NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Friday, September 11, 2009

HATIMAYE KIINGEREZA KUTUMIWA KAMA LUGHA YA KUFUNDISHIA KUANZIA SHULE ZA MSINGI

Mnaionaje sera hii mpya ya elimu Tanzania?
 • Kiingereza kianze kutumiwa kama lugha ya kufundishia kuanzia shule za msingi. Kiswahili kifundishwe kama somo.
 • Shule za binafsi ziruhusiwe mapema kuanza kutumia Kiingereza kama lugha ya kufundishia na baadaye shule za umma/serikali zitafuata.
 • Soma makala hapa chini kutoka gazeti la "The Guardian" la jana.
=======================================
English set to be a medium of instruction in primary schools

By Erick Kabendera

The Guardian, 10th September 2009

 • Use of Kiswahili will be consolidated and that of English expanded
The proposed new education policy has highlighted the importance of using English language as a medium of instruction in primary schools in the country, ‘The Guardian’ has authoritatively learnt.

A draft of the policy, whose copy was obtained by this newspaper this week from impeccable sources, also indicates that the government has given the green light to a section of private primary schools to use English as a medium of instruction due to requests from parents who favoured their children to be taught in English instead of Kiswahili.

The government notes in the report that the use of English had increased due to globalisation, thus necessitating making it a medium of instruction in primary schools in future.

However, the policy points to the heated debate in the country on whether English or Kiswahili be used as a language of instructions at primary school level.

“So there is need to consolidate the use of Kiswahili and expand the use of English as a medium of instruction in primary schools,” reads the policy in part.

It maintains that the languages of instruction would be both English and Kiswahili, but that English would only be used as a medium of instruction in private schools and taught as a subject in most of the public primary schools.

Kiswahili became the medium of instruction at primary schools shortly after independence while English is taught as a subject and used as a medium of instruction in secondary and tertiary education.

However, proponents of Kiswahili as a medium of instruction argue that using English as a medium of instruction would lead to giving the language more emphasis at the expense of Kiswahili.

This school of thought wants Kiswahili to become a medium of instruction from primary school to higher learning institutions.

The policy will be submitted to the Cabinet for approval in two months time before the final draft is relayed to the Parliamentary Social Services Committee for review, after which the Attorney General will prepare a bill from the national policy on education to amend the 1978 National Education Act.

The proposed policy will replace the current Education and Training Policy which has been in use since 1995.

The general secretary of Tanzania Association of Managers and Owners of Non Governmental Schools and Colleges (TAMONGSCO), Benjamin Nkonya welcomed the proposed policy, but said it was unjust for the policy to recommend the use of Kiswahili and English as mediums of instruction at primary school level but limit secondary schools to using English alone.

Nkonya said non-government schools had advised the government to endorse a system which would allow students to use one language as a medium of instruction from pre-school to tertiary level.

“We will make the problem worse if students who are taught in Kiswahili at primary level abruptly switch to English as a medium of instruction in secondary school. The decision will weaken the students’ creativity and their ability to learn new concepts.

“We want the two languages as mediums of instruction to be introduced at the secondary school level so that students may decide which way to go. A student who learned in Kiswahili in primary school should be given a choice to continue learning in the same language until he or she finishes the university,” said Nkonya.

Following failure to include such provision in the draft policy, Nkonya vowed that non-government schools through their coalition would make sure the provision is included before the policy is endorsed by the ministry of education.

Elizabeth Missokia, the Executive Director of Hakielimu, an educational NGO said in a telephone interview this week that NGOs dedicated to education would meet at the end of next week under the Tanzania Education Network (TenMet), a national network of more than 200 members to discuss the proposed policy and give their recommendations.

She said Hakielimu does not favour any of the languages being used as a medium of instruction but said there was need to distinguish between a language of instruction and language of communication.

The country needed English as a language of communication but Tanzanians needed to ask themselves if there were enough competent teachers to teach English as a medium of instruction or as a subject, she said.

“Teachers need to master the language they are using to teach. The quality of education is going down in Tanzania and Africa in general so we need to redefine and reflect what we want to achieve otherwise we will never get anywhere,” said Missokia.

Tanzanians always developed the best policies, but Missokia reckoned that the problem was the implementation of such policies, saying the education policy needed to put special emphasis on improving quality of education and teachers’ welfare rather than focusing on infrastructure development.

“It is important we start enrolling students who score division one and two into teachers’ colleges instead of those with division four…” she said.

According to the draft policy, English will remain the medium of instruction at secondary school level, but a research that was conducted by Martha Qorro, a senior lecturer in languages and linguistics at the University of Dar es Salaam titled: “Does Language of Instruction Affect Quality of Education?” says teachers and students at all education levels are able to debate and discuss and ask and answer questions and therefore generate knowledge when they understand the language of instruction.

“In Tanzania the language of instruction factor has been ignored for a long time and this has had a negative impact on the quality of education…..insisting on using English as the language of instruction in Tanzanian secondary schools and institutions of higher learning does more harm than good towards the provision of quality education as well as language teaching,” she concludes in her research.

9 comments:

 1. sijui kwakweli. japo nakumbuka moja ya sababu ya kuiona shule ngumu ilikuwa ni matumizi ya Kidhungu. walimu hawajui kudhungu wala wanafunzi kwa hiyo mwalimu anateseka saana kutafuta maneno

  ReplyDelete
 2. Ni wazo zuri ukichukulia changamoto tulizonazo za utandawazi, teknolijia na sayansi, lakini tatizo hao waalimu wa kufundisha watoto masomo yote kwa kiingereza tunao. Hawa wa sasa hivi tu ni wa kuokoteza na hawatoshi, kazi tunayo

  ReplyDelete
 3. Mi naona hii itakuwa vurugu mechi tu. Walimu wako wapi? Na kale ka mtindo ketu ka kuchukua watu wanaofeli form four ndiyo tunapeleka wakawe walimu je?

  ReplyDelete
 4. Mmmh no! Kama mwanafunzi wa primary aliyemaliza 2003 nasema sio wazo zuri kabisaaaaaa. Kiingereza kiwe somo kama Maarifa ya Jamii (kama hili somo bado lipo). No offence ila hao walimu...I say no more kaka.

  ReplyDelete
 5. Kama alivyosema Kamala itarahisisha wanafunzi kuelewa kwa urahisi kile wanachofundisha aidha itamrahisishia na mwalimu. Lakini kubwa zaidi ni kwamba kwa kufanya hivyo basi tujue tunatokomeza moja ya vielelezo muhimu vya utamaduni wetu!. wamarekani (weusi) sasa wanaamka usingizini na kutafuta asili yao ikiwa ni pamoja na kujifunza lugha za kiafrika hususan kiswahili. sasa hivi kiswahili kinafundishwa kwenye vyuo lukuki nchini marekani, nasikia hata ujerumani. iweje leo sisi "waswahili" wenyewe tuone hakifai? Profesa Matondo, profesa Ngonyani na mwalimu Mazara nisaidieni jamani! Binafsi nakubaliana na hoja kwamba kutumia kiswahili elimu ya msingi na baadaye kiingereza elimu ya sekondari hadi vyuoni kunachanganya wanafunzi. Mimi nadhani tukiache kiswahili kiendelee kukua (amini usiamini sasa kinakua kwa kasi!) Ili hapo baadaye kitumike kuanzia elimu ya msingi hadi chuo kikuu. I don't believe kama lugha inaweza ku-determine kiwango cha elimu.

  ReplyDelete
 6. Sawa kabisa mliyoyasema wote, Ni kweli kuanza kufundisha kiingireza kuanzia shule ya msingi itakuwa vurugu. Yaani kwanza lazima kuwe na walimu ambao wanaweza kweli kiingereza sio hiki cha kubabaisha kwa kweli tutakula hasara. Ni wazo zuri sana, Na pia nadhani ndio kwa sasa linalofanya wanafunzi wengi kushindwa kuendelea na masomo kutokana na kuanzia la kwanza mpaka la saba wanafundishwa kwa kiswahili halafu kuanzia form one na kuendelea anaanza na lufha mpya kwali hapo ataambua kitu sio kama kuchanganya kila kitu na kutoka na div. IV. Kwa mawazo yangu waanza kwanza na kuwa na walimu BORA hapo labda tunaweza kuwa na matumaini.

  ReplyDelete
 7. kama nia yao itakuwa kutufanya wote tufanane kwakuwa watoto wetu watasoma english medium basi wanatudanganya!walimu wa hii english medium mpya hawako fit.

  ReplyDelete
 8. Kimsingi hata mimi sipingi Kiingereza kutumiwa kama elimu ya kufundishia lakini:

  (1) Walimu wa kukifundisha Kiingereza chenyewe wapo? Kumbuka kwamba kimsingi siye tunachukua watu waliofeli mitihani yao ya kidato cha nne kwenda kusomea ualimu. Nashawikishika kuamini kwamba pengine serikali za Uingereza na Marekani zimetoa donge nono katika utekelezaji wa sera hii. Basi mapesa hayo yawekezwe katika kuboresha maslahi ya walimu kiasi kwamba vijana wanaopata division I na II wavutike kwenda kusomea ualimu. Vinginevyo hakuna kitu.

  (2) Ni ukweli uliothibitishwa kisayansi kwamba watoto hujifunza vizuri na kukomaa kiakili hadi kufikia kilele halisi cha uwezo wao wa kitaaluma pale tu wanapofundishwa katika lugha wanayoielewa ambayo ni lugha ya mama. Pengine hii ndiyo sababu kwamba nchi karibu zote ambazo zimeshaendelea zinatumia lugha zao za mama katika elimu. Vinginevyo elimu yetu itaendelea kuwa elimu ya kukariri tu bila hata kuelewa unachokikariri kina maana gani au kwa nini unatakiwa ukikariri...Tanzania kusema kweli haikuwa na sababu ya kutumia lugha ya kigeni katika mfumo wake wa elimu kama ingekuwa na nia ya kufanya hivyo. Kiswahili kingewezeshwa kingekuwa nyenzo muhimu kabisa ya kutuokoa kifikra na kitaaluma hata kuifanya elimu yetu iwe na maana tena - na Kiingereza kingefundishwa vizuri kabisa na walimu waliobobea kusingekuwa na tatizo lolote. Ngoja tuone utekelezaji wa sera hii lakini si ajabu ikageuka kuwa kizaazaa zaidi.

  ReplyDelete
  Replies
  1. vema kabisa, Watanzania tufunguke akili. siku zote mcheza kwao hutunzwa, na mwacha asili si jasiri ni mtumwa. jamani huu ni utumwa wa kifikra. watanzania elimikeni.

   Delete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU