NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Tuesday, September 22, 2009

KUMEKUCHA: KAMALA LUTANISIBWA LUTABASIBWA KUMVAA DR. KAMALA BUNGENI

Kutoka kwa Mjengwa. Pichani ni mwenzetu Kamala Lutatinisibwa nyuma yake kushoto ni Mbunge Ole Sendeka wa Simanjiro, mahali ni kijiwe cha Royal Chef, Lumumba. Taarifa zilizonifikia ni kuwa Kamala Lutatinisibwa keshokutwa alhamisi atakuwa ni miongoni mwa wabunge wa upinzani kwenye Bunge la Vijana litakalofanyika pale Ukumbi wa Karimjee Dar. Niliongea nae kwa simu jana na amenihakikishia kuwa kati ya mambo atakayoyavalia njuga ' atamvaa' Mbunge na Waziri wa Afrika Mashariki Dr. Deodoros Kamala ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo lake. Bila shaka ni kuhusiana na suala la Muungano wa nchi za Afrika Mashariki na nafasi ya Vijana wa Tanzania kwenye soko la ajira. Je, safari ya mwenzetu Kamala Lutatinisibwa kwenda 'Bunge la Kweli Kweli' imeanza?!

Kamala Lutanisibwa Lutabasibwa - Kweli kumekucha! Nakutakia kila la heri, na kama alivyosema Mjengwa basi huu uwe ndiyo mwanzo wa kumwangusha Dr. Kamala ili uingie kwenye 'Bunge la Kweli Kweli". Hili likitokea nitategemea kwamba utaendelea kublogu na kwamba hutatugeuka na kutupa mgongo kama ilivyo kawaida kwa wale wanaofanikiwa kukifikia kilele!

3 comments:

 1. Mmmmmh!Good luck,Kamala nenda kapambane nao hao,tunataka watu kama wewe kaka.

  ReplyDelete
 2. Kamala nakutakia yote mema uwe na nguvu nyingi. Tupo pamoja wangekuwa watano kama wewe basi labda tungesonga mbele.

  ReplyDelete
 3. Kama nalikuwa naota vile manake wakati na-post comment yangu sikujua hili latokea. Hii ni poa kaka.

  Kandamiza kwa kwenda mbele ng'wanawane

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU