NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Saturday, September 26, 2009

NI LAZIMA TUKOJOE "VICHOCHORONI"?

Mwanafunzi mmoja mzungu aliyekuwa anafanya utafiti kule Tanga, Mbeya na Dar es Salaam alinieleza kushangazwa kwake na tabia ya wanaume kukojoa hovyo hovyo mijini. Swali hilo lilinikumbusha Mtanzania mmoja ambaye alipigwa faini kali pamoja na kupewa adhabu ya kuokota takataka mabarabarani baada ya kubambwa laivu akikojoa katika sehemu ya maegesho ya magari kule jijini Los Angeles. Mtanzania huyu alishangaa zaidi kwamba tabia yake hii ya kukojoa hovyo kidogo imletee matatizo alipokwenda kwenye usaili kwa ajili ya kupatiwa "Green Card". Aliulizwa kama alikuwa amewahi kukojoa tena hadharani. Baada ya miaka saba - bado rekodi zilikuweko kwamba alikuwa amewahi kukojoa hadharani (public urination, indecent exposure)!

Ati, ni kwa nini tunapenda kukojoa mabarabarani na vichochoroni? Ni ukosefu wa vyoo vya umma na miundombinu wezeshi (kama mitaro mizuri, madampo, magari ya kuzoa taka n.k) au ni tabia yetu ya kupenda "uchafu"? Ni kweli kwamba sisi tunapenda "uchafu"?

Huyu mwanafunzi mzungu aliniambia kwamba vikojozi wote wa umma aliowaona walikuwa wanaume na kamwe hakuwahi kuona mwanamke akikojoa barabarani. Nilimpa maoni yangu kuhusu suala hili na kumtaka asifikie majumuisho (generalizations) ya haraka haraka kama mababu zake walivyofanya walipotia guu Afrika kwa mara ya kwanza wakiwa na Biblia zao mikononi huku wakidai kwamba walikuwa wamekuja "kutustaarabisha"

Hawa jamaa hapo juu wamenifurahisha jinsi walivyoamua "kukilinda" kijiwe chao na hili tangazo. Wasiwasi wangu ni kwamba sidhani kama hili tangazo litasaidia cho chote!

7 comments:

 1. I like this. ipo siku natokaga nyumbani na kujibanza sehemu ili nikojoe. noma kama kuna mtu anakuja. huwa nakojoa vichochoroni karibia kila siku na sioni tatizo kwani majani hupata mbolea. inapendeza kukojoa vichochoroni huku unaang alia mimea na hewa safi huuuuu raha iliyowakati mwingine unajamba kwa furaha.

  ina raha yake kukojoa vichochoroni mkuu

  ReplyDelete
 2. Nimecheka kweli nilipofika sehemu ya usaili wakati wa kuomba 'green card' ha ha hah, ila si tabia nzuri kukojoa sehemu ambazo hazijatengwa rasmi kwa ajili ya haja ndogo au kubwa, hii ndiyo inayochangia kuendelea kusambaa kwa magojwa ya kuambukiza hasa kwa kuwa maeneo hayo watu hutembea miguu peku ama kujishughulisha kwa kilimo cha jembe na mikono mitupu. Ipo siku tutajua tu maana na jinsi ya kuzingatia misingi ya afya!

  ReplyDelete
 3. We anony. wa kwanza unayefurahia kukojoa uchochoroni, una nini? Nashangaa mpaka wakati huu kuna watu wanafurahia kukojoa uchochoroni. Majani yanapata mbolea au unayaua. Ungeweka jina lako hapa ningekufuatilia siku moja nikuripue viboko mpaka maji uyaite mma!

  ReplyDelete
 4. I HATE THIS HABIT!!!!!!!! KHA!!! Its disgusting...ni hayo tu ila anayekojoa vichochoroni...kuna siku jitu zima anakojoa kwenye ukuta wa shule...i was like wtf????...excuse my language but guys...its DISGUSTING...STOP IT IF YOU ARE DOING IT!!!...sorry kaka Masangu lakini habari ndio hiyo...hehehehe

  ReplyDelete
 5. Huyo Anony wa kwanza nimemfahamu na ntamfuatilia...na ntawapweni ripoti..lol!! Yawezekana ni mmoja wa wale walo-embrace concept mpya ya ecological sanitation toilets ambapo unatenganisha mkojo na haja kubwa na kisha kuitumia kulima japo concept hii imeleta mashaka kwa jamii za kiislamu ambapo kwenda choo lazima kutumia maji na imebidi wamjamaa wakune vichwa ku-design vyoo vya namna hii kuweza kuwa na vile vinavyowafaa ndugu zetu wa kiislamu!


  Masangu, huyo zeruzeru (samahani-mkurya hatofautishi kati ya watu hao na maalbino..lol) ulozungumza ambaye alifanya utafiti Tanga, Dar, na Mbeya alikueleza kama hao watu alowaona wakijinafasi vichochoroni walikuwa wamekula ugimbi ama walikuwa hawajalamba ulanzi? manake yawezekana akawa amekutana na walevi kwa asilimia 90 akajumuisha wote kuwa wanamaindi saaaana vichochoro.

  pamoja na kuwa kuna wapendao kujikamua vichochoroni, lakini ukweli unbaki kuwa miundombinu kwa ajili ya haja ndogo na kubwa zinapatikana kwa shida na hata zikipatikana ni nongwa. Hata pale zinapokuwapo na wanatoza mapeni huduma inakuwa haina 'value for money'. na kwa wale bahiri kama wapare (Da Koero na Mt Simoni na wengineo, sina nia ya kugombana nanyi...pengine nyie siyo wabanifu..lol), wanaona wakimbilie vichochoroni badala ya kutoa bati (sh 100) ama 200 kwa haja.

  Halafu yawezekana wanaume woote asilimia 99 wanaokojoa vichochoroni ni wakristo kama Kamala na wapagani!!!!lol! Kwani waislam ni lazima watumie maji kunanihii, ama!!

  ReplyDelete
 6. Chacha mimi na ukristo? astagahfuraruai

  duh sina cha kusema ila vyoo vingine kusimama na kuviangalia muda woote wa kutoa kojo, waweza jibanza kwenye ukuta wa jirani

  Subi, ntakuletea picha za kuta zilizoharibiwa na mikojo

  ReplyDelete
 7. Serikali ya wanafunzi hapa chuoni imepatwa na kashfa baada ya kubainika kuwa kiongozi wake mmoja aliwahi kukamatwa na kupigwa faini kwa kukojoa hadharani (public urination). Naona jamaa wamemjia juu sana na sijui kama atajiuzuru. Sasa wanasema kwamba watakuwa wanachunguza wasifu wa wagombea kwa makini zaidi ili kuepuka kuwa na vikojozi wa barabarani katika serikali hapo baadaye. Kazi kweli kweli!

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU