NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Thursday, September 3, 2009

NI KWELI OBAMA ANAJARIBU KUMFUFUA KARL MARX KULE MAREKANI?

 • Obama anapigwa vita vikali sana na wahafidhina wa chama cha Republican; na mapendekezo yake ya kuubadilisha mfumo wa bima ya afya ili kumwezesha kila Mmarekani kupata tiba anapougua yamewasha moto mkali wa upinzani. Tayari ameshapachikwa jina la mkomunisti.
 • Wakati mabishano haya yakiendelea deni la taifa linazidi kukua, vita kule Afghanistan (ambavyo sasa ameanza kulaumiwa kwa kuviendeleza) haviendi vizuri, majimbo hayana pesa za kutosha, hali ya maisha ya Wamarekani (waliozoea raha ajabu) inazidi kuporomoka...... Hali hii inawafurahisha sana wahafidhina kwani wanafikiri kwamba pengine wataweza kumwangusha katika uchaguzi wa mwaka 2012 na kuwa rais aliyeshindwa. Tangu hapo siasa ni mchezo mbaya ati!

4 comments:

 1. so suluhisho la hiyo maneno ni kuacha watu wafe na waendelee kuionea Cuba wivu kwa kutoa first class health services....!!

  Kwa hiyo wanamwona kama kaJK fulani vile, ama!!??

  ReplyDelete
 2. Yaani we acha tu. Nilikuwa nasoma leo kuhusu kundi la wazazi kule Texas ambao wanapinga watoto wao kwenda kumsilikiza Obama ambaye anategemea kwenda kutoa hotuba huko. Wanasema watoto wao pengine watakwenda kulishwa propaganda za kisoshalisti. We acha tu!

  Cha kushangaza zaidi ni kwamba hata watu masikini ambao hawana bima ya afya nao wanapinga haya marekebisho ya bima anayoyapendekeza. Na ukitaka kuwaogopesha watu hapa basi taja usoshalisti. We acha tu

  ReplyDelete
 3. Siasa za USA ni ngumu,,Pale wanaosema hayo meengi au kumpiga vita ni hao walioshindwa na wale wanaopinga watu weusi,mimi ninavyofikilia kama uchaguzi waweza kufika Obama akiwa amerekebisha mdororo wa uchumi ukaimilika kidogo! baasi hio ndo itampa kula.Hayo mengine waliyaanza hata kipindi alikua bado hajachaguliwa.

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU