzungu atakupenda eti kwakuwa unajidharau a black man/woman is always a black man/woman huoni kwamba utamuharibia mambo huyo mzungu mumeo mtarajiwa kwakuwa wewe tayari ni mweusi(hata kama ni mweupe wa asili au kwa mkorogo)So you ENVY Maimatha wa Jesse. Mwanaume ni mwanaume tu awe mzungu au black akiamua kukufanya kikaragosi hiyo ni tabia yake. unafikiri wanawake wote wawe ni wazungu au blacks waliolewa na wazungu wanafurahia ndoa zao? Nakushauri angalia TVs mbalimbali soma majarida mbalimbali na utaelewa kuhusu ulimwengu na kinachoendelea. Soma hata novels mbalimbali uone dunia inavyokwenda. Unafikiri madanguro yaliyopo kwa wazungu wateja wa hayo madanguro si waume za watu ambao wake zao ni VERY WAZUNGU? achilia mbali weusi nyie mnaokaa na kuomba kwa Mungu mjaliaaliwe kuolewa na wazangu. Miss very beautiful Aika na uzuri ulionao bado mzungu hajatambua uzuri wako na kutoa posa? Si ajabu hata likitokea zee la kizungu ambalo hata uwezo wa kwenda haja ndogo limepoteza, ukaruka nalo. We mama unatakiwa kubadilika na kuheshimu wazazi waliokuleata hapa duniani maana naamini wao pia si wazungu kwakuwa nashindwakuamini kwamba wewe ni mzungu hata kwa fikra tu. Ni kweli u mrembo weye na hausubiri mwanamume wa kizungu lakini wewe mwenyewe unayekesha na kuomba zali litokee ili uruke na A VERY KIKONGWE WA KIDHUNGU. Simpendi hata kidogo mwanamke mwenye fikra kama zako huyo mzungu atakayerealize urembo wako na kuvutiwa nawe na kukuoa namuonea huruma kwani hata watoto wako sijui kama utawapenda kwani si wazungu na kamwe hawatakuwa wazungu. USITUABISHE WANAWAKE WENZIO. Mjadala nawe sina na hata kama ni msomi na una kazi nzuri nafikiri marks zako ni za KAMANYOLA BILA JASHO. Natarajia kukusoma kwenye mijadala yenye akili na si huu upuuzi wako. USHINDWE KWA JINA LA WAUNGWANA NA ULEGEE PIA MAANA U PEPO MCHAFU

  ReplyDelete
 12. Aika, your very beautiful woman, to whom? me, Matondo, mzee wa changamoto or? how beautiful is beautiful? beautifulness yako imo akilini mwako au mwa yule akutizamaye? niliwahi waona wanawake wa Machame wakisema hivyo.

  your rich? compared to whom?

  haya
  maneno yako kamwambie yule aliyekufanya uzaliwe afrika na umwaambie kosa lake ili arekebishe kazi hiyo.

  lakini kimaumbile na sisi kama binadamu, tofauti ya mwafrika na mzungu ni ipi? weweza kulala chumba kimoja na kinyeshi cha mzungu eti kwa kuwa cha mwafrika kinanuka?

  ReplyDelete
 13. We anony mwenye VERY HANDSOME BLACK MAN-VERY TANZANIAN. Poor you yaani mpaka nakuhurumia mimi. Utapayuka wee hapa lakini ukweli uko pale pale. Ungeweka jina lako nikakujua basi ningekuonyesha jinsi huyo VERY HANDSOME BLACK MAN-VERY TANZANIAN wako alivyo malaya na pengine liko HIV+ tayari. Hopeless. Hata wewe unayejiita Kamala nimekupata and what are you talking about? Unarefer kwenye debate zilizopitwa na muda za akina Plato eti what is beauty? Rudi shule ukasome. Pfuu.

  Naona nyote mnazunguka tu bila kujibu swali la msingi lililoanzisha hii ishu MBONA KILA MAHALI UKIWEKA MTU MWEUSI MAMBO YANAHARIBIKA????????????????????????????????????

  Mkitaka maendeleo ya haraka it is very simple. Allow the white man to come back and colonize you again. Na hapo mtaona angalau wataweza kuzifanyia ukarabati reli walizowajengea ambazo mpaka leo ni zile zile na hamuwezi kuzifix. Watawakarabatia bandari na mambo mengine. MBONA KILA MAHALI UKIWEKA MTU MWEUSI MAMBO YANAHARIBIKA????????????????????????????????????

  ReplyDelete
 14. Jamani chonde chonde. Muoneeni huruma ant Aika, kwa sababu inaonekana kwamba kuna yaliyomsibu ndio maana anatoa kauli chafu kiasi hichi. She is a damaged soul. Mumuelewe hivyo, vinginevyo you can't escape FROM WHO YOU'RE. Ha,ha, ha!!! I have heard that before. Euro-centric arguements. Unaweza kumuelewa mtu through his/her arguements. AIKA your an ANGRY MADAM. My humble advice to you is: SEE YOUR FAMILY DOCTOR, ninginevyo hizo hasira zako zitakungamiza.

  ReplyDelete
 15. Aika M. Asante kwa "changamoto" Wakati mwingine ni vizuri kupata mawazo yanayokinzana kwani ni kwa kufanya hivi ndipo ustaarabu wetu na kukomaa kwetu kunajidhihirisha zaidi. Hili limejionyesha vizuri sana kwa watu waliojaribu "kukuelimisha" ingawa sina uhakika kama unayo hamu na nia ya kuelimika.

  Mimi naamini kwamba mtu mweusi hana kasoro yo yote. Pengine sababu za kihistoria na makovu ya kisaikolojia aliyoyapata kutokana na kutawaliwa na hao wazungu unaowaabudu yamemfanya asijiamini na wakati mwingine kujidharau (kama wewe mwenyewe pia unavyofanya). Vinginevyo mtu mweusi ametoa mchango mkubwa sana katika historia ya maendeleo ya binadamu katika nyanja zote (google tu utaona). Siku ukienda huko kwa wazungu pengine utashangaa kugundua kwamba nao si wakamilifu na si ajabu ukajikuta unatamani kurudi nyumbani, japo hukupendi (nyumbani ni nyumbani ati!). Jipe muda, jichunguze, jitafute na siku moja macho yako yatafumbuka na siku hiyo itakapofika, utajivunia kuwa na hiyo ngozi nyeusi.

  Na kama kweli unatafuta mwanaume mzungu, mbona wamejaa tele katika intaneti? Lakini kuwa mwangalifu usije ukapata "serial killer" au mla watu akakuoa na akishakununulia bima ya maisha ya dola milioni moja, anakuulia mbali, anapata dola zake milioni moja na kuoa mzungu mwenzake. Haya mambo yapo na yanatokea sana huku. Kwa hivyo kuwa mwangalifu na hao wazungu wako!

  ReplyDelete
 16. We anony wa August 19, 2009 6:58 AM. Nimwone family doctor kwa nini? Mi sina ugonjwa wo wote, nyinyi ambao hamtaki kujitambua and to see the truth ndiyo mnahitaji kumwona doctor. By the way pengine umekaa Canada kwa muda mrefu sana na umesahau kwamba huku Bongo hakuna mambo ya family doctor. Familia yako kule Bukoba mna family doctor? Au kwa vile unabeba maboksi Canada kwenye huduma za bure ndiyo unafikiri everybody ana family dr. Kalagabaho!

  Hata wewe mwenye blogu sikuelewi japo kidogo umeonyesha ukomavu. Mimi sina Psychological problems wala nini lakini I am telling the truth. Tena usinitishe na story za uwongo za serial killer. Hata nipate serial killer mzungu ni afadhali kuliko hii myanaume yenu myeusi - liars, lazy, dirty, womanizers and HIV+. What I want to know ni MBONA KILA MAHALI UKIWEKA MTU MWEUSI MAMBO YANAHARIBIKA? Hamjibu swali na badala yake mnaniattack. Jengeni hoja tuone!

  Na shoga yangu mwenye VERY HANDSOME BLACK MAN-VERY TANZANIA umepotelea wapi? Au unahangaika mitaani kufuatilia janaume lako lisizini na kukuletea HIV+? Pole mama lakini zigo ushajitwisha mwenyewe. Waweza lishusha anytime ukitaka. Pole!

  ReplyDelete
 17. AIKA, I always knew there is something wrong with you, tangu zamani, lakini sasa nimehakikisha. Niliwahi kusekia wasomi wakisema SILENCE IS GOLDEN, sasa nimehakikisha. Sentensi chache tu za Anti AIKA zimedhihirisha yeye ni nani: NOT EVEN CONFORTABLE IN HER OWN SKIN. "I WISH I WERE NOT BLACK BECAUSE IT IS A SHAME" HA HA! Namuonea huruma atakaye kuoa au kuzaa na wewe. Yu will never be a good mother unless you get some help. Kwa sababu, if you are not proud of who you are, how will you be able to instil confidence in your own children? AIKA I have seen many people like you: very disturbed individuals who want to be something they are not, and will never be. Matokeo yake ni stress, anger, hate, na low self esteem.

  ReplyDelete
 18. WE ARE UNHAPPY BECAUSE WE NO LONGER HAVE OUR OWN SELF ESTEEM. WE ARE UNHAPPY, BECAUSE WE NO LONGER BELIVE WE ARE SPECIAL MIRACLE, A SPECIAL CREATION OF GOD. WE HAVE LOST FAITH IN OUR SELVES.

  ReplyDelete
 19. "Nothing is so good for an ignorant man as silence; and if he was sensible of this he would not be ignorant."
  Saadi

  MAY BE THAT'S ME...

  But wait........

  "It is worse still to be ignorant of your ignorance."
  Saint Jerome

  ReplyDelete
 20. Aika M (A - Town Queen)August 20, 2009 at 1:57 AM

  Nyie nyote mnazidi tu kunitibua. We anony. wa August 19, 2009 9:30 PM. Nani amekwambia mimi nataka mtoto? Mijitu mingine bwana! Na mimi siamini katika stress, anger, hate, na low self esteem kwani hizo ni constructs ambazo mtu unakuwa nazo akilini mwako. Tangu lini Mwafrika akawa na stress? Umekaa Canada kwa muda mrefu sana kwa sababu ya kukosa makaratasi kiasi kwamba uko detached na real situation ya Bongo. Rudi upaone, maboksi utayakuta tu yanakusubiri kama umeshapata makaratasi.

  Na wewe anony wa August 19, 2009 11:06 PM. Unamleta Mungu wa nini tena? He is the one who CURSED the blacks halafu unamwingiza tena katika mjadala. Ukifanya hivyo mjadala utaenda katika mzunguko and it won't make any sense kwani hakutakuwa na cause and effect implications. Created in the image of God my foot! Inabidi useme Blacks were created in the image of the DEVIL. Hapo nitakuelewa!

  Wewe Changamoto. You are back for more? I thought you declared defeat. Sasa umeibuka na vi-quotation visivyo na kichwa wala miguu. Masikini sijui umeenda maktaba kubukua na ukaibuka na hivyo vi-quotation viwili ili uonekane educated. Nakupa hongera this time though kwa sababu hukuja na arguments za wavuta bangi wa raggae. Umepiga hatua na endelea hivyo.

  Nijibuni: MBONA KILA MAHALI UKIWEKA MTU MWEUSI MAMBO YANAHARIBIKA?????????????????????????????

  ReplyDelete
 21. MBONA MNASAKAMA CHALII WANGU. AIKA WAPE VIPANDE VYAO, WAMEZOEA VIBAYA. NAKUOMBEA MUNGU UIBUKE NA MTASHA HAPO A-TOWN ILI UWAACHIE NCHI YAO YA MA-CHEATERS, LIARS, AND BLACK. KYERUUUUUUUUUU!!!!  S.KIMARO.

  ReplyDelete
 22. Aika. Sijarejea kuendeleza debate. Na naamini nimerejea kuangalia uwezekano wa kujibu maswali uliyouliza. Ni kweli kuna "point" kuwa kwanini sehemu nyingi wawekwazo weusi kunakuwa na tatizo. Lakini tatizo ni kuwa wanakubali kufanyishwa vile ambavyo weupe wanataka.
  Mfano mzuri ni namna tuonavyo vita barani Africa. Kila MUASI anapotaka kupigana anawahi kuchukua sehemu yenye madini ama malighafi. Kisha unasikia wakisema nchi imewekewa vikwazo, lakini walioweka vikwazo wanajua kwa kufanya hivyo watakuwa wameshusha soko la malighafi hizo na ndio maana wanaweza KUZINUNUA kwa bei ya chini kumuwezesha muasi kupata pesa ya silkaha. Ni ile hali ya DIVIDE AND RULE.
  Kwa hiyo tatizo sio kwamba waafrika hawana uwezo wa kuongoza, lakini WANAOPANDIKIZWA HAPO ni kwa manufaa ya weupe hivyo wanaonekana kuwakilisha weusi lakini si ukweli halisi. Ni NJAA inayotusumbua na siwezi kuwalaumu weupe kwa hili. NJAA INAMSUMBUA KAPUKU (japo hata weupe wenye njaa wanafanya mambo ya ajabu saana).
  Kwa hiyo kwangu utaona kuwa "divide and rule" ndio tatizo na inapotokea mtu akataka kuiacha, atakutana na yaliyopmkuta SAVIMBI. Si unajua kilichomsibu? Alivyotangaza kuwa hatauza madini kwa "nchi shirika" akauawa within a week ili aitoe siri?
  Ama jiulize kuhusu vita vinavyoendelea kuwa kwanini kabla havijaanza utakuta nchi hazina hata bunduki za kuwatosha askari wake, lakini wakishasema wanaanza vita, wanapata mikopo ya silaha watakayokuja kuilipa kwa miaka mingi na pia watauziwa chakula maana wakati wote wa vita hakuna atakayelima
  Hao weupe wanachukua advantage ya NJAA NA KUTOTHAMINI UTU KWETU lakini haimaanishi kuwa asilimia kubwa ya weusi ako hivyo. Naamini asilimia chache yenye mamlaka na madaraka ndio wabaya na wanatuchafulia wote.
  Blessings

  ReplyDelete
 23. Aika M (A - Town Queen)August 20, 2009 at 1:56 PM

  S. Kimaro. Hayo maneno yako ni kejeli au? Kama siyo kejeli basi uko sawa. Inachosha sana kuona sisi blacks tangu enzi na enzu hatuwezi kufanya kitu vizuri na kila mahali tunapowekwa ni kuboronga. Hawa black americans wamepata bahati wakapelekwa utumwani huko na baadaye wakakombolewa lakini bado GENES zetu wanazo - wavivu, wachafu, walafi, kwa magonjwa ndiyo wanaongoza na sasa literally wanakula sana na kunenepeana and then die. Angalia kule Carribean - mambo ni yale yale. Tazama Haiti, ooh boy. Kazi yetu kuoneana hata nchi iwe very rich kama yetu hakuna jambo la maana linaloendelea. Mijitu inaiba na kuwaacha wengine hawana cho chote. Yenyewe inafikiri jinsi ya kuiba na nyumba ndogo tu. Maendeleo yatatoka wap? Halafu tunakaa na kulaumu wazungu. Leave the white man alone please!

  Mzee wa Changamoto inabidi sasa nikuvulie kofia. Baada ya heated debate bado upo tu tena kwa ustaarabu. For that I have to admit that you are an intellectually mature person na siyo kama wababaishaji wengine waliojaribu kupayuka hapa . Umepevuka na unayoyasema hapa ni OK but it is only a tip of an iceberg - dalili tu za ugonjwa wenyewe. Mifano hiyo ni ya Afrika, je vipi kwingineko duniani? Don't blame everything on the white man - allover the world. Mzungu ndiye anatulazimisha tuwe mafisadi? Mzungu ndiye anatulazimisha tuwe lazy? Kwa nini hatuwezi kuwa na transparent society? Kwa nini hatuwezi kuwa na viongozi wanaojali watu wao? Kwa nini tusiwe na responsible leaders? Ni kwa sababu ya mzungu? I don't think so. Ndiyo maana mimi naamini kwamba something is inherently wrong with blacks!

  ReplyDelete
 24. Unataka kunijua mimi, ninaitwa MAKIA JOHNSON HOBE simu yangu +49 228 975 60-0 email yangu makiaj@rua-bartiza.org.
  Sijapotea ila nona huna SERA. HIV+ si tusi la kumtukana mtu na hata kama Mungu angenijalia kulikwaa gonjwa hilo bado mume wangu angeendelea kuwa mume wangu. I feel very sorry for you,you are a good for nothing SCHIZOPHRENIC.Huna tofauti yoyote na vichaa wanao tukana ama kuandika matusi kwenye kuta na magari kwakutumia nene la VIUNGO VYA UZAZI VYA MAMA ZAO. You are very pathetic. You really are some FRUMO pole sana. Eti mume wangu huenda ana HIV so what! does that makes him less a man? Kama ulitoswa basi huyo hakuwa RIZIKI yako. Tulia mama JIPANGE SAWASAWA. Haulpi dada wenzako wameshachukuliwa na wazungu utalala makaburini sana na kuishia kufanya mapenzi na mbwa, siye tunapeta na wakwetu hata kama wana nyumba ndogo sijui HIV+ poa lakini tunao wa kuwakumbatia. hayo yote ni maneno ya mkosaji. Hunitishi kwakuniambia eti my beloved black handsome hubby has HIV sijali (SIDANGANYIKI)why don't we for a change discuss fruitfully matters. Kwakuwa huujui ulimwengu unavyokwenda ndo maana wafikiri kwamba watu wakikuqambia kwamba wazungu are not perfect wafikiri wanakudanganya. Wana madanguro kibao kwa ajili ya uasherati na uchafu mwingi tu. Afrika kunaweza kuwa na uchafu wa takataka lakini huku mama ni balaa. Chukua muda angalia SKY news just for a single day you'll see kwa macho ayko ya nyama what we mean.
  Kwahiyo baada ya kutoswa ukamlaani sana yule Chalii na kumuombea apate UKIMWI? na kufikiri kumnyooshea mtu kidole kwamba ana UKIMWI ndo umemtukana sana? Watu wapo na maUKIMWI yao na wanapeta tu, kwahiyo donot concentrate on that mama. I have closed mjadala nawe, sema sana mpaka mate yakauke/andika sana mpka vidole vipate ukoma you will remain hte HONOURABLE PATHETIC SCHIZOPHRENIC.Have a very good day na muache Chalii (your EX) atanue na aliye MREMBO ZAIDI YAKO.CIAO!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
  Makia J.

  ReplyDelete
 25. Bora tumepata mwanga toka kwa AIKAMBEEEEEEEEEE!! ili tuweze kuendelea na kuondokana na laana tulizo nazo waafrika wote tunatakiwa kuondoka Afrika na kuolewa au kuoa Wazungu, na Wazungu warudi wachukue nchi yao. Asante sana Aika nami natafuta mzungu nikimpta sirudi NG'OOOOOOO.
  Lakini nikifikiri mara mbili nakuona bonge la MWEHU you stupid Eupoean in a black skin? Ulaaniwe kwakuwa huna hesima kwa wazazi waliokuzaa. Au wewe ni yatima? Haya hivyo you are still OBLIGED kuwaheshimu na kukuleta duniani na ukatua AFRICA. Poleeeee!!!!!!!!!!!!!

  ReplyDelete
 26. Naona mjadala huu umeharibika sasa. Tuacheni matusi kama wewe anony. wa mwisho. Hatuwezi wote kuwa na mawazo yanayofanana na huyu Aika anayo haki ya kuwa na hayo mawazo na msimamo wake. Matusi kamwe hayasaidii cho chote. Ndiyo maana wazungu (ambao Aika anawapenda sana) wana msemo "Don't argue with a fool. People might not notice the difference" Ndiyo, wakati mwingine kukaa kimya ndiyo njia bora ya kushinda mjadala na kupomorosha matusi mara nyingi ni dalili za kutokomaa. Tuonyeshe kujizuia na tuelewane kutoelewana vizuri. Naamini katika uhuru wa kila mtu na huwa sipendi kubania comment ya mtu lakini matusi nitayazima.

  ReplyDelete
 27. Masangu Matondo Nzuzullima it's getting hot in here. Asante sana kwa kuongoza mjadala mkali, na kwa kudimisha freedom of speech.

  ReplyDelete
 28. Anti AIKA anasema, "NANI AMEKWAMBIA NATAKA MTOTO?" hii kauli inanikumbusha hadithi za Sungura mjanja, sizitaki mbichi hizi. Kwa hasira ulizonazo you don't deserve them at all. You might end up abusing them.

  ReplyDelete
 29. Aika M (Queen wa A-Tauni)August 21, 2009 at 1:28 AM

  Aika mimi queen wa A - tauni nipo nimejaa ngwe na wala hamnifanyi cho chote. Naona sasa hoja zimewaishia na mmeanza kuporomosha matusi - dalili ya utoto, ujinga na upwelepwe. So far ni Mzee wa Changamoto pekee na Nzuzullima ambao angalau wamejaribu kuweka mambo katika perspectives. Wengine ni kuropoka tu - mpaka wengine mmefikia kujifanya madaktari na psychologists. Hopeless. Huu ni msimamo wangu - watu weusi tumelaaniwa, tuko wavivu, wachafu, maneno mengi la maana hakuna, magonjwa kibao, waongo n.k, n.k. Uthibitisho wa msimamo wangu ni kuharibika kwa mambo kila mahali mtu mweusi anapotia mguu. Haiwezekani bara zima (linalokaliwa na weusi), bara ambalo ni tajiri kabisa liwe hopeless namna hii. Afrika ingekuwa inakaliwa na wazungu naamini mambo yangekuwa tofauti. Ni kosa kuwa na msimamo wa namna hii mpaka mniandame tena bila hoja bali matusi? Inakuwaje hata mtu mweusi aliyeko nje ya Afrika - Marekani, Ulaya, Australia mambo ni yale yale? Mimi ni mweusi lakini siwezi kujitia katika "fog" kwamba eti we are the same na wazungu. Nope! Ndiyo maana walitutawala hawa and looking back at it, I think we deserved it. Shameless beasts!!!

  Na wewe shoga yangu mwenye VERY HANDSOME BLACK MAN-VERY TANZANIAN (MAKIA JOHNSON HOBE simu +49 228 975 60-0). Ukichukua MAKIA, ukatoa M ya mwanzo na kubadilisha mpangilio wa alphabet kidogo unaweza kupata jina zuri kuliko yote (AIKA!) na kuachana na jina MAKIA lisilo na ladha wala maana yo yote. Nakushauri ufanye hivyo. Badilisha jina lako legally angalau uitwe AIKA! Hata kama uko very ugly, watu wakisikia AIKA they may think kwamba you are something even though you are NOTHING!

  Mbona nimepiga simu haiingii? Au uko kwenye kubeba maboksi huko Ujerumani? Kweli wewe ni HOBE na sina haja ya kuendelea kujibizana nawe kwani napoteza muda bure tu. Umefikia kuandika hivi, nanukuu"...Haulpi dada wenzako wameshachukuliwa na wazungu utalala makaburini sana na kuishia kufanya mapenzi na mbwa, siye tunapeta na wakwetu hata kama wana nyumba ndogo sijui HIV+ poa lakini tunao wa kuwakumbatia..." This is the lowest a real woman can go. Peta na HIV+ yako ya kujitakia mama. Nakutakia kifo chema siku hayo madawa ya kurefusha maisha yatakapounguza liver yako. Wanawake kweli tunayo safari ndefu ya kwenda ili kujikomboa. I doubt hata kama una fununu na hoja zo zote za maana na jinsi mjadala huu ulivyoanza. Kwangu mimi wewe ni LOSER na mtu aliyekata tamaa. Nitaendelea kujaribu kupiga na ole wako nikupate au huyo HIV+ mwenzio VERY HANDSOME BLACK MAN-VERY TANZANIAN. Njoni mfie nyumbani. Msisubiri mfie huko halafu muanze kusumbua watu kuchangishana ili kusafirisha maiti! Kalagabaho HOBE!!!

  Na wewe anony. wa mwisho, unashangaa mtu kutotaka mtoto? Yaani majitu mengine bwana? Mimi nilikuwa sijui kama ni lazima mtu kuwa na mtoto. Ninyi watu mnaotaka kuwafanya wengine wafikiri na kuwa na myopic view of the world kama yenu mnanishangaza sana! Mtu akiwa na different views basi huyo ameshageuka adui,mnajivika na udaktari wa papo kwa pao na kum-diagnose SCHIZOPHRENIC na upuuzi mwingine. Mbona hivyo? Kila mtu huru is entitled to his/her msimamo na badala ya kutoa pointi mnaporomosha matusi. We anony. wa mwisho pengine ulikuwa abused ndiyo maana uko hivyo. Ulikuwa altar boy nini na wenye majoho walikutenda? Ndiyo, mimi sioni faida ya kuwa na watoto katika ulimwengu wa sasa. Kama una hoja zitoe na siyo kuropoka upupu hapa.

  Ni lazima niseme tena. Mimi Aika (Queen wa A-Tauni) nipo. Anayetaka tuonane aje tukutane A-Tauni, accomodation na chakula juu yangu. Na nitaendelea kupambana nanyi mpaka mwisho. Leteni hoja na matusi yenu nipo navisubiri!!!

  ReplyDelete
 30. MR. Matondo, naomba uniunganishie kwa AIKA. Huyu ndie mwanamke ninae muhitaji kwa maisha ya ULAYA. Kwa sababu yupo Africa na tayari ni mzungu. Akifika hapa haitaji darasa la intergration.

  ReplyDelete
 31. Aika kamwe huwezi kupota mtoto mimba zote ulizoporomosha. You donot have a woumb anymore labda UASILI. Hayo ndo madhara ya kuchezea ujana wako. Pole sana. Wewe ndo chanzo cha kuharibu mjadala kwaajili ya mawazo yako machafu ambayo kimsingi tulitakiwa kukaa kimywa lakini tulishindwa kutokana na kutaka kukusaidia tu. Kwakuwa tunakujali na lengo ilikuwa kukunyoosha. Bakia hivyo ulivyo huenda kwa muujiza anaweza kuwa chachu ya maendeleo ya bara la Africa. Kwa uungwana wako waonaje ukinyamaza kwani SASA TUNAKUBALIANA NAWE. KILA LA HERI

  ReplyDelete
 32. Anony. wa August 20, 2009 5:59 PM. Ni kweli hapa kulipata joto kidogo lakini nadhani tunaendelea vizuri. Asante kwa kuchangia.

  We anony. wa August 21, 2009 6:35 AM. Aika mi simfahamu. Kwa vile nyote mpo hapa, mbona msitafutane? Najua maneno yako hayo ni satire. Aika ngangari eeh! Peke yake amesimama kidete kupigania msimamo wake "usiokubalika" na wengi kwelikweli. Utamuweza mwanamke wa aina hii? Kumbuka pia kwamba yeye hataki weusi na sina uhakika kama wewe ni mzungu! Kazi ipo!

  ReplyDelete
 33. Aika M (Queen wa A-Town)August 21, 2009 at 10:37 AM

  Aika (Queen wa A-Town);
  Naona bado mnarusha vijembe. Wewe unayenitafuta kwa kejeli weka e-mail yako hapa halafu nitakuandikia. Mimi siogopi mtu. Ndiyo maana yule mchovu wa Ujerumani - the ugly MAIKA kanywea! Na wewe Nzuzullima unanijibia. Mimi sihitaji msaada wa mtu. I can fight and fend for myself and I don't need your help. Anayenitafuta nipo na kama uko A-Tauni tunaweza hata kuonana tukanywa chai na kuargue ana kwa ana. Pengine hoja za ana kwa ana zitakuwa hazina matusi wala vijembe.

  Na wewe anony. wa August 21, 2009 9:13 AM, nilipokuwa ninatoa hizo mimba ulikuweko? Na umejuaje kwamba nimeshatoa mimba, na kwamba mimi ni mzee (nimechezea my youth?). Mijitu mingine bwana. Kwa vile dada zako wameshatoa mimba basi unageneralize hata kwa watu usiowajua. Kugeneralize mambo ni sign ya mental dullness and surely you are one of them. Hata kama nimetoa mimba wewe inakuhusu nini? Eti mnanijali na lengo lenu lilikuwa kuninyosha - jinyosheni kwanza nyie. Toeni kwanza vibanzi in your eyes. Mkiweza kupata jibu la kwa nini kila mahali akiweko mtu mweusi mambo yanaharibika, mtakuwa mmegundua formula ya maendeleo Afrika na kwingineko duniani waliko blacks - US, Carribean, Australia kwa ndugu zenu Aborigines mpaka Papua New Guinea. Jibu la hili swali ni critical kwani mkiendelea katika paradigm mliyonayo ni wazi kwamba you won't go anywhere. IT IS NOT WORKING! Kaeni mpige akili na mkishapata sababu inayomfanya mtu mweusi awe masikini, mchafu, mvivu, maneno mengi, mpenda kufanyiwa vitu na ombaomba POPOTE DUNIANI basi mkae chini mtafute paradigm mpya itakayochange the way you view the world and this might change things. Lakini mkikalia mambo ya wewe ulishatoa mimba, wewe ni schizophrenic, wewe ni mjinga, mtakuwa mnazunguka pale pale mkiwa na kamba yenu ya upumbavu mliyofungiwa shingoni na mzungu au pengine ni laana ya Mungu aliyewaumba mi sijui. Please, think outside the current paradigm na mtaona matunda yake.

  Mimi niko tayari kukaa kimya mkiacha kunichokonoa. Mkiendelea kunichokonoa na huu upupu wenu daima nitaendelea kujidefend hata hii ishu iendelee kwa karne nzima. Ma wewe owner wa blogu usijaribu kubania comment ya mtu. Hiyo itakuwa ni dalili ya woga usio na maana. Acha niwafanye wafikiri hawa wasiofikiri!

  ReplyDelete
 34. Aika, una inferiority complex iliyoshindikana. Ila mimi kama msichana niliyeolewa na mzungu, wazungu wanapenda wanawake wa kiafrika wanaojivunia utamaduni wao sio ma sell out kama wewe. lo...pole mama, Unahitaji msaada mkubwa. Acha kujichukia. Inaonekana una akili nyingi lakini your personal hatred is blocking your vision. Honestly nenda kwa psychologist.

  ReplyDelete
 35. Jamani mlishindwa Aika? Hatujajibu swali lake? Ukweli ni kwamba kizazi cheusi kina laana! Huwezi kusema ni historia ya kutawaliwa, Huwezi kusema ni mfumo wa uchumi! Na huwezi kusema ni Mungu (Kwani dhana ya Mungu kwa wanaoamini ni Mungu wa haki)Miaka karibia 50! toka tutoke mikono mwa wakoloni, lakini tunaendesha gari letu kinyume nyume!

  ReplyDelete
 36. kweli waafrika ni ma-lunatic.mimi siamini kama nyny wote hamumwelewi Aika!!.anauliza kwanini popote alipomtumweusi kuna matatizo?.swali ni vivid and clear.mnabaki tu kulalamika bila kujibu hoja za kisayansi.mwanasayansi na mtaalam wa genetic,amewahi kunukuliwa akisema kutokana na majaribio ya kisayansi,amegundua ubongo wa mtu mweusi ni hafifu zaidi ya yule wa mtu mweupe.ikumbukwe huyu mwanasayansi literature zake zinasomwa masecondary na vyuoni.
  uchunguzi pia umegundua ,nchi maskini kuliko zote duniani ni za watu weusi,viongozi wapenda madaraka na kukalia demokrasi wanaongoza ni waafrika.mfano mobutu,bokasa,mugabe na wengine wengi.kuhusu magonjwa subsaharanafrican countries wanaongoza kwa umaskini wa kupindukia,vita,na ukimwi na malaria ikiua maelfu.sitaki kugusia huko ulaya kwenye hili.hivi dini zote takatifu zinatoka kwa watu weupe hili hamwezi bisha.nashkuru kidoogo babu wa loliondo anatibu ngoma nimtu mweusi labdamungu aliona tunakwisha akabadili kibao kidoogo ila sina hakika hapa. na mungu anaeabudiwa ni mzungu,wenye nywele ndefu.cc tupo tayari kuchukiana wakti wao wanaelewana.tukieenda kwenye fashion,mwanamke mweusi natengeneza nywele ziwe kama za mzungu zianguke kwenye uso atingishe kichwa kwa madaha zirudi nyuma.mawigi,makalkiti,wave,mamisi karibu wote wananywele za kizungu.sjawahi ona dawa ya kuji-black,ila za kujichubua uwe mweupe tunazijua.nyny mnadhani michael jackson ni mzungu?lugha nazo za kizungu ndo zinaheshimiwa,kiingereza,kifaransa,kiarabu.waafrika leo wanavaa hijabu kama wako jangwani kwenye vumbi.utumwa ambao wazungu wanadai lilikuwa janga la asili kwetu limeaathiri waafrica kuliko kundi lingine ulimwengu wote.ieleweke unaposema janga la asili ni kama tetemeko la ardhi,mvua ya mawe ambapo binadamu hanamaamuzi nalo.tunadai wazungu(caucausian)ngozi zao haziwezi vumilia jua na ni wadhaifu,lakini wao ndo wanaonekana wanaweza kupambana na nature yoyotekuliko mtu mweusi. wazungu walijaribu kutu-civilize(kutustarabisha)sisi na nyani.walimvalisha nguo nyani na sisi pia.walimpeleka nyani mwezini.lakini sisi tukawa bora kuliko nyani.wazungu walituletea mungu na sasa wanatuletea ushetani. Ufrimansoni,na uchafu wote.yah tuko tayari kuiga.hata nyie mlioko ujermani,Canada mnajiona wasomi na watu wajuu kwa kuwa mko ulaya kwa wazungu.na hata mkidai hamjioni sisi tulioko bongoland na afrika tunaona nyinyi ndo mmeshawini kimaisha huu ndo ukweli.wachaga si watu wa kwanza kugundua mlima Kilimanjaro ni wazungu.kama mlienda ulaya kwa usomi wenu.lazima swali hili mlijibu na mkapata marks ktk shule zetu za kata huku afrika. Tulianza karibu sawa kiuchumi na china lakini leo china ni namba mbili duniani.kama tatizo ni ujamaa mbona Russia,china ndo waalimu wa huo wametoka.wekeni hoja za kulinda ngozi nyeusi,mimi nimeona moja tu ni ugunduzi wa dawa kijijini samunge liliondo mkoani arusha.ambapo hata baadhi ya dini za kizungu bado zinampinga.

  ReplyDelete
 37. Ni watu wachache cku hizi wanamajina ya kiafrika,kama shambagumu,walinguzo,nguvumawe, mhogo mchungu,waafrika sku hizi wanawapa watoto wao majina ya kizungu kama,abdallah.livingstone,nk.utastaajabu pia hata yeye mwenyewe hawezi ku-pronounce vizuri jina lenyewe na maana yake pia hajui.Sishangai kuona wamasai wanacheza mbele ya raisi wamarekani na kuonyeshwa kama wanyama pori wa mbugani kwa kisingizio eti tunatukuza mila na utalii,huku vongozi wao wa kiafrika wamevaa suti iliyotengenezwa ulaya.kama ni mila wangevaa basi kama mfalme mswati.na wao wavae rubega.Miongoni mwa matatizo ya kiafrika ni hili la unafiki.si ajabu utakuta mtu anamuhudumia ndugu yake anayeugua ngoma akikubali mgonjwa kukooa mbelee yake hatimaye naye anjikuta kaambukizwa, akijidai anamjali saana.Kunawa kwenye bakuli moja wanaanza wakubwa then watoto,eti ni undugu na mshikamano,bila kuangalia tunaambukizana magonjwa kama minyoo,nk.
  Na si ajabu mtu kutetea uafrika wake ili watu wamwone ana busara saana,wakati ukweli anauona.ni bora ukijua namna ya kujikosoa ili ubadilike.Swala la kujikubali ni la msingi lakini kwa hii mada lazima tuwe wa kweli. Kwani ukweli ukuweka huru.hauwezi kutatua tatizo kama hujui sababu.wachaga waliacha kucheza ngoma za kienyej baada ya kugundua hazina mantiki wakaanza ku-hustle.wakati kuna makabila yakakumbatia ngoma mapenzi,na uchawi.si ajabu kukuta na mtu anakupiga biti.. usicheze na mimi,nimeaga kwetu’’ uko kuaga kuna maana ya ushirikina tu.utakuta tangazo mganga na mtabiri toka sumbawanga.,yaani wao ni uchawi tu wanajua huko kwao.ni juzi tu wameanza kuelewa ubaya wa kuwa mnafiki.jitambue katika mfumo wako wa maisha ili uweze kutatua matatizo yako.huyu dada wa A-town nampa bigup sana.Kama utaanza kubadilika utaweza kubadilisha wengine,na hii inaanza pale unapojipima na wengine kama uko pouwa ama la. Ni kweli wazungu ma-serial killer wapo na wala watu pia, nk, but huku afrika tumewahi kuwa makabila yanayotaka kumzika mtu akiwa hai amsindikize rafiki yake aliefariki.pia yanayopiga mwanamke na kumuua kwa madai kupiga ni upendo.ukeketaji leowasomi wanadai ni mila potofu lakini ilikuwa mila ya msingi enzi hizo ingawa hii tabia bado haijaisha.si hapo tu kuna tabia ya kurithi wajane,haangalii kama mume kafa na ngoma ama la!kuna mila za kutakasa wazee(widow cleansing),Mijitu isiyotaka kubadili katiba kama tized,mfalme mswati na kuoa mabikira kila mwaka ile ndo dalili kuu ya mtu mweusi,mnadhani hii mila ya waswazi ina akili au ni umalaya wa jadi?kuacha madaraka wengine watawale imekua tatizo kuu la watawala afrika.kama ugandaZimbabwe kwa Mugabe na huu ni unafiki na ubishi wa kujida isisi waafrika tupo sahihi,mwisho wa siku tunasababisha vita ya wenyewe kwa wenyewe.kisingizio kikubwa ni unafiki wa kudai sisi ni wazalendo.mijitu iliyojaa roho za kichifu na tamaa.haitaki mtu aone mbali.inataka dunia iamini wao waliumbwa kutawala duniani.Ndo maana hapa bongo watu wanatunza chura na kuwapandisha kwenye ndege mpaka marekani,na kukataa wakazi kupata umeme eti chura ni maeneo ya chura yaani chura anathamani kuliko binadamu?!!
  Scientific facts zinathbitisha kuwa ukizaa na mzungu una-upgrade uzao wako.nani asiependa kuwa na watoto machotara?!.kwa hili naliunga mkono kwako dada Aika.bigup kwa kugundua hili mapema.
  Tuache unafiki waafrika tunachemka duniani saana tu.labda ni kutokana na kuumbwa na ubongo hafifu.mafrimansoni wanaamini cc ni kizazi cha mtoto alielaaniwa wa nuhu. Mwanahiphop wa marekani Eminem aliwahi kutuhumiwa kwa kuponda wanawake weusi akidai watakupenda utakapokuwa na kitu.uchunguzi nchini uingereza unadai asilimia kubwa wanawake weusi wanapenda vya dezo na tegemezi kwa wanaume.kwa mfano,ukienda out na mwanamke mweusi gharama zote utalipia wewe mwanaume.lakini kwa wanawake wa kizungu hawapendi kuwategemea wanaume kwenye kulipa matumizi na ikitokea umelipa leo next time lazima atakuahidi kulipia.hii ni dalili ya mtu mweusi kupenda vya dezo.hata mimi nataka kuoa mwanamke wa kizungu tena mwakani sitaki mweusi wanapenda kupiga mizinga,mara nipigie.naomba salio,shenz type staki hii tabia.

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU