NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Thursday, September 24, 2009

KABURI LA WILLIAM SHAKESPEARE LINAHITAJI MATENGENEZO - LA SHAABAN ROBERT JE?

(1) Paa la kanisa alimozikwa William Shakespeare - yule mwandishi mashuhuri katika fasihi ya Kiingereza (kule Stratford-upon-Avon) limeoza na linahitaji matengenezo yatakayogharimu dola 80,000 za Kimarekani. Matengenezo hayo yanategemewa kuanza mara moja!

(2) Hapa chini ni kaburi la Shaaban Robert - yule mwandishi bora kabisa katika fasihi ya Kiswahili. Kwa nini William Shakespeare aenziwe vile na Waingereza na sisi tumfanyie hivi Shaaban Robert wetu? Mwamko wetu wa kitamaduni uko wapi? Makaburi ya akina Chifu Mkwawa, Kinjeketile, Mtemi Mirambo na mashujaa wetu wengine tunayatunzaje kwa ajili ya vizazi vijavyo? Hata hili nalo mpaka tupate wafadhili? Kwa uchambuzi wa kina kidogo kuhusu suala hili gonga hapa.

4 comments:

 1. Haya ndio MAWAZO YAKINIFU. Asante Mwalimu. Pengine cha kuanza kujiuliza ni kuwa wangapi wanamthamini Shaaban Robert nyumbani? Nina hakika wabunge wengi wametumia kazi zake kujikweza mpaka walipo na sasa wamefika hawamkumbuki. Serikali imemtumia kuielimisha jamii (enzi hizo) kwa kutumia kazi zake katika mitaala lakini pumziko lake halithaminiwi. Nadhanikuna UOZO mwingi wa kusafisha mwakani (japo sitashangaa kuona uozo ndio unaotumika kupiga kura tukitegemea kupata kilicho bora)

  Yaani TANZANIA YANGU inasuuza nguzo safi kwa maji machafu.
  Asante kaka na KARIBU TENA JAMVINI

  ReplyDelete
 2. Kaka hapo umenena, inabidi lipigwe baragumu ili wadau wa kiswahili pamoja na serikali walione hilo....Ni aibu kusahau yale yaliyofanywa na mzee huyu katika kukienzi kiswahili chetu....

  ReplyDelete
 3. ndio. kumkumbuka ni lazima angalau tusome mashairi yake kama hatuwezi kulijengea kaburi

  ReplyDelete
 4. na bado yawezekana bibi yake Kamala aitwaye Maria akifa tu hatutoona tena wala kusikia hotuba zile za Wosiya wa Baba zinapigwa katika ile redio ya UKWELI na UHAKIKA!!!, lol!

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU