NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Wednesday, September 16, 2009

HIZI TAKWIMU ZA ELIMU MBONA ZINAKATISHA TAMAA???

Mwaka 2007 - wanafunzi wanaofikia milioni nane (8,000,000) walikuwa wameandikishwa (wanasoma) katika shule za msingi (darasa la 1 - 7).

Lakini....

Mwaka huo huo (2007), ni wanafunzi milioni moja na elfu ishirini na mia tano na kumi (1,020,510) tu ndio walikuwa wameandikishwa (wanasoma) katika shule za sekondari (kidato cha 1 - 6)

Kuna anayejua/anayejali wanakoenda hawa karibia milioni saba (7,000,000) ambao hawaonekani katika shule za sekondari? Na kati ya hawa milioni moja ambao wamebahatika kufika sekondari, ni wangapi wanafika hadi chuo kikuu? Nilikuwa sijui kama bado tuko nyuma namna hii katika suala zima la elimu. Kwa data mbalimbali za elimu Tanzania, tembelea hapa.

6 comments:

 1. Kwa kweli ni jambo la kusikitisha , inawezekana hawa labda wengi wao huishi kupata mimba na hapo ndio huwa mwisho wa elimu yao.

  ReplyDelete
 2. Inawezekana kabisa miaka saba iliyopita waliandikisha watoto milioni mbili tu ila miaka ya sasa ndio wanaandikisha hao miloni 8

  ReplyDelete
 3. Kaka kwa swal ala elimu hapa nchini, serikali yetu haipaswi kujivunia kwa kweli.
  Kuna matatizo mengi sana katika mfumo weu wa elimu, yanahitajika mabadiliko makubwa.

  ReplyDelete
 4. kaka nimesema sana juu ya swala hili. ahsante kwa kuendeleza libeneke.....

  ReplyDelete
 5. Asanteni nyote kwa maoni yenu. Hizi takwimu ni za serikali na sitashangaa kama hazionyeshi picha halisi. Lakini hata picha iliyoonyeshwa hapa haitii matumaini sana kwani watoto wanaopata bahati ya kuendelea na masomo ya sekondari ni wachache mno. Kamwe huwezi kujenga jamii isiyo na uhasama mkali wa kitabaka ukiwa na mfumo hafifu wa elimu kama huu. Sote tunahitaji kujibidisha sana kuhakikisha kwamba watoto wetu wanapata angalau hiyo elimu ya sekondari.

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU