NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Thursday, September 24, 2009

ATI MABINTI - NI LAZIMA MUOLEWE?

 • Katika jamii nyingi za Kiafrika wanawake walitegemewa kuolewa mara tu walipovunja ungo. Binti ambaye alibakia kuwa nyumbani bila kuolewa alionwa kama mwenye matatizo na kwa kawaida halikuwa jambo jema. Hata mwanamke angekuwa amesoma vipi, hata kama angekuwa na kazi nzuri au uwezo mkubwa wa kiuchumi kiasi cha kuweza kuendesha maisha yake bila kumtegemea mwanaume, bado jamii ilimtegemea aolewe. Kule Usukumani wanawake wa aina hii walikuwa wakiitwa 'bagidatolwa' - wasiooleka!
  • Katika gazeti la USA Today la leo kulikuwa na makala iliyokuwa, mbali na mambo mengine, inaonyesha jinsi ambavyo idadi ya wanawake wenye umri kati ya miaka 15 na kuendelea ambao hawajawahi/hawataki kuolewa imekuwa ikingezeka hapa Marekani. Kwa mfano makala hiyo imebainisha kwamba mwaka 2006 asilimia 27.3 ya wanawake wote hapa Marekani walikuwa hawajaolewa na hawategemei kuolewa. Mwaka 2008 idadi hiyo ilikuwa imefikia zaidi ya asilimia 28.1%. Wanawake wengi wanasema kwamba hawaoni sababu ya kuolewa. Naamini kwamba katika nchi nyingi za Ulaya na kule Skandinavia kwa dada Yasinta, mambo ni yale yale.
  • Kwa vile hizi ni zama za utandawazi - ambapo tunaiga kila kitu cha wazungu, sitashangaa kama jambo hili tutaliiga pia. Hata hivyo nadhani kwamba pengine uigaji wetu hapa utachukua muda kwani nimeambiwa kwamba sasa kuoza mtoto pale Dar es salaam imegeuka kuwa ni nafasi ya wazazi kujionyesha uwezo wao wa kifedha kuanzia kitchen party, send off party (sijui kama hizi ni tofauti) na hatimaye harusi yenyewe. Wazazi wanatumia mamilioni ya shilingi katika shughuli hizi za kuoza watoto wao na pengine kila binti atapenda siku moja kushiriki katika umeremetaji huu wa kitambo na kuwafurahisha wazazi wake. Naamini pia kwamba jamii bado inaiona ndoa kama taasisi muhimu katika ujenzi na utangamano wa jamii. Swali hasa ambalo ningependa kuwauliza wanawake ni hili: Je, kuolewa ni lazima? Kwa nini?
  • Ati, jamii ya leo inamtazamaje mwanamke ambaye ameamua kukaa peke yake bila kuolewa?
  Hebu tumsikilize Daudi Kabaka na wimbo wake Mashuhuri wa Msichana Mwenye Sura Nzuri.

  17 comments:

  1. Sawa kabisa! Kwa kweli kama ulivyosema kuoelewa hasa katika afrika hapo zamani ilikuwa ni mila na desturi binti lazima aolewe na asipoolewa ingeonekana ni aibu kubwa sana katika jamii.

   Na pia ni kweli huko Skandinavia kuolewa si muhimu unaweza kuona watu wanaishi pamoja lakini hawajafunga ndoa,lakini wana watoto. Hili swala kwangu mimi limekuwa ni utata kidogo kwani leo wanaishi pamoja na kesho wamesambaratika. Swali lako kama kuolewa ni lazima inategemea wapi lakini kwa wengi si lazima na kwa wengine ni lazima. Nimesema hivi kwa sababu kuelewa ni watu wawili wapendao kwa hiyo kama mtu anaolewa basi amempenda yule aliyeolewa naye. Lakini hata hivyo wapo wengi wanoochezea PENZI. wanaamua kuachana baada ya muda au ndo hivyo wanawake wengi wanaamua kuishi bila kuolewa. Ila kama hapa Sweden wanawake wengi wanapenda sana kuwatawala waume zao labda inawezekana ni sababu. naacha hapa ili na wengine waseme.

   ReplyDelete
  2. Kuolewa sio lazima lakini kama umeamua kuishi bila kuolewa ni vema ujiheshimu usiwe chanzo cha kusababisha migogoro katika ndoa za wenzio.kuna wengine wameamua kutokuolewa lakini wanataka watoto si mbaya ni nzuri lakini make sure unakuwa na uwezo wa kuwalea watoto katika maadili mema pia itapendeza zaidi kama utazaa na mwanaume mmoja na sio kila mtoto na babake.

   ReplyDelete
  3. bado naamini katika ile falsafa ya zamani juu ya heshima ya binti kuwa ma mume naye ajenge nyumba yake aitwe mama, labda bado mi mzamani kiaina so nafunga kinywa nafungua mijicho yangu nione wadau wengine wanasemaje.

   ReplyDelete
  4. niko na viva. ndoa ni muhimu kwani dunia nzima inategemea mwanamke. kama unadhani huhitaji kuishi na mwenzio, ebu jaribu kutengana naye ndipo utaona umuhimu. kuna jamaa yangu alimtimua mkewe na kuishi peke yake, sasa jamaa halali tena nyumbani kwake na wala haendi kwingine isipokuwa kwenye kibanda alichohamia mkewe. wakati anayafanya ya kumtimua alidhani hamwitaji kumbe ni zaidi.

   jamaa mwingine alidhani hataki kuoa sasa kavuta kijibinti na anaishi nacho uzeeni.

   ninao marafiki kadhaa wa kike waliosoma. walipegwa chini na wapenzi wao na kudhani hawahitaji kuolewa, sasa wamezeeka na wanawatafuta wachumba kama hawana akili nzuri. wanafika hatua ya kuniambia eti niwatafutie wakati miaka ile waliwakandia wanaume wote.

   ndoa ni muhimu kwa kiasi chake. mimi bado ni mchanga katika ndoa lakini naona kama imenibadilisha sana.

   ReplyDelete
  5. Bongo bado kuna wengi wanaamini ni heshima Mwanadada aliolewa ingawa itabadilika tu kama ilivyobadilika Ulaya na Marekani.

   Ila kasheshe iko mwanamke akiachika. NAAMINI kuna wanawake wengi wako kwenye ndoa wanazoteseka lakini wanaogopa stigma ya kutambulika katika jamii kuwa walichwa na waume zao.


   Ukiondoa hoja za Wasenge ambayo ya ndoa zao ni topiki nyingine tena, mie naamini wanawake ni muhimu sana ingawa hata kama unahisi kuwa nao ni karaha lakini na kutokuwa nao ni bomba la shughuli, hukawii kuanza kulipia wa kulipia mpaka ukamzoea mmoja akawa wa kila siku ingawa unalipia:-(

   ReplyDelete
  6. Mimi kama "msichana" I mean bado sijaolewa, sidhani kama ni "lazima" kuolewa kwa maoni yangu na ninavyoona mimi ila mimi kama mimi "ningependa" inshallah kuolewa (in the future) tho sio lazima, inategemea na maamuzi ya mtu...

   ReplyDelete
  7. Labda niombe fafanuzi ya NDOA kabla sijachangia.
   Maana nilishagongana na "wapendwa" wa Strictly Gospel kuhusu hili.
   Msaada tutani tafadhali. Mkinisaidia TAFSIRI HALISI YA NDOA ntakuwa na upeo wa nini cha kusema
   Blessings

   ReplyDelete
  8. Da Yasinta kaleta hoja fulani isoweza kwenda bila kuzungumzwa ya 'wanawake kuwatawala wanaume'. Anony nae kaleta ingine ya 'ajiheshimu asotaka kuolewa'.Je kuwatawala wanaume na kujiheshimu maana yake nini katika muktadha huu?

   ninaongezea tu kati ile ya MwC aloomba msaada tutani!!!! LoL!

   ReplyDelete
  9. Chacha wambura; wananawake kuwatawala wanaume, ni kwamba wanawake hao hawataki waume zao waseme kitu kuhusu mambo ya ndani ya nyumba yaani wao ndio wenye sauti. lakini hii nadhani inatokana na kwamba wanajivunia wana kazi na mshahara na kama hautoshi basi serikali inawasaidia.

   ReplyDelete
  10. Mimi ni mdada wa miaka 40 sijaolewa na ninaishi Tanzanina. Nilikuwa na mpenzi wangu miaka ya 90, yule kaka alikwenda kusoma Ufaransa ana alizamia huko. Juzi nimepata mawasiliano naye kupitia facebook, tumekuwa tukiwasilia na alinieleza alikuwa kwenye uhusiano na kubahatika kupata watoto wawili wakiume. Ameshakuja bongo kunitembelea na kuniomba tuwe pamoja, kila nikifiria katika umri wa miaka 40 kuenda kuanza maisha Ulaya hainijii akilini lakini ndoa ninaitamani na jamaa hana mpango wa kurudi bongo??

   ReplyDelete
  11. We anony wa mwisho - mdada mwenye miaka 40. Achana kabisa na huyo jamaa wa Ufaransa kwani kutokana na uzoefu wangu katika ndoa huyo jamaa yako kamwe HATAMUACHA huyo aliyezaa naye watoto wawili. Kwa nini alikuacha in the first place? Don't be desperate - utakwenda huko Ufaransa na kuwa frustrated tu. Don't uproot your life and everything you have kumfuata huyo mbabaishaji huko Ufaransa. Utajuta sana na utaukumbuka ushauri wangu huu. Just don't do it!

   ReplyDelete
  12. kwa maoni yangu yote ni maisha kama hujaolewa sio mbaya wala usijione huna bahati au nini na ukiolewa haina maana unabahati ni kawaida tu kwani wengi walioolewa msaada yao midogo ktk famili zao na ukikuta mtu asiyeolewa anaweza akaifaa famili yake kuzidi aliye olewa so mimi naona yote maisha tu

   ReplyDelete
  13. Kama umeamua kutoolewa basi ujiheshimu, usiwe papa la mji na kuanza kuharibu ndoa za wenzako. Kama utajituliza na kuishi kwa kujitandika midori au kuwa na wapenzi ambao si waume au wake za watu mimi sioni tatizo ingawa kusema kweli hutaheshimiwa. Bado kuolewa ni muhimu aisee

   ReplyDelete
  14. Aha!!! Bado msaada tutani kwa msee ya changamoto haijatolewa.

   Da Yasinta, nadhani hapo ndo wamama wanapoharibu wanapodhani kuwa kuwa na kipato ndo ukuwe na fursa ya 'kumkalia' mumeo, lol!

   Nakumbuka mwaka 2002 nilikuwa Karlstad kwa miezi kadhaa nilipata fursa ya kuongea na wamama wa huko...wakanieleza kuwa kuna kitu inaitwa 'sambu' yaani living-lovers kama ulivoeleza hapo juu ya kuwa wamjamaa wanaishi pamoja na kubamba watoto hata bila kuwa na legal back-up (kuoana rasmi).

   sasa swala linabaki palepale, je kuna umuhimu wa kuvuta ama kuvutwa katika ndoa? (usijali sana lugha yangu kwani mie mkurya bwana..lol!

   Nadhani hili ni suala binafsi kulingana na muktadha tofauti tofauti. Na ndo maana kuna usemi kuwa 'walio ndani wanataka kutoka na walio nje wanataka kuingia ktk ndoa' halafu 'ndoa ndoana' ...lol!

   pengine kubwa ni kuwa wengi wetu (wakaka) na wadada tunaingia katika mahusiano na ndoa bila hasa kujua tunachokiendea pengine hamu ya kumega/kumegwa ...lol!

   halafu kuna kaukweli kwa aliyosema kaka kamala kuwa kabadilika, wakati ukifika ntashea nanyi....lol

   ReplyDelete
  15. Suala la ndoa ni very complex. Kila mtu ana sababu tofauti kwanini amejiingiza kwenye maisha hayo. Wapo wamejikuta katika mafungamano ya ndoa kwa sababu za kiuchumi, wengine mapenzi, kutaka kuwa na watoto na sababu nyingine mchanganyiko. Walio wengi wapo ndani ya ndoa bila kujua ni kwanini wako ndani ya ndoa. Ilitegemewa kwamba watu walioko kwenye ndoa basi wasingekuwa waathirika wa UKIMWI lakini ni kinyume chake wengi hupima na kujikuta wako safi lakini baada ya kupata watoto wawili basi maradhi huingia ndani ya chandarua. Huenda mama au baba hakuwa mwaminifu kitu ambacho ni msingi mkubwa katika ndoa, pia hakumpenda mwenzi wake kiasi cha kwenda kuyachezea maisha ya mwenza wake. Ndoa ina maana ya kuyakabidhi maisha yako kwa mwenzi wako sasa ana yathamini vipi ama anayachezea vipi ni maumivu kufikiri. Kama utajiheshimu unauwezekano mkubwa sana wa kulinda maisha yako kulikoni kumpa mtu ambaye hayathami na kubakia bila ndoa.
   Ni bora kuwa singo kulikoni kuwa kwenye ndoa yenye karaha na uasherati uliokithiri. Kama baba na mama wanaheshimu ndoa zao basi ndoa ni jambo la kheri lakini kama hujabahatika kuolewa usiumize kichwa

   ReplyDelete
  16. Hatuna wanasosholojia hapa. Ati, ndoa ni nini? Mzee wa Changamoto anasubiri jamani!

   ReplyDelete
  17. Hallo sis Yasinta hilo swala lakuoana inatokea tu kwa sababu ya maisha, kwa upande wa watu wengine. Nina maana kwa mifano mingi ambayo ndio ya kweli. mimi ni mwanaume nimekuja hapa Denmark mwaka 86 offcourse sikupanga kuoa lakini nililazimika kuoa bila hata kupanga na mtu niliemuoa wala hata nilikuwa simjui lakini kwa sababu mimi nilikuwa na shida ikabidi iwe hivyo. sasa hio ni sababu ya shida na waya wetu wa kibongo wakati ule wa Nyerere kama unavyojulikana.Baada ya miaka miwili ya ndoa nikajikuta nina mtoto tayari nae. Kwa kweli ilikuwa ni sitation hard kwani halikuwa lengo langu kuishi maisha ya ndoa . Baadae niliomba mwenyewe divorce nikawa naishi kivyangu! ajabu eti sasa baada ya kuwa tunaishi tofauti yeye kwake mimi kwangu maisha yakawa mazuri mno na tukawa marafiki na maelewano mazuri sana kupita maelezo ninapokuwa najisikia namwambia anakuja na yeye anapojisikia ananiomba niende yaani raha kweki kweli, miaka miwili baadae tukapata wa pili na bado tunaishi hivyo hivyo na mapenzi ni mazuri tu.

   Sasa ninachotaka kusema ni kwamba sio lazima kuoana ndio maisha yananoga , HAPANA. Kwani binadamu wengi hawawezi kuishi na wapenzi au mke/mume kwa ukaribu kiasin hicho ndio maana ndoa nyingi huishia muda mfupi halafu mnaachana, hio yote ni kwa sababu mnaishi pamoja sana. Mimi bado ni baba wa watoyo wangu nawapa mapenzi yote kama baba na wala hawaoni tofauti yoyote ya mimi kutokuwa pale kwa mama yao.
   Hayo ndio mawazo yangu kuhusu ndoa. Na watoto naenda nao sana bongo kama kawaida bila mama yao kujali chochote, na imeiha kuwa mibaba ina niheshimu kama kawaida. Lakini mimi na mama yao kila mtu kwake nikimuhitaji naenda akinihitaji nipo tena tunavinjari kwa eraha zetu.
   MDAU COPENHAGEN

   ReplyDelete

  JIANDIKISHE HAPA

  Enter your email address:

  Delivered by FeedBurner

  VITAMBULISHO VYETU