NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Thursday, September 10, 2009

HATIMAYE IMEKUWA - WAJAWAZITO RUKSA MTIHANI DARASA LA SABA

Hii ni hatua muhimu katika harakati za kujikomboa kwa wanawake wa Tanzania. Juhudi ziimarishwe zaidi kuwadhibiti wanaowapa mimba mabinti hawa (mf. adhabu kali). Tunasonga mbele!

Picha kutoka kwa Mjengwa (Gazeti la Sauti ya Watu Tanzania, 9/9/200). Kwa habari kamili soma hapa.

5 comments:

 1. Hili haliwezi kuwapa kiburi watoto hawa wakike?
  Watoto hawa wa kike hawachangii wenyewe kuingia ktk tatizo hili?
  Binafsi siridhiki sana na maamuzi haya.

  Si wote wanaopata mimba wakiwa mashuleni wanakuwa wamebakwa wala kudanganywa, wengine ni tabia zao tu.

  ReplyDelete
 2. kissima acha hizo wewe.

  kuzaa ni baraka na waache wazazi wasome bwana. mimi nilikuwa mimba na ndivyo wazaliwavyo wengine. waache wasome na nafikiri kuwazuia kufanya mtihani ni kuwaonea wivu wa bure kwani katika jamii zetu kuzaa ni bonge la baraka.

  nikifikiria huru bila kubanwa na kibubusa chochote kile, waache watoto waishi vile wapendavyo na wasome, sio haki kuwazuia masomo eti kwa kuwa wamefurahia ngono uifurahiayo wewe.

  tena wanafunzi wasomao na kupata mimba yaweza kuwa ishara ya kuwa na akiri na ndiyo maana wanafanya ngono mpaka kupewa mimba bila wewe kujua wala kutarajia.

  sioni shida juu ya hili. aliwahi kuniuliza swali kijana mmoja kuwa, wakifanya ngono wakubwa twasema sawa, wakifanya wadogo twasema ni uasherati, uzinzi na matusi lukuki, kwani wao wanatumia viungo gani na sisi tunatumia vipi? si vile vile tu?

  si wanajaribu kama wanafaunction na wao?

  ReplyDelete
 3. Mmh, opinion yangu ni kwamba hii itawa-encourage hawa watoto kuingia kwenye vishawishi kwasababu at least ile "hofu" ya kufukuzwa shule ilikuwepo so number za wanafunzi wenye mimba zikizidi, who is to blame? Remember with more freedom comes more responsibilities. Ni maoni yangu tu

  ReplyDelete
 4. Mimi pia nina maoni yanayofanana kidogo na ya Kamala. Inabidi tukubali kwamba tutake tusitake wasichana hawa "watajaribu" wakati wao ukifika. Pengine swali ambalo inabidi tujiulize ni kwa nini "wanajaribu" - udadisi, maisha magumu, kurubuniwa, au? Na tukijua sababu basi tuamue kutafuta mbinu muafaka zitakazosaidia kupunguza tatizo hili. Haikuwa haki kwa wasichana hawa kunyimwa haki ya kuendelea na masomo wakati wavulana/wanaume waliowapa hizo mimba wakiendelea na masomo na shughuli zao.

  Wamarekani wana hukumu ya kifo "death penalty" na wananyonga watu wengi kweli kila mwaka. Ilitegemewa kwamba hukumu hii ingewafanya watu waogope kutenda makosa makubwa kama mauaji na mengineyo. Utafiti hata hivyo unaonyesha kwamba hukumu hii haisaidii cho chote katika kupunguza uhalifu. Pengine huu si mfano makini kuutumia hapa lakini wazo ni kwamba kuna vitu vingi ambavyo tunadhani kwamba tunajua kwa uhakika madhara au matokeo yake - na mara nyingi vinatokea kuwa kinyume. Sitashangaa kama hatua hii itawafanya mabinti kuwa na uwazi zaidi katika suala hili.

  ReplyDelete
 5. Suala ni kwamba watoto wa kike wanatakiwa kupewa elimu kuhusu AFYA YA UZAZI na madhara ya kuanza ngono mapema. Kwa asilimia kubwa wengi huzipata kwa kurubuniwa na watu wazima, bikifuatiliwa na tamaa, na hali mbaya kiuchumi ya wazazi/walezi. Kama suala hilo lingezungumzwa mapema basi mambo yanayotokea hivi sasa yasingekuwepo. Enzi zetu hatukuwa tukifahamu watoto wanatoka wapi, lakini sasa huu utandawazi yote yako wazi. Mifano mingi inaonesha kwamba wasichana waliopata mimba na wazazi wao kuamua kuwaendeleza wamefanikiwa. Tukiwaacha watakuwa mzigo kwa jamii. Elimu ni mkombozi tusiwanyime fursa hiyo. Wengine wamepata mimba kutoka kwa watu wa karibu sana kwao wakiwemo baba wa kuwazaa, wajomba, baba wakubwa au wadogo, babu zao, kaka zao, walimu wao. Hali ni mbaya sana tufanye mikakati ya kujua chanzo cha balaa hili. Hata UKIMWI nao unachangia kwanini watu wazima kuwafuata watoto kwa imani kwamba watoto bado ni salama.

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU