NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Saturday, August 22, 2009

VYUO VIKUU BORA VYA MAREKANI HIVI HAPA

Kila mwaka gazeti/shirika la U.S News and World Report huchapisha orodha ya vyuo vikuu bora hapa Marekani. Baadhi ya vigezo vinavyotumika katika kuandaa orodha hii ni pamoja na upatikanaji wa mahitaji muhimu (waalimu, vifaa n.k), idadi ya wanafunzi wanaoomba kujiunga na wale wanaopokelewa, idadi ya wanafunzi wanaohitimu pamoja, maoni kutoka kwa marais wa vyuo n.k. (tazama hapa). Kwa mwaka huu chuo nilichosoma shahada za uzamili (M.A) na uzamifu (PhD) katika Isimu (Linguistics) kati ya mwaka 1997 - 2003 kimeshika namba mbili kwa ubora kati ya vyuo vya umma. Hiki si kingine bali ni Chuo Kikuu cha California, Los Angeles - University of California, Los Angeles (UCLA). Chuo hiki kimezungukwa na Hollywood, Beverly Hills na Bell Air; na maisha hapa ni ghali sana. Ni chuo bora kabisa katika nyanja nyingi zikiwezo Isimu, Udaktari, Biashara na fani nyinginezo. Kumi na tano bora ya vyuo vikuu vya Marekani mwaka huu imekaa ifuatavyo:

(I) VYUO VYA UMMA

1. University of California Berkeley
2. University of California Los Angeles (UCLA)
2. University of Virginia
4. University of Michigan
5. University of North Carolina, Chapel Hill
6. William and Mary (Virginia)
7. Georgia Tech
7. University of California, San Diego
9. University of Illinois, Urbana Champaign
10. University of Wisconsin, Madison
11. University of California, Davis
11. University of California, Santa Barbara
11. University of Washington
14. University of California, Irvine
15. Penn State
15. University of Florida (chuo ninachofundisha sasa)

Kwa orodha kamili ya vyuo ya umma tazama hapa.

II. Ukijumlisha na VYUO BINAFSI, kumi bora imekaa ifuatavyo:

1. Harvard University
1. Princeton University
2. Yale University
4. California Institute of Technology
4. Massachusetts Institute of Technology (MIT)
4. Stanford
4. University of Pennyslvania
8. Columbia University
8. University of Chicago
10. Duke

Kwa orodha kamili ya vyuo vyote (umma na binafsi) tazama hapa.

Nyumbani kumeibuka vyuo vikuu vingi sana kwa miaka ya karibuni. Kama tukivipanga kwa ubora sijui itakuwaje. Mlimani naamini kitachukua nambari wani...na vitakavyofuatia hapa wala sina fununu lakini pengine Mzumbe....

3 comments:

  1. Asante kwa infor hizi. This is very important to some of us. Thanks

    ReplyDelete
  2. Bongo nasikia vyuo vipo lakini walimu hawatoshi kwa hiyo ni kawaida kabisa kusikia Mwalimu mmoja anafundisha vyuo vikuu vitatu nasikia. Kama ni kweli sasa sijui hiyo inakuwaje.

    ReplyDelete
  3. Nimepata Provisional admission kutoka chuo kikuu cha NM-AIST. Natafuta sponsorship. please help

    ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU